Rais Magufuli atengua uteuzi wa DCI, Diwani Athuman

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
2,436
4,429
Kuna habari kuwa DCI ametenguliwa uteuzi wake.

fcf419f0-f30a-4b6a-911e-e1cdbe179899-jpg.426145


Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (Director of Criminal Investigation – DCI), Diwani Athuman Msuya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Rais Magufuli ametengua uteuzi huo leo.

Bila kutoa ufafanuzi wa sababu za mkuu huyo wa nchi kuchukua hatua hiyo, taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa Athuman atapangiwa kazi nyingine.

“Kufuatia uamuzi huo, uteuzi wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai utatangazwa baadaye,” imeeleza sehemu ya taarifa kutoka Ikulu.
 
Daaaah mkuu huyu atakuwa alidanganya.....

Kwenye vetting za baadhi ya wateule wa rais .......

Swala la kushindwa kesi nyingi kwa serikali nalo laweza kuwa tatizo....

Kwa Mara ya kwanza rais amefanya jambo la umakini .....

Siku zote tunatakiwa kupambana na chanzo cha tatizo sio tatizo.......
 
Back
Top Bottom