Wanabodi,
Naangalia mubashara tukio la kuapishwa kwa mawaziri, kumbe jamaa jana usiku alishinda JF, sasa kikawaida kwenye sherehe za kuapishwa hakunaga hotuba.
Lakini kufuatia rais kufuatia Jamii Forums na kilichosemwa humu kumhusu Mwakyembe,
Hivyo akamuelekeza Msigwa kutoa fursa kwa Mwakyembe asalimie kwa niaba ya wote.
Baada ya salaam za Mwakyembe Mkuu akadokeza kuhusu mitandao ya Kijamii ilivyo ya hovyo, jana ilitangazwa Mwakyembe atagomea uteuzi, hivyo amempa fursa ili watu waone.
This is good, yaani licha ya hii mitandao ilivyo ya hovyo, na hadi kutamani kugeuka malaika na kuifunga lakini bado anaisoma na hadi kubadili protokali.
This is very big impact. Hivyo tuendelee kwa nguvu sana kupeleka ujumbe nyumba kuu kupitia JF, ujumbe utafika.
Paskali