Jollie
Member
- Jul 26, 2019
- 35
- 64
Rais wa Tanzania, John Magufuli amemtaka Rais wa Yoweri Museven wa Uganda kuwa mkali kwa watendaji wake ambao wanakwamisha kuanza kwa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini humo mpaka Tanga, Tanzania.
Magufuli ametoa mfano wakati alipoingia madarakani Novemba 5, 2015 alibadilisha makamishna wakuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) watano lengo ni kuongeza ufanisi katika mamlaka hiyo.
Akizungumza wakati wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika leo Ijumaa Septemba 6, 2019 jijini Dar es Salaam, Tanzania, Magufuli amesema Serikali yake ilifanya mabadiliko ya sheria ili kupunguza sehemu ya kodi kwa ajili ya mradi huo.
Amemtaka pia Rais Museven kuchukua hatua nchini kwake kwa kuwa tayari kupoteza kidogo kama Tanzania ilivyofanya ili apate kikubwa zaidi.
Pia, amemshauri kama watendaji wake ndiyo kikwazo asisite kuwaondoa na kuweka wengine.
“I wish (ninatamani) hawa watendaji wa Tanzania wangeenda Uganda na wa Uganda waje Tanzania ili ni-deal (nishughulike) nao angalau kwa mwezi mmoja tu,” amesema Rais Magufuli huku washiriki wa mkutano huo wakicheka.
Amewataka watendaji katika nchi za Uganda na Tanzania wahakikishe wanafanikisha miradi mikubwa ambayo inatengeneza ajira nyingi. Amesema watendaji wengi hawajali kwa sababu wanapata mishahara.
Kwa upande wake, Rais Museven amewataka wafanyabiashara kujadiliana kwa kina na kujibu swali linalouliza “utajiri wa mataifa unatoka wapi?” kama lilivyoulizwa na Adam Smith kwenye kitabu chake cha Wealth of Nations (Utajiri wa Mataifa).
Museven amesema suala la miundombinu ni muhimu katika kurahisisha biashara baina ya mataifa hayo kwa sababu gharama za usafirishaji wa kontena kutoka bandari ya Dar es Salaam kwenda Port Berry itakuwa Dola za Marekani 1600 badala ya Dola 4500 za sasa.
Kiongozi huyo alimhakikishia Rais Magufuli kwamba serikali yake itahakikisha bomba la mafuta linajengwa na mafuta ambayo yamekuwepo kwa miaka milioni mbili iliyopita yanapatikana kwa maendeleo ya wananchi.
Chanzo: Mwananchi