Rais Magufuli endapo utarudi madarakani badilika

Rais Magufuli endapo utarudi madarakani badilika

Rufiji dam

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2020
Posts
4,449
Reaction score
10,763
Mheshimiwa Rais kwanza pole na misukosuko ya kampeni za uchaguzi ambapo unajiwinda kurudi tena. Ila mambo sio mepesi, hata kama utashinda ila utakuwa umejifunza la sivyo utakiacha chama chako tabuni sana kipindi ukiondoka. Mungu akuepushe na mipango ovu ya wapambe wako wanaotaka ubaki madarakani, jambo hili hata mimi linanipa hofu kubwa ila mungu akupe hekima na busara ukimaliza muda wako upumzike.

1. Mheshimiwa Rais JPM. Akingalia hali hii ya kampeni zako zimekuwa ngumu sana hasa kwa wasaka tonge kukudanganya juu ya mipango yao ya kujidai wanatokomeza upinzani kwa kununia madiwani na Wabunge, hapa walisahau kitu diwani anachaguliwa na raia je kuna jipya jema ambalo umemtendea raia. Ukirudi acha kuongea kwa kudharau watanzania, punguza chuki na wapinzania.

2. Endapo utarudi, japo najua utarudi tengeneza taifa la wapendwa, acha kutengeneza mipaka ya maendeleo leta kongamano la upendo wa kitaifa uje uhudumu kama baba mzazi. Jukwaani ongea ukifundisha upendo na mshikamano. La sivyo ukiendelea na tabia yako ya dharau utaiacha CCM katika hali mbaya.

3. Ukirudi tena rudisha pesa kwa kwa Wananchi na endesha nchi kwa uwazi sana. Japo napatwa na hofu kuu hasa juu ya wewe kuachia madaraka maana ulisjasema hii miradi mikubwa uliyoanzisha ukiondoka unadhani itaishia hewani na kuna kila dalili mpaka unaondoka hakuna mradi hata mmoja ambao utakuwa umekamilika kwa asilimia 100. Ukidanganywa ucheze na katiba utakuwa umekosea sana mizimu yetu na wazee wetu. Fanya kwa kiasi chako muda ukimalizika ondoka. Ila nakushauri ubaki kuwa mwenyekiti wa CCM ili uweze kumuendesha mgombea uraisi wenu.

4. Naamini kabisa 2023 kuna watu watakuibukia ndani ya chama chako na uenda ukavaa upinzani mkubwa sana maana utakuwa na mwaka mmoja tu wa kuwa raisi. Hivyo nakuomba ubadilishe aina ya mfumo wa kuendesha nchi. Kinachoendelea ni chuki za wazi juu ya mfumo wako wa kuendesha nchi, hii nchi inahitaji kuungwa upya kutokana na mfumo wa uongozi uliofanya.

5. Muite Lissu unywe nae chai...hapa utaishangaza dunia. Lisu analia Lisu kaumizwa najua fika wewe haukuhusika lakini kumbuka mtoto wa jirani kaumia ndani ya nyumba yako. Na wewe baba mwenye nyumba umekaa kimya ebu onyesha kukemea lakini matokeo yake. Wajomba na baba wadogo wanazidi kutoa maneno ya hovyo kwa majeruhi yaliyompata mtoto wa jirani.
Ukirudi mfukuze Polepole na genge lake hawa hawana jema na wewe.

Nakutakia kampeni njema na ushindi mnono.
 
Yote ni sahihi, yote yanawezekana na kwa nia njema.

Siyo wote watafurahia haya yafanyike hasa waliozoea kumpotosha kmna kumsifia. Lakini sasa hali halisi anajionea mwenyewe.

Jambo moja tu ambalo kwake ni ngumu kutimiza na endapo atafanikiwa hata Malaika watamsifu, ni kuupenda upinzani na kukaa meza moja na TL.
 
Nani ka kwambia kuwa magufuli anaweza sikiliza ushauri wa mtu?

Watu aina Ya magufuli sio rahis Kama unavyofikiria kuwa anaweza kumsikiliza mtu akiwa anamshauri, ila umemshauri vizur Sana, hata Mimi nimeliona hilo kuwa Kama akirudi akaendelea na Yale Yale manyanyaso atategeneza taifa lililopasuka na kugawanyika vipande vipande na kutakuwa na vurugu kubwa miaka Yote mitano ya utawala wake na asitegemee CCM 2025 kushinda tena, kutakuwa na vuguvugu la kufa mtu na Mimi ningekuwa Kama wazee wale akina lukuvi ningeachia mapemaaaa mambo ya siasa ili kupona na kinachoenda kutokea huko mbeleni, yani magufuli hata akishinda kutatokea shida kubwa mno huko mbele, kwenye chama chake, Kwan raia, huko serikalini na kwenye vyama vya siasa anatakiwa ajue kuwa katumbukiza taifa kubaya na vijana ndio wanapikwa na chadema hasa hasa wanakuwa wengi na wakudhubutu na Kwa kuwa sasa wameanza kukataa kuonewa, kuna shida mbele
 
kwa sasa hivi hata akishinda asitegemee kuwaamabia watu kuwa siasa basi no, hilo asilitegemee hata tone, hilo nigumu Sana Kwa mazingira Ya sasa, watu hawatakubali na wataongezeka mno kwa kupasa Sauti na kutakuwa na mgawanyiko mkubwa kwenye chama chake maaana anaonesha kutaka kupenyeza issue ya kikabila kwenye chama na kwenye taasisi, magufuli akipita ategemeee misuguano mikali mno Na itakayotoka nje ya nchi na ndani Ya nchi na Nina Uhakika hata wale wasiojulikana wataanza kuogopa kila itakapokuwa inaongezeka misuguano
 
Alishasema yeye ni jiwe tena jiwe kweli kweli.
 
Sikio la kufa halisikii dawa, jamaa ndio lilivyozaliwa Hyu Atashukiwa na Mungu mwenyewe coz ameshupaza shingo sana.

Aonywae mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafla wala hatapata dawa.
Sikio La Kufa Halisikii Dawa
La Kuvunda Halina Ubani
Sikio La Kufa Litasikia Kwa Mungu

Kusikia Kwa Kenge Mpaka Atoke Damu Puani Na Masikioni
 
Ila kuna kitu atajifunza, maana Kama ameanza kuchungulia Picha za lisu za nyomi Ya lisu na kuja kusema kuwa xile ni Picha za 2015 nadhani haaamini kuwa watanzania aliofikiria kuwa wanampenda kiasi cha kuitwa YESU ndio Hawa Hawa?
[emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
18e8ff2e1c344300cc5553e721112f22.jpg
 
Mkuu naona umeanza kukata tamaa ya lisu kushinda[emoji3][emoji3]
Unaweza kuleta ushahidi wa mimi kuona kuwa TAL atashinda?! Ila nachufurahi ni huyu mtu kupata kibano na ajifunze kuishi na wenzake vizuri.
 
Magufuli hawex shinda ndio maaana ameweka kikosi Dodoma cha kuchakachua idadi ya wapiga kura, sasa mtu amewaogopa had wanawake waliojitokeza kuombea ubunge ameagiza wakatwe Kama Yule wa mlimba ndio atashinda?
 
Yote ni sahihi, yote yanawezekana na kwa nia njema.

Siyo wote watafurahia haya yafanyike hasa waliozoea kumpotosha kmna kumsifia. Lakini sasa hali halisi anajionea mwenyewe.

Jambo moja tu ambalo kwake ni ngumu kutimiza na endapo atafanikiwa hata Malaika watamsifu, ni kuupenda upinzani na kukaa meza moja na TL.

Sidhani kama kuupenda upinzani maana yake ni kukaa meza moja na Lissu!

Ni vigumu:
[emoji277]Kukaa kwenye kijiwe kimoja na mtu ambaye kila akipata fursa ya kusema kitu ni kukutukana na kukukashifu tu.
[emoji277]Kupanda mtumbwi mmoja na mtu ambaye ana hila za wazi wazi za kutoboa mtumbwi uzame. Maalim, Lissu na Zitto ni watu ambao wameonesha kwa vitendo utayari wao kufanya chochote ili nchi yao ipate tabu, wakiamini shida watakazozipata wananchi zitawanufaisha wao kisiasa.

Sio dhambi kukaa mbali na mwanasiasa narcissist kama Lissu (mtu ambaye kipaumbele chake ni yeye mwenyewe). The correct order of things ni taifa kwanza, Lissu baadaye (sio Lissu kwanza, taifa baadaye)!
 
Sidhani kama kuupenda upinzani maana yake ni kukaa meza moja na Lissu!

Ni vigumu:
[emoji277]Kukaa kwenye kijiwe kimoja na mtu ambaye kila akipata fursa ya kusema kitu ni kukutukana na kukukashifu tu.
[emoji277]Kupanda mtumbwi mmoja na mtu ambaye ana hila za wazi wazi za kutoboa mtumbwi uzame. Maalim, Lissu na Zitto ni watu ambao wameonesha kwa vitendo utayari wao kufanya chochote ili nchi yao ipate tabu, wakiamini shida watakazozipata wananchi zitawanufaisha wao kisiasa.

Sio dhambi kukaa mbali na mwanasiasa narcissist kama Lissu (mtu ambaye kipaumbele chake ni yeye mwenyewe). The correct order of things ni taifa kwanza, Lissu baadaye (sio Lissu kwanza, taifa baadaye)!
Hivi wewe una akiri kweliii? Yani mtu anaeuwa watu wake na kuteka na kuwwaacha watoto wa watu Yatima unamtetea? Yani magufuli katiri vile unaweza kuwa na ujasiri wa kumtetea mtu katiri Kama Yule? Yani hata Aibu huna? Magufuli kafanya ukatiri hadharani pasipo kificho uje humu kumtetea kuona kuwa akina lisu ndio wabaya? Au kwakuwa hayajakukuta?
 
Back
Top Bottom