Rais Magufuli ataka Rais Museveni kuwa mkali kwa watendaji wake

Jollie

Member
Jul 26, 2019
35
64
Rais wa Tanzania, John Magufuli amemtaka Rais wa Yoweri Museven wa Uganda kuwa mkali kwa watendaji wake ambao wanakwamisha kuanza kwa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini humo mpaka Tanga, Tanzania.

Magufuli ametoa mfano wakati alipoingia madarakani Novemba 5, 2015 alibadilisha makamishna wakuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) watano lengo ni kuongeza ufanisi katika mamlaka hiyo.

Akizungumza wakati wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika leo Ijumaa Septemba 6, 2019 jijini Dar es Salaam, Tanzania, Magufuli amesema Serikali yake ilifanya mabadiliko ya sheria ili kupunguza sehemu ya kodi kwa ajili ya mradi huo.

Amemtaka pia Rais Museven kuchukua hatua nchini kwake kwa kuwa tayari kupoteza kidogo kama Tanzania ilivyofanya ili apate kikubwa zaidi.

Pia, amemshauri kama watendaji wake ndiyo kikwazo asisite kuwaondoa na kuweka wengine.

“I wish (ninatamani) hawa watendaji wa Tanzania wangeenda Uganda na wa Uganda waje Tanzania ili ni-deal (nishughulike) nao angalau kwa mwezi mmoja tu,” amesema Rais Magufuli huku washiriki wa mkutano huo wakicheka.

Amewataka watendaji katika nchi za Uganda na Tanzania wahakikishe wanafanikisha miradi mikubwa ambayo inatengeneza ajira nyingi. Amesema watendaji wengi hawajali kwa sababu wanapata mishahara.

Kwa upande wake, Rais Museven amewataka wafanyabiashara kujadiliana kwa kina na kujibu swali linalouliza “utajiri wa mataifa unatoka wapi?” kama lilivyoulizwa na Adam Smith kwenye kitabu chake cha Wealth of Nations (Utajiri wa Mataifa).

Museven amesema suala la miundombinu ni muhimu katika kurahisisha biashara baina ya mataifa hayo kwa sababu gharama za usafirishaji wa kontena kutoka bandari ya Dar es Salaam kwenda Port Berry itakuwa Dola za Marekani 1600 badala ya Dola 4500 za sasa.

Kiongozi huyo alimhakikishia Rais Magufuli kwamba serikali yake itahakikisha bomba la mafuta linajengwa na mafuta ambayo yamekuwepo kwa miaka milioni mbili iliyopita yanapatikana kwa maendeleo ya wananchi.

IMG_2220.JPG

Chanzo: Mwananchi
 
Nimemsikia pia.

Ila hili swala la kuingilia nchi nyingine na kuonyesha kana kwamba hawafanyi kazi vizuri kwa kweli siyo uungwana. Tanzania bado ina mapungufu mengi sana katika utendaji chini ya awamu hii. Kubadilisha Commissioners wa TRA haina maana kwmba utendaji umekuwa mzuri. Mfano haukuwa sahihi hata kama ulikuwa ni utani tu haukuwa mahali pake!!
 
Hakuna ubaya wowote na hakumlazimisha na hata uwezo huo hana ila alichokifanya ni Kumshauri tu kama Rais mwenzie ili waweze kwenda sambamba na Kuyawahi Maendeleo wanayoyataka ya huu Ukanda wetu. Tupunguze sana Chuki kwa Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Magufuli kwa kila alifanyalo au alisemalo japo hata Yeye kama Mwanadamu tulivyo Mimi na Wewe ana Mapungufu yake pia ila tumsaidie badala ya Kumsakama mara kwa mara.
 
Hakuna ubaya wowote na hakumlazimisha na hata uwezo huo hana ila alichokifanya ni Kumshauri tu kama Rais mwenzio ili waweze kwenda sambamba na Kuyawahi Maendeleo wanayoyataka ya huu Ukanda wetu. Tupunguze sana Chuki kwa Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Magufuli kwa kila alifanyalo au alisemalo japo hata Yeye kama Mwanadamu tulivyo Mimi na Wewe ana Mapungufu yake pia ila tumsaidie badala ya Kumsakama mara kwa mara.
Nimemshangaa Mr. Zero
 
Hapo ndio rais wetu anakosea. Huwezi kumwambia rais wa nchi nyingine aongoze nchi yake unavyotaka wewe tena mbele ya hadhara.

Museven mwenye uzoefu wa uongozi miaka 3u aje kuelekezwa namna ya kuongoza na mtu mwenye uzoefu wa miaka 3? Hata kama ila sio kwa mtindo huo.
 
Hakuna ubaya wowote na hakumlazimisha na hata uwezo huo hana ila alichokifanya ni Kumshauri tu kama Rais mwenzio ili waweze kwenda sambamba na Kuyawahi Maendeleo wanayoyataka ya huu Ukanda wetu. Tupunguze sana Chuki kwa Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Magufuli kwa kila alifanyalo au alisemalo japo hata Yeye kama Mwanadamu tulivyo Mimi na Wewe ana Mapungufu yake pia ila tumsaidie badala ya Kumsakama mara kwa mara.
Hadharani ndio busara????
 
Mapungufu na Fundisho la sakata la mradi wa bomba la mafuta Hoima Uganda mpaka bandari ya Tanga, Tanzania :

Na hata mradi mkubwa wa mamilioni ya dola za Kimarekani wa reli mpya ya SGR utakwama kutokana na kutegemea wateja wa Uganda, kaskazini ya mashariki DR Congo na Rwanda maana wana mbadala wa wapi wapitishe mizigo au waingize wapi fedha wapi mfano reli ya SGR Tanzania au watumie barabara iliyopo mpaka Mombasa.

Miradi mikubwa ilenge soko, migodi na viwanda vya ndani vipya na vilivyopo vya Tanzania na ikitokea majirani wakaona faida ya kuitumia basi hilo ni la ziada lakini focus ya miradi mikubwa ya barabara na reli iwe kwanza kwa faida ya Tanzania.
 
Nimemsikia pia.

Ila hili swala la kuingilia nchi nyingine na kuonyesha kana kwamba hawafanyi kazi vizuri kwa kweli siyo uungwana. Tanzania bado ina mapungufu mengi sana katika utendaji chini ya awamu hii. Kubadilisha Commissioners wa TRA haina maana kwmba utendaji umekuwa mzuri. Mfano haukuwa sahihi hata kama ulikuwa ni utani tu haukuwa mahali pake!!
Wewe unategea vyanzo vya Habari toka sehemu zisizo aminika mwenzio Jiwe ana vyanzo vyake hadi pale Ikulu so pengine anajua huo mradi unakwama kwa sababu gani
 
Back
Top Bottom