Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SUMATRA

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Mhandisi Dkt. John Ndunguru na kuivunja bodi hiyo kuanzia tarehe 24 Septemba, 2018.

Mhe. Rais Magufuli amechukua hatua hiyo kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 Septemba, 2018 na matukio mbalimbali ya ajali za barabarani hapa nchini yanayosababisha vifo, ulemavu na uharibifu wa mali.

Pamoja na hatua hiyo kamati ya uchunguzi ambayo itatangazwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa baadaye leo, itaendelea na uchunguzi wa ajali ya kivuko cha MV Nyerere kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kama ilivyopangwa.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

24 Septemba, 2018
Dn1WLtWX0AAkW-f.jpg large.jpg
 
Rais John Pombe Magufuli, ametengua Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Maji na Nchi Kavu (SUMATRA), John Ndunguru
Sasa kamtimua mkurugenzi au kavunja bodi wa wakurugenzi??

Au wewe unaona yote ni kitu kimoja??
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom