Rais Magufuli ataka Rais Museveni kuwa mkali kwa watendaji wake

Nimemsikia pia.

Ila hili swala la kuingilia nchi nyingine na kuonyesha kana kwamba hawafanyi kazi vizuri kwa kweli siyo uungwana. Tanzania bado ina mapungufu mengi sana katika utendaji chini ya awamu hii. Kubadilisha Commissioners wa TRA haina maana kwmba utendaji umekuwa mzuri. Mfano haukuwa sahihi hata kama ulikuwa ni utani tu haukuwa mahali pake!!
Ufipa mna angalia pakutokea ni wapi !
 
Mambo kama hayo nadhani yalistahili kuzungumzwa faragha. Kumkosoa Rais mwenzako hadharani namna hiyo, nadhani haikuwa poa.
Exactly huyu Magufuri amelewa madaraka anadhani kila anayeongea naye yuko chini yake. Hizi ni athari za mtu anayeishi kwenye nchi ambayo uhuru wa maoni umekandamizwa
 
Rais wa Tanzania, John Magufuli amemtaka Rais wa Yoweri Museven wa Uganda kuwa mkali kwa watendaji wake ambao wanakwamisha kuanza kwa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini humo mpaka Tanga, Tanzania.

Magufuli ametoa mfano wakati alipoingia madarakani Novemba 5, 2015 alibadilisha makamishna wakuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) watano lengo ni kuongeza ufanisi katika mamlaka hiyo.

Akizungumza wakati wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika leo Ijumaa Septemba 6, 2019 jijini Dar es Salaam, Tanzania, Magufuli amesema Serikali yake ilifanya mabadiliko ya sheria ili kupunguza sehemu ya kodi kwa ajili ya mradi huo.

Amemtaka pia Rais Museven kuchukua hatua nchini kwake kwa kuwa tayari kupoteza kidogo kama Tanzania ilivyofanya ili apate kikubwa zaidi.

Pia, amemshauri kama watendaji wake ndiyo kikwazo asisite kuwaondoa na kuweka wengine.

“I wish (ninatamani) hawa watendaji wa Tanzania wangeenda Uganda na wa Uganda waje Tanzania ili ni-deal (nishughulike) nao angalau kwa mwezi mmoja tu,” amesema Rais Magufuli huku washiriki wa mkutano huo wakicheka.

Amewataka watendaji katika nchi za Uganda na Tanzania wahakikishe wanafanikisha miradi mikubwa ambayo inatengeneza ajira nyingi. Amesema watendaji wengi hawajali kwa sababu wanapata mishahara.

Kwa upande wake, Rais Museven amewataka wafanyabiashara kujadiliana kwa kina na kujibu swali linalouliza “utajiri wa mataifa unatoka wapi?” kama lilivyoulizwa na Adam Smith kwenye kitabu chake cha Wealth of Nations (Utajiri wa Mataifa).

Museven amesema suala la miundombinu ni muhimu katika kurahisisha biashara baina ya mataifa hayo kwa sababu gharama za usafirishaji wa kontena kutoka bandari ya Dar es Salaam kwenda Port Berry itakuwa Dola za Marekani 1600 badala ya Dola 4500 za sasa.

Kiongozi huyo alimhakikishia Rais Magufuli kwamba serikali yake itahakikisha bomba la mafuta linajengwa na mafuta ambayo yamekuwepo kwa miaka milioni mbili iliyopita yanapatikana kwa maendeleo ya wananchi.

View attachment 1199967

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu mzee korosho imemshinda, mafuta ataweza? Lipi ameliweza angalau kwa 60% katika nchi hii??
Shwaaain zake huko.
 
Huyo mzee wenu alikataa kupangiwa kazi zake lakini yeye kila kukicha anataka kuwaingilia wenzake kwenye kazi zao. Ipo siku atamshauri Trump namna ya ku deal na wachina.
 
Unajua wewe Mzee Museveni TRA wako wanakukwamisha...
Huyu mtu ilibidi afundishwe mambo mengi ingawa yeye anadhani anajua kila kitu
 
Sina hakika kama ni hiyo Mamlaka inakwamisha ama ni sheria za nchi? Hivi M7 amesemaje kuhusu hilo?
 
Ukali wake yeye umesaidia nini mpaka sasa hivi? Mbona nchi inaliwa kama kawa.
 
Yeye na ukali wake umesaidia nini kuleta maendeleo kwenye utawala wake toka ameingia madarakani.
 
Nimemsikia pia.

Ila hili swala la kuingilia nchi nyingine na kuonyesha kana kwamba hawafanyi kazi vizuri kwa kweli siyo uungwana. Tanzania bado ina mapungufu mengi sana katika utendaji chini ya awamu hii. Kubadilisha Commissioners wa TRA haina maana kwmba utendaji umekuwa mzuri. Mfano haukuwa sahihi hata kama ulikuwa ni utani tu haukuwa mahali pake!!
Kwa kuwa ni zero basi naishia hapa
 
Magufuli is a country bumpkin.

No tact, no diplomacy.

Cha ajabu zaidi, yeye bingwa wa kusema hataki kupangiwa, ni wa kwanza kupangia wenzake.

Kiitifaki na kidiplomasia hapo kaharibu sana, ni kama anamfundisha rais mwenzake jinsi ya kufanya kazi kwa kusema yeye Magufuli anajua kazi ya urais zaidi.
 
Ona sasa ulivyo mjinga! Wenzio wameongelea suala la utendaji ili hilo Bomba likamilike wananchi wapate ajira, wewe unaleta Habari za majenerali?
Unafikiri pale alikuwa ni ccm na chadema au Magufuli na Membe pale?

Huyo Museveni ni tapeli tu, aliwahi kupewa bandari ya Tanga baada ya kuomba aindeleze ili mizigo ya Uganda ishukie hapo lakini mpaka leo ni hadithi. Hilo bomba kashaongea mpaka na Uhuru kwamba atalipitisha Kenya mara kabadilika analipitisha Tanzania. Huyo huyo Museveni walikuwa na umoja wao ndani ya E. Afrika wao Kagame na Uhuru enzi za JK, yote waliyokubaliana imekuwa ni hadithi.

Hata wakati Magufuli anakwenda kuzindua hilo bomba kwa mbwembwe kule Tanga na kutaja kama sehemu ya mafanikio ya utawala wake, tulisema anaingizwa mjini na Museveni. Leo hii utapeli wa hilo bomba uko wazi na usishangae akaamua alipitishie Kenya. Hata haya yaliyomleta sasa hivi hapa nchini ni nini kama sio porojo? Uganda na Tanzania zipo East Afrika, ni kipi wameshindwa kujadili wakiwa kwenye jumuiya, hadi leo hivi inakuwa kuna biashara ya Tanzania na Uganda tu? Huu mchezo si unataka kuwa ule ule wa coalition of the willing iliyovunjika?
 
Back
Top Bottom