Rais Magufuli aongezewe Ulinzi

TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
4,305
2,559
Naviomba vyombo vya ulinzi nchini vimwongezee ulinzi rais Magufuli,apewe ulinzi mkali wa wanajeshi kutoka vikosi maalum waambatane naye popote anapokwenda kufanya ziara.

Hatua anazozichukua za kupambana na kila aina ya ufisadi dhidi ya fedha za umma na rasilimali za taifa zinaweletea maumivu baadhi ya watu,zinawafanya wapoteze ulaji waliouzowea,wanachukizwa na wanaweza kufanya lolote.

Tunaomba rais aimarishiwe ulinzi mzito.
"Hotuba hii ya Rais Magufuli ni moja ya hotuba bora kabisa katika historia ya siasa za Tanzania."

Hili lilikuwa hitimisho langu katika mtandao wa kijamii wa Twitter mara baada ya Rais John Magufuli kumaliza kulihutubia Bunge wiki iliyopita, huko Dodoma.

Na kwa hakika watu kadhaa waliafikiana na hitimisho hilo. Kilichovutia wengi waliosikia hotuba hiyo, katika shughuli ya ufunguzi wa Bunge la 11, sio tu mpangilio wa hotuba yenyewe bali pia jinsi kila alilotamka lilivyoonyesha bayana kuwa lilitoka moyoni mwake kwa dhati kabisa.

Rais alianza hotuba yake hiyo kwa kuorodhesha matatizo mbalimbali aliyobaini wakati wa kampeni zake za urais ambapo alizunguka takriban Tanzania nzima. Alitoa uchambuzi wa kina wa matatizo hayo kabla ya kuelezea kwa undani ni kwa jinsi gani serikali yake itayashughulikia. Ilikuwa ni zaidi ya hotuba ya kisiasa, na pengine ingeweza kabisa kuwa mhadhara wa kitaaluma uliofanyika katika lugha nyepesi na ya kueleweka.

Moja ya vitu vilivyonivutia sana katika hotuba hiyo ni jinsi Rais Magufuli alivyoweza kutupatia jibu la swali ambalo kwa miaka kadhaa lilionekana kuwatatiza viongozi wetu mbalimbali: ?Kwa nini Tanzania ni masikini licha ya utajiri lukuki wa rasilimali ilionao.? Alieleza bayana na kwa kirefu jinsi ufisadi, rushwa na uhalifu vinavyochangia kukwamisha maendeleo ya taifa letu.

Kadhalika, alifafanua, kwa kutumia takwimu halisi, jinsi mabilioni ya fedha yalivyotumika visivyo kwa matumizi yasiyo muhimu na yaliyo nje ya uwezo wa taifa letu masikini.

Kwa hakika ilikuwa hotuba ya kihistoria iliyofunika kabisa utovu wa nidhamu wa hali ya juu ulioonyeshwa awali na wabunge wa upinzani ambao walitumia muda mwingi kabla ya hotuba hiyo kuzomea na baadaye kuamiriwa kutoka nje ya ukumbi huo.

Lakini kwa vile sio rahisi kumridhisha kila mtu, baadhi ya wenzetu waliosikiliza hotuba hiyo walidai kuwa eti ?haina tofauti na hotuba nyingine kadhaa zilizokuwa nzuri kuzisikiliza lakini zikaishia kuwa maneno matamu tu.? Wengine walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa hata mtangulizi wa Rais Magufuli, Jakaya Kikwete naye pia alianza urais wake kwa hotuba za kutia moyo kama hizo lakini mengi ya aliyoahidi, hususan lile la ?Maisha Bora kwa Kila Mtanzania,? yaliishia kuwa ahadi tu.

Sikubaliani na wakosoaji hao, japo hoja zao zinaweza kuwa na mantiki kidogo. Ni kweli kwamba ukosefu wa hotuba za kuvutia si moja ya matatizo yanayoikabili nchi yetu. Wengi wa wanasiasa na viongozi wetu ni mahiri sana wa maneno lakini tatizo huwa katika kutafsiri maneno yao kuwa vitendo.

Wakosoaji hao hawapo sahihi kwa sababu, kama nilivyoeleza awali, hotuba hiyo ilikuwa ya kutoka moyoni.Ilikuwa hotuba ya kiongozi anayeguswa na yanayoisibu nchi yake, kiongozi mwenye uelewa wa changamoto zinazoukabili uongozi wake, na mwenye dhamira thabiti ya kukabiliana na changamoto hizo.

Kuna mbinu moja muhimu ya kubaini iwapo mtu anaongea ukweli au anahadaa, nayo ni kumwangalia usoni. Tangu kuanza kwa kampeni zake za urais na hadi wakati wa hotuba hiyo ya wiki iliyopita, uso wa Rais Magufuli wakati anaongea unaonyesha bayana kuwa kila neno linalotoka mdomoni mwake ni la dhati, linatoka moyoni na si sehemu ya porojo tulilozoea kutoka kwa wengi wa wanasiasa na viongozi wetu. Mtaalamu yeyote wa kubaini ukweli na uongo hatoshindwa kuafikiana nami kuwa uthabiti wa kauli za Magufuli upo wazi kwa yeyote anayemwangalia usoni wakati anaongea.

Lakini pia, hotuba hiyo ilikuwa mwendelezo wa ishara nzuri zilizoanza kujitokeza siku moja tu tangu Rais Magufuli aingie ofisini, ambapo alifanya ziara ya kushtukiza Wizara ya Fedha, kabla ya kufanya ziara nyingine kama hiyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Na siku ya uzinduzi wa Bunge, alitukumbusha enzi za (Waziri Mkuu wa zamani) hayati Edward Sokoine, aliyesifika kwa uchungu wa mali za umma, baada ya kuamuru zaidi ya shilingi milioni 200 zilizochangwa kwa ajili ya hafla ya mchapalo ya sherehe za uzinduzi wa Bunge jipya zielekezwe kwenye ununuzi wa vitanda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, na kiasi kidogo tu kitumike kwa ajili ya hafla hiyo.

Kihesabu, chini ya wiki tatu tangu aingie madarakani, Rais Magufuli amekwishaokoa jumla ya shilingi milioni 900 kutokana na hatua alizochukua dhidi ya matumizi yasiyo ya lazima. Kwa kasi hii, tuna kila sababu ya kutarajiwa kuiona nchi yetu ikipaa kiuchumi, na hatimaye Watanzania kunufaika na neema lukuki ambayo nchi yetu imejaaliwa kuwa nayo.

Sina shaka kuhusu uwezekano wa mafanikio ya hatua za Rais Magufuli huko serikalini. Licha ya kuwa na Waziri Mkuu mchapakazi mzoefu, Majaliwa Kassim Majaliwa, kuna kila dalili kuwa baraza la mawaziri ambalo hadi wakati ninaandaa makala hii lilikuwa halijatangazwa, litasheheni wachapakazi kama yeye. Kwa hiyo, kazi ya kurejesha nidhamu serikalini, kupunguza matumizi yasiyoendana na umasikini wetu na kupambana na ufisadi ina dalili kubwa za mafanikio.

Eneo ambalo Rais Magufuli hawezi kufanikiwa peke yake pasipo ushirikiano wa Watanzania wote ni nje ya serikali na huko mtaani. Mara kadhaa nimekuwa nikisisitiza umuhimu wa wananchi kujenga kasumba ya kudai haki na stahili zao badala ya kuona haki/stahili hizo ni kama fadhila au upendeleo flani. Wenzetu huku Ughaibuni wamejenga desturi ya kutokubali huduma au bidhaa inayotolewa chini ya kiwango wanachostahili. Haki na stahili za mpokea huduma ni miongoni mwa vitu vinavyopewa umuhimu mkubwa huku tulipo.

Haitokuwa rahisi kwa Rais Magufuli au wasaidizi wake kwenda kila sehemu kuwezesha au kuharakisha upatikanaji wa huduma. Jukumu hilo linapaswa kusaidiwa na wananchi wenyewe ambao mara nyingi ndio wahanga wakubwa wa huduma mbovu. Kadhalika, watoa huduma nje ya serikali wanapaswa kutambua kuwa hizi ni zama mpya, na asiyeweza kuendana na kasi ya Rais Magufuli na ajiweke kando.

Lakini mchango mkubwa zaidi wa wananchi wote unahitajika zaidi katika kupambana na ufisadi, rushwa na uhalifu mwingine nje ya serikali. Wakati Rais ameahidi kukabiliana na 'mapapa' wa uhalifu kama kwenye biashara hatari ya dawa za kulevya, pasipo wananchi kumsaidia kwa kuwatenga wahusika na kuwaripoti - badala ya kuwasujudia na kuwapa majina ya heshima kama 'wazungu wa unga' au 'mapedejee' basi tutamkwamisha, na nchi yetu itaendelea kuumizwa na vitendo hivyo viovu.

Kadhalika, ili kauli-mbiu ya 'Hapa Ni Kazi Tu' iweze kuleta matokeo kusudiwa na kuwa ya ufanisi ni muhimu kwa kila Mtanzania kuachana na dhana fyongo ya kusaka mafanikio kwa njia za mkato, turejee zama za Ujamaa na Kujitegemea ambapo waliokula bila kuvuja jasho tuliwaita 'kupe.' Sote tuchape kazi, tuache kufanya 'ujanja ujanja,' tuone fahari kuwa na shughuli halali badala ya kuamini kuwa ufisadi, rushwa, uhalifu, nk ndio njia rahisi na sahihi za kufikia mafanikio kwa haraka.

Baada ya kumpoteza Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyetujengea misingi imara ya taifa letu, japo sasa inamong?onyoka kwa kasi, na mzalendo wa daraja la kwanza, Sokoine, sala/dua zetu katika wimbo wetu wa taifa katika maneno "Mungu Ibariki Tanzania" zimesikika, na Mwenyezi Mungu ametuletea "Nyerere na Sokoine mpya" kupitia kwa Rais wetu mpya Dk. Magufuli. Tusijiangushe wenyewe kwa kutotumia ipasavyo fursa hii adimu.

Nimalizie makala hii kwa wito "wa kitaalamu" kwa ndugu zangu wa Idara ya Usalama wa Taifa, ambao pamoja na majukumu mengine, wana dhamana ya ulinzi wa Rais wetu na viongozi wengine wakuu kitaifa. Kama alivyosema mwenyewe, vita aliyoanzisha dhidi ya kila vitendo na kasumba zinazolikwaza taifa letu ni nzito na inawagusa watu wazito. Kwa vile yayumkinika kusema kuwa vitendo vya rushwa, ufisadi na uhalifu vimefikia hatua ya 'kimafia,' basi ni muhimu kuimarisha ulinzi wa Rais wetu (na viongozi wengine wanaopatiwa ulinzi) kwa sababu "tupo vitani".

Simaanishi kuwa ulinzi uliopo una upungufu lakini angalizo hili linazingatia ukweli kwamba 'vita' hiyo inagusa maslahi ya wengi, maslahi ya 'kupe' lukuki walioigeuza Tanzania yetu kuwa ni 'shamba la bibi,' la kuvuna wasichopanda, sambamba na wahalifu wanaoingiza, kuuza na kusafirisha dawa za kulevya kana kwamba ni bidhaa iliyoidhinishwa na Shirika la Viwango la Taifa (TSB), majangili wanaoshindana kuua wanyamapori wetu na kusafirisha nyara za serikali, na wahalifu wengineo.

Rais Magufuli ameahidi kutotuangusha, basi nasi tusimwangushe.

Hapa Ni Kazi Tu!

Raia Mwema

Ndugu zangu wana Jf Rais wetu kwa sasa ana maadui wengi sana kiasi kwamba kunatakiwa juhudi za ziada kuhakikisha kuwa anaendelea kuwahudumia wananchi wa Tanzania.

Katika hili kunahitajika kuimarisha BRIGEDI YA ULINZI WA RAIS ili kuhakikisha Rais wetu anaendelea kuwa salama. Mimi ni askari msitaafu niliyehudumu Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kikosi cha Jeshi Lugalo ingawa bado nahudumu Serikali hii katika sekta nyingine.

Ninapenda kutoa wito kwa Brigedi ya ulinzi wa Rais kuimarisha ulinzi wa Rais Magufuli ili kukabiliana na maadui wa Rais wanaoongezeka siku hadi siku. Nikiangalia walinzi wa Rais ninaowaona akiambatana nao naona kuna haja ya kuangalia vizuri kwani kwa maoni yangu ule ulinzi sio imara sana. Siwezi nikasema wasiwasi wangu uko wapi kwa sababu za kiusalama, lakini nina uhakika watu wa ulinzi na usalama watanielewa.

Kuna walinzi wa ''FEATURES'' fulani ningetegemea kuwaona katika ulinzi wa Rais ninaowaona akiwa nao lakini siwaoni. Vile vile ningependekeza ulinzi wa Rais uwe na Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wengi (waliovua makwanda) si kwasababu mimi nimetoka huko ila kiukweli hawa hawajaathiriwa sana na rushwa na hawawezi kurubuniwa/kushawishiwa kirahisi ukilinganisha na Polisi na Usalama wa Taifa ambao wengi wao wamejikita sana kwenye siasa.

Hata hivyo bado natoa wito kwa Mkuu wa Majeshi (CDF) GENERALI DAVIS MWAMNYANGE na makamanda wengine wa JWTZ kuwa Rais anahitaji ulinzi kwa nguvu zote.

Najua wengi mtaona hoja yangu haina mashiko lakini mimi kama mlinzi wa nchi hii ingawa nimestaafu lazima nitoa tahadhali zangu.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais wetu.

Amina.
 
Tehe teh rais kawa bize kufuta michapalo ya watu. Hiv mwenge nao ni mchapalo?
 
"Hotuba hii ya Rais Magufuli ni moja ya hotuba bora kabisa katika historia ya siasa za Tanzania."

Hili lilikuwa hitimisho langu katika mtandao wa kijamii wa Twitter mara baada ya Rais John Magufuli kumaliza kulihutubia Bunge wiki iliyopita, huko Dodoma.

Na kwa hakika watu kadhaa waliafikiana na hitimisho hilo. Kilichovutia wengi waliosikia hotuba hiyo, katika shughuli ya ufunguzi wa Bunge la 11, sio tu mpangilio wa hotuba yenyewe bali pia jinsi kila alilotamka lilivyoonyesha bayana kuwa lilitoka moyoni mwake kwa dhati kabisa.

Rais alianza hotuba yake hiyo kwa kuorodhesha matatizo mbalimbali aliyobaini wakati wa kampeni zake za urais ambapo alizunguka takriban Tanzania nzima. Alitoa uchambuzi wa kina wa matatizo hayo kabla ya kuelezea kwa undani ni kwa jinsi gani serikali yake itayashughulikia. Ilikuwa ni zaidi ya hotuba ya kisiasa, na pengine ingeweza kabisa kuwa mhadhara wa kitaaluma uliofanyika katika lugha nyepesi na ya kueleweka.

Moja ya vitu vilivyonivutia sana katika hotuba hiyo ni jinsi Rais Magufuli alivyoweza kutupatia jibu la swali ambalo kwa miaka kadhaa lilionekana kuwatatiza viongozi wetu mbalimbali: ?Kwa nini Tanzania ni masikini licha ya utajiri lukuki wa rasilimali ilionao.? Alieleza bayana na kwa kirefu jinsi ufisadi, rushwa na uhalifu vinavyochangia kukwamisha maendeleo ya taifa letu.

Kadhalika, alifafanua, kwa kutumia takwimu halisi, jinsi mabilioni ya fedha yalivyotumika visivyo kwa matumizi yasiyo muhimu na yaliyo nje ya uwezo wa taifa letu masikini.

Kwa hakika ilikuwa hotuba ya kihistoria iliyofunika kabisa utovu wa nidhamu wa hali ya juu ulioonyeshwa awali na wabunge wa upinzani ambao walitumia muda mwingi kabla ya hotuba hiyo kuzomea na baadaye kuamiriwa kutoka nje ya ukumbi huo.

Lakini kwa vile sio rahisi kumridhisha kila mtu, baadhi ya wenzetu waliosikiliza hotuba hiyo walidai kuwa eti ?haina tofauti na hotuba nyingine kadhaa zilizokuwa nzuri kuzisikiliza lakini zikaishia kuwa maneno matamu tu.? Wengine walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa hata mtangulizi wa Rais Magufuli, Jakaya Kikwete naye pia alianza urais wake kwa hotuba za kutia moyo kama hizo lakini mengi ya aliyoahidi, hususan lile la ?Maisha Bora kwa Kila Mtanzania,? yaliishia kuwa ahadi tu.

Sikubaliani na wakosoaji hao, japo hoja zao zinaweza kuwa na mantiki kidogo. Ni kweli kwamba ukosefu wa hotuba za kuvutia si moja ya matatizo yanayoikabili nchi yetu. Wengi wa wanasiasa na viongozi wetu ni mahiri sana wa maneno lakini tatizo huwa katika kutafsiri maneno yao kuwa vitendo.

Wakosoaji hao hawapo sahihi kwa sababu, kama nilivyoeleza awali, hotuba hiyo ilikuwa ya kutoka moyoni.Ilikuwa hotuba ya kiongozi anayeguswa na yanayoisibu nchi yake, kiongozi mwenye uelewa wa changamoto zinazoukabili uongozi wake, na mwenye dhamira thabiti ya kukabiliana na changamoto hizo.

Kuna mbinu moja muhimu ya kubaini iwapo mtu anaongea ukweli au anahadaa, nayo ni kumwangalia usoni. Tangu kuanza kwa kampeni zake za urais na hadi wakati wa hotuba hiyo ya wiki iliyopita, uso wa Rais Magufuli wakati anaongea unaonyesha bayana kuwa kila neno linalotoka mdomoni mwake ni la dhati, linatoka moyoni na si sehemu ya porojo tulilozoea kutoka kwa wengi wa wanasiasa na viongozi wetu. Mtaalamu yeyote wa kubaini ukweli na uongo hatoshindwa kuafikiana nami kuwa uthabiti wa kauli za Magufuli upo wazi kwa yeyote anayemwangalia usoni wakati anaongea.

Lakini pia, hotuba hiyo ilikuwa mwendelezo wa ishara nzuri zilizoanza kujitokeza siku moja tu tangu Rais Magufuli aingie ofisini, ambapo alifanya ziara ya kushtukiza Wizara ya Fedha, kabla ya kufanya ziara nyingine kama hiyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Na siku ya uzinduzi wa Bunge, alitukumbusha enzi za (Waziri Mkuu wa zamani) hayati Edward Sokoine, aliyesifika kwa uchungu wa mali za umma, baada ya kuamuru zaidi ya shilingi milioni 200 zilizochangwa kwa ajili ya hafla ya mchapalo ya sherehe za uzinduzi wa Bunge jipya zielekezwe kwenye ununuzi wa vitanda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, na kiasi kidogo tu kitumike kwa ajili ya hafla hiyo.

Kihesabu, chini ya wiki tatu tangu aingie madarakani, Rais Magufuli amekwishaokoa jumla ya shilingi milioni 900 kutokana na hatua alizochukua dhidi ya matumizi yasiyo ya lazima. Kwa kasi hii, tuna kila sababu ya kutarajiwa kuiona nchi yetu ikipaa kiuchumi, na hatimaye Watanzania kunufaika na neema lukuki ambayo nchi yetu imejaaliwa kuwa nayo.

Sina shaka kuhusu uwezekano wa mafanikio ya hatua za Rais Magufuli huko serikalini. Licha ya kuwa na Waziri Mkuu mchapakazi mzoefu, Majaliwa Kassim Majaliwa, kuna kila dalili kuwa baraza la mawaziri ambalo hadi wakati ninaandaa makala hii lilikuwa halijatangazwa, litasheheni wachapakazi kama yeye. Kwa hiyo, kazi ya kurejesha nidhamu serikalini, kupunguza matumizi yasiyoendana na umasikini wetu na kupambana na ufisadi ina dalili kubwa za mafanikio.

Eneo ambalo Rais Magufuli hawezi kufanikiwa peke yake pasipo ushirikiano wa Watanzania wote ni nje ya serikali na huko mtaani. Mara kadhaa nimekuwa nikisisitiza umuhimu wa wananchi kujenga kasumba ya kudai haki na stahili zao badala ya kuona haki/stahili hizo ni kama fadhila au upendeleo flani. Wenzetu huku Ughaibuni wamejenga desturi ya kutokubali huduma au bidhaa inayotolewa chini ya kiwango wanachostahili. Haki na stahili za mpokea huduma ni miongoni mwa vitu vinavyopewa umuhimu mkubwa huku tulipo.

Haitokuwa rahisi kwa Rais Magufuli au wasaidizi wake kwenda kila sehemu kuwezesha au kuharakisha upatikanaji wa huduma. Jukumu hilo linapaswa kusaidiwa na wananchi wenyewe ambao mara nyingi ndio wahanga wakubwa wa huduma mbovu. Kadhalika, watoa huduma nje ya serikali wanapaswa kutambua kuwa hizi ni zama mpya, na asiyeweza kuendana na kasi ya Rais Magufuli na ajiweke kando.

Lakini mchango mkubwa zaidi wa wananchi wote unahitajika zaidi katika kupambana na ufisadi, rushwa na uhalifu mwingine nje ya serikali. Wakati Rais ameahidi kukabiliana na 'mapapa' wa uhalifu kama kwenye biashara hatari ya dawa za kulevya, pasipo wananchi kumsaidia kwa kuwatenga wahusika na kuwaripoti - badala ya kuwasujudia na kuwapa majina ya heshima kama 'wazungu wa unga' au 'mapedejee' basi tutamkwamisha, na nchi yetu itaendelea kuumizwa na vitendo hivyo viovu.

Kadhalika, ili kauli-mbiu ya 'Hapa Ni Kazi Tu' iweze kuleta matokeo kusudiwa na kuwa ya ufanisi ni muhimu kwa kila Mtanzania kuachana na dhana fyongo ya kusaka mafanikio kwa njia za mkato, turejee zama za Ujamaa na Kujitegemea ambapo waliokula bila kuvuja jasho tuliwaita 'kupe.' Sote tuchape kazi, tuache kufanya 'ujanja ujanja,' tuone fahari kuwa na shughuli halali badala ya kuamini kuwa ufisadi, rushwa, uhalifu, nk ndio njia rahisi na sahihi za kufikia mafanikio kwa haraka.

Baada ya kumpoteza Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyetujengea misingi imara ya taifa letu, japo sasa inamong?onyoka kwa kasi, na mzalendo wa daraja la kwanza, Sokoine, sala/dua zetu katika wimbo wetu wa taifa katika maneno "Mungu Ibariki Tanzania" zimesikika, na Mwenyezi Mungu ametuletea "Nyerere na Sokoine mpya" kupitia kwa Rais wetu mpya Dk. Magufuli. Tusijiangushe wenyewe kwa kutotumia ipasavyo fursa hii adimu.

Nimalizie makala hii kwa wito "wa kitaalamu" kwa ndugu zangu wa Idara ya Usalama wa Taifa, ambao pamoja na majukumu mengine, wana dhamana ya ulinzi wa Rais wetu na viongozi wengine wakuu kitaifa. Kama alivyosema mwenyewe, vita aliyoanzisha dhidi ya kila vitendo na kasumba zinazolikwaza taifa letu ni nzito na inawagusa watu wazito. Kwa vile yayumkinika kusema kuwa vitendo vya rushwa, ufisadi na uhalifu vimefikia hatua ya 'kimafia,' basi ni muhimu kuimarisha ulinzi wa Rais wetu (na viongozi wengine wanaopatiwa ulinzi) kwa sababu "tupo vitani".

Simaanishi kuwa ulinzi uliopo una upungufu lakini angalizo hili linazingatia ukweli kwamba 'vita' hiyo inagusa maslahi ya wengi, maslahi ya 'kupe' lukuki walioigeuza Tanzania yetu kuwa ni 'shamba la bibi,' la kuvuna wasichopanda, sambamba na wahalifu wanaoingiza, kuuza na kusafirisha dawa za kulevya kana kwamba ni bidhaa iliyoidhinishwa na Shirika la Viwango la Taifa (TSB), majangili wanaoshindana kuua wanyamapori wetu na kusafirisha nyara za serikali, na wahalifu wengineo.

Rais Magufuli ameahidi kutotuangusha, basi nasi tusimwangushe.

Hapa Ni Kazi Tu!

Raia Mwema
 
hilo halina mjadala...vyombo vya dola vimlinde magufuli kwa nguvu zote...ili ayapasue majipu...tena yapo kila mahali...
 
Hivi unafikirk vyombo vya ulinzi na usalama havijaliona hilo ?

Labda iko haja mambo kidogo yawe yanaachiwa kwa mfano ulinzi wa marehemu baba wa Taifa ungetolewa documentary kidogo watu wapate mwanga na "ulinzi wa Rais". . . . .
 
Habari wanajamii wenzangu kwa kipindi kirefu tulikua tunalilia kiongozi bora na sibora kiongozi, wanachama wa nje na ndani wamekubali kwa awamu hii ya tano kupata kiongozi mzuri mwenye kujielewa na mwenye msimamo wa kikazi.

Mungu kasikia kilio cha watz kuwaletea kiongozi mwenye kujali wananchi wake, vigogo wasiopenda wananchi wameanza kulialia na kuletafujo, acha niende kwenye point, raisi wetu "MUNGU" aendelee kumuongoza, kumlinda na amuepushe na balaa na husda za watu ambao hawapendi maendeleo ya wananchi kwa maslahi yao binafsi, na ndo maana nikasema kwamtindo huu aliokuja nao lazima atakua na maadui wengi kupita kiasi na kati ya maadui hao lazima atakua nao kwenye vikao vyake vya siri ila hatowajua.

Katika point yangu nashauri bora awe karibu na ulinzi wa JWTZ kuliko hao wengine tunaowafikiria ni watendaji wazuri kwa rais mpya jeshi hili limekua likisifiwa kwa kiasi kikubwa katika utendaji wa kazi naamini kwa lazima jwtz raisi awe nao karibu kama ulinzi wake na sivinginevyo.
 
sasa nyinyi ndo mnaomuombea mabaya,kwanini kila siku mnazungumzia usalama wake?kwani yeye ni mwehu hajui anachokifanya?
 
Back
Top Bottom