Rais Magufuli ataweza kurejesha Azimio la Arusha? Tujadili

KooZito

JF-Expert Member
Dec 14, 2020
396
1,377
Ukijaribu kuona aina ya uongozi wa Rais Magufuli na hata anavyojinasibu kupitia kwa wapambe wake ni kwamba anaenenda kama Rais wa kwanza Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere.

Miongoni mwa Mambo aliyoanzisha Nyerere ni pamoja na Azimio la Arusha lililotaka watumishi wa umma kutenganisha utumishi wao na mali kwa maana ya kuachana na biashara. Kwamba, mfano wewe ni waziri usimiliki biashara ili kuepuka mgongano wa kimaslahi litakapokuja suala uamuzi katika biashara hiyo.

Lakini tunachokishuhudia leo ni kila kiongozi wa umma na chama kumiliki biashara kubwa kubwa wengine kwa majina yao halisi wengine kwa majina ya ndugu zao na mifano iko tele.

Ninaamini hata fomu watakazojaza za mali wanazomiliki ni uongo mtupu. Hivi mfano, Waziri Mwigulu ataandika kumiliki mabasi ya Esther? Hapana, atadai ni za mkewe nakadhalika.

Baraza la Mawaziri ndio washauri wakuu wa Rais. Ni Waziri yupi atamshauri Rais kurejesha sera za Ujamaa na matakwa ya Azimio la Arusha? Je, naye Magufuli ataonesha mali zake zote? Je, hafanyi biashara ya ujenzi? Je, huku kupora kwa nguvu fedha za watu kwenye mabenki ndio tangazo la uhujumu uchumi alipotoa Edward Moringe Sokoine?

Mwl Nyerere alisalimu amri kwa "wakubwa" kwa sera hizi za ki-Azimio la Arusha kwa sababu alijikuta anahubiri yeye na waumini ni yeye huyo huyo. Waliomzuka hawakuamini wala kusadiki injili hiyo. Kwa nini Magufuli hajifunzi? Hivi hajui waliomzunguka wanamng'ong'a tu? Wanamuabudi kinafiki?

Naomba kuwasilisha.
 
Mtu aliezungukwa na mambo mengi kama kina Mayanga Construction na ameshindwa kuyatolea ufafanuzi, anayekataza wasaidizi wake wasitumie V8 wakati yeye anatumia kwenye misafara yake, hawezi kusimamia kurejesha Azimio la Arusha.
 
Huwezi maliza ufisadi hali we ni fisadi.
Esther luxury coach dar kiomboi, Chato beach resort, mayanga construction.
We lipa Kodi inatumikaje usihoji utawabip wasiojulikana.
 
Back
Top Bottom