Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SUMATRA

Tengua teua tengua teua tengea tena halafu teua tena.

Mwisho wa siku alietenguliwa Dodoma atateuliwa Mwanza maana hawezi kuwakumbuka aliowatengua.
 
Hii ngoma Sumatra hawaikwepi lazima wawajibike,

Abiria kupanda chombo cha Majini bila Life Jackets ni uzembe wa hali ya juu.

Ule ndiyo usalama wako ikitokea ajali ya kwenye Maji,vyombo vyote vinavyofanya safari za kwenye maji ni wajibu sasa kuwapatia abiria hizo Life Jackets kabla ya kuanza safari.
SUMATRA haihusiki kabisa hapo. SUMATRA inatekeleza sheria inayoitwa Mechant shipping act sheria haigusi kabisa vyombo vya serikali wala sumatra haina mamlaka juu ya ferries na watumishi wake kwa maana ya taaluma zao. Ferries za serikali zinasiamiwa na sheria nyingine sijui inaitwa nini huko ferries cap 73 sijui nimepatia na waziri mwenye dhamana ndo mwenye mamlaka ya kutunga regualations juu ya usimamizi wa vivuko jambo ambalo sijui kama ameshawahi kufanya hivyo. Kwa hiyo kuwarukia SUMATRA ni sinema zilezile tu za kila siku
 
Hata angetumbua kuanzia watendaji wote wa vijiji, kata tarafa wilaya mkoa haisadii chochote. Hii ni system ILIYOPARALAIZI. Hivyo uchumi na maendeleo ,siasa, diplomasia na demokrasia na kila kitu kimeparalaizi. Nionyeshe jambo walau moja tu la maana tulilofanya km taifa tukafanikiwa .Tukasema hili tumelifanya kwa ukamilifu wake na matunda yake yakaonekana.
 
kazi ya utumishi wa umma ni changamoto.... kifaa chenyewe kilikuwa hoi, idadi ya wahitaji ni kubwa kuliko huduma. Kwa nini tusinunue vivuko vingine vilivyo imara na vyenye kukidhi mahitaji, kuliko kusubiri matukio ndio tutafute mchawi. Mbunge wa eneo hilo alishaomba sana na hata kutoa tahadhari, serikali ilichukua hatua gani?

Kwa maamuzi haya, inastahili viongozi wote wenye dhamana akiwemo waziri husika wajiuzulu au watumbuliwe kuonyesha uwajibikaji, tofauti na hapo ni kuwaonea watumishi wa chini kwani taarifa za ubovu wa kivuko hicho zilishatolewa na hakuna cha maana kilichofanyika.

Kama hatutaukubali ukweli wa makosa yetu ila tukadhani njia nzuri ni kumtafuta nani wa kumtupia zigo afe nalo, basi kazi itakuwa ni kutumbua na kuteua kila siku.

Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, amina.
 
Kukitokea ajali, mwenye mamlaka ya kuzuia zisitokee ajali anawajibika. Ila kama ni kweli Sumatra hawana mamlaka ya kusimamia usafiri wa vivuko basi kutakuwa na mushkeri.

Proactive action ni muhimu. Asiyetimiza wajibu wa kuzuia mabaya na atumbuliwe tu. Hatuna namna. Tumelala vya kutosha. Sasa ni mboko tu.
 
Mtendaji Kuu wa TEMESA vipi?? Meneja Temesa MWanza vipi? Waziri Wa Miundombinu vipi?? Ushauri Mbunge Ukerewe ulifanyiwa kazi? Kuvunja bodi sio suluhisho!! ...............nunua vivuko vyote acheni kununua wapinzani!
Mzee baba kama uko sehemu ya kinywaji a giza ntakuja kulipia

Ova
 
Back
Top Bottom