mamayoyo1
JF-Expert Member
- Jul 25, 2018
- 1,011
- 1,019
Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa kusimamia wawekezaji wasisumbuliwe katika uwekezaji wa viwanda.
Rais Magufuli pia amewaomba Watendaji ndani ya Serikali kutowasumbua wafanyabiashara wanaotaka kuwekeza nchini.
"Niwaombe Watendaji ndani ya Serikali tusiwasumbue wafanyabiashara wanaotaka kuwekeza nchini,Waziri Bashungwa wewe bado kijana kasimamie hili Wawekezaji wasisumbuliwe, katika uwekezaji wa viwanda tutumie teknolojia za kawaida ambazo ni rahisi kwa watu wetu kujifunza," amesema leo Rais Magufuli wakati akizundua kiwanda cha Mohamed Enterprises.
"Viwanda ndio muhimili mkuu wa maendeleo ya uchumi, hakuna Taifa duniani linaloweza kufanya mageuzi ya haraka kiuchumi bila kuendeleza sekta ya viwanda tukiwa na viwanda vya kimkakati kwa mazao ya kimkakati tunaweza kusindika mazao yetu na kuzalisha bidhaa zilizokamilika."