Rais Magufuli atangaza Baraza Jipya la Mawaziri - 10 Disemba 2015

baada ya jpm kuanza kwa kasi na sera yake ya hapa kazi tu tayari ameanza kuonyesha kuishiwa na pumzi.
Hii imeonekana leo kufuatia tangazo lake la baraza la mawaziri.

Watanzania hawakutegemea kuona na kusikia majina na sura za mawaziri waliokuwemo kwenye baraza la awamu ya 4 ya rais wa chalinze.

Watanzania tulitegemea jpm aje na sura mpya na tofauti za wachapa kazi wenye kulingana na kasi yake. Hii inaonyesha kwamba magufuli ameanza kushindwa na mfumo wake wa ccm na hasa baada ya kutishwa juzi kwenye kikao cha kamati kuu ya ccm iliyomwonya kwamba anapotumbua majipu lazima kwanza ajiridhishe hilo jipu limekaa kaaje maana kuna majipu mengine yako kwenye sehemu za makalio, sehemu nyeti n.k.

Siamin masikio yangu kusikia jina kama prof. Muhongo aliyeingia kwenye kashfa ya escrow account wakti akiwa waziri wa nishati na madini na karudishwa hapohapo. Mtu kama mwigulu nchemba hangestahili wala kupashwa kurudi kwenye uwaziri kwani yeye pamoja na waziri wake wa fedha inaonyesha walishindwa kusimamia tra na bandari katika kukusanya mapato ya serikali na kwa maana hiyo ni sehemu ya tatizo.

Dk. Mwakyembe pamoja na mbwembwe zake hakuna alichofanya wakti wa kiwete huko bandari na trl ambako kumekutwa madudu lukuki. Hivyo mwakyembe hakustahili kuwemo kwenye baraza hili la jpm.

Kwa mtaji huu inaonekana mambo yatakuwa ni yaleyale ya ccm ni ile ile.

Hakuna mabadiliko ccm.


nenda kale malimau kwanza ili uweze kuondoa ukakasi! Mtajibeba mwaka huu..katatueni mgogoro wa madiwani ilala....tafuteni muelekeo mpya wa kuwaonyesha watanzania kuwa nyinyi ni wana siasa...kwa kifupi chadema mmeshafilisika kimtaji wa siasa na kimvuto kwa wananchi wa tz.... Namba mtazisoma kweli kweli ....na mtapata mateso bila chuki...
 
Sijui mnafaidikaje kuendeleza uhasama kwenye Jamii. Ningekuona ww sio kenge endapo ungetoa ushauri wakamalize bifu zao offline.
Watanzania wanataka mabadiliko
 
Mshaaza kuleta miuzi yenu ya ajabu ajabu,nyalandu hata asijaribu kwa jpm,hawezi kasi yake,bottom line sio msafi
 
Mkuu nimeshangaa kuona Mwakiembe anarudi huku aliyekuwa katibu mkuu wizara yake bw. Mwinjaka kapigwa chini kwa kashfa ya ubadhirifu
 
Kusema kweli kwa hali ya siasa ndani ya ccm ilivyo Mh rais kajitahidi sana na kwa maneno mengine amekua na ujasiri mkubwa kuja na baraza hili la mawaziri dogo na likiwa na mawaziri wachache sana wa zamani. Naamini amepata mashinikizo ya watu mbalimbali na ameyashinda.
 
nlisema sio chuki na mh magufuli sasa yote yamedhihika.

waziri wa nishati~mtuhumiwa wa escrow

waziri wa habari~tutafunga bao la mkono

waziri wa kilimo~alishindwa kusimamia bandari na tra.

waziri wa katiba~ alishindwa kusimamia TRL

January makamba~alishindwa kuzidhibiti kupitishwa sheria mbovu za cybercrime adi desemba MCC hawatoi hata senti.

Ngonyani~ hapa ndio nimechoka kabisa nahisi kuna sayansi Fulani inapigiwa promo

bado tutamsifia magufuli? think criticallyu
 
Nimeangalia baraza jipya la mawaziri Rais Magufuri amejaribu kuteua kufuata kanda kwa kugusa mikoa na kanda mbalimbali, pamoja na mikoa ya Tabora na Kigoma kuachana na vyama vya uoinzani lkn mikoa hiyo imetoa waziri mmoja ambaye ni Dr. Hamis Kigwangala. Hongereni Tabora na Kigoma.
 
Wanajamvi,

Nimeogopeshwa sana na Mkuu wa Kaya kwa staili ya majibu kwa waandishi wa habari, hali hii nasikitika kuwa ni ishara mbaya kwa uhuru wa habari huko mbeleni.

Mzee amewajibu waandishi kama kwamba waandishi ni maadui hivi badala ya kuwaona kama partners katika kuwahabarisha Watanzania Mustakbali wa nchi yao.

Nimejawa na hofu kwamba isije ikawa ule Uhuru wa habari ambao watanzania tumeufikia na kuuenjoy ukageuka kuwa kizungumkuti katika serikali hii.

Ni vyema Mzee akanong'onezwa kuwa presentation matters, Japo kweli tunahitaji Kazi, lakini "Dignity" ya Stakeholders mbalimbali ikalindwa na kuheshimiwa!

Mkuu hata mimi huo udhaifu wa kujibu kwa mkato hata mimi nimeuona. sitarajii rais kuwa anajibu kwa style hii kama tutafika salama huko tuendako. Nadhani mahali penye maswali magumu na panapohitaji maelezo ya kina tutakutana na majibu ya dhihaka na udhaifu mwingine mwingi kama huo. Yetu macho.
 
Back
Top Bottom