Rais Magufuli anamjenga Tundu Lissu kisiasa bila kujua!!

Sasa kama nchi imepinda ulitaka afanyeje? Ni lazima ainyooshe kwanza halafu ndio aanze k usafiri nje ya nchi

Sent using Jamii Forums mobile app

Katika vihoja vya Rais Magufuli ni pamoja na hilo la kudai ati akisafiri kwenda nje ya akirudi atakuta watu wameanza kupiga dili!!!! Hiki ni kichekesho. Wewe ulishaona wapi nchi inaendeshwa na mtu mmoja?

Serikali ni mfumo(system) wa watu kwa maana ya Rais, Makamu wake, PM, CJ, CDF, Baraza la Mawaziri na Viongozi wengine kama Timu na vyombo vya dola ndio wanatengeneza Serikali!!! JPM peke yake hawezi kuwadanganya watu kwamba yeye akisafiri kila kitu kinaparaganyika, huu ni uongo wa mchana. State organs zinafanya kazi gani??
Maana kwa lugha hizi kuna Siku Magufuli atawaambia Watanzania kuwa HALALI INABIDI AKESHE maana akilala tu watu wanapiga dili!!!!
 
Ah wapi!

Hamna lolote hapo.

Tundu Lissu anajibomoa yeye mwenye pamoja na hicho chama chake kwa kuchochea ukabila.

Na Watanzania watazikataa hizo siasa za kutugawa kimakundi.

Hamuoni tu hata CHADEMA wenzie walivyo kimya kuhusu hizo tuhuma zake?

Ni kwa sababu wanajua ni uzushi tu.
Hata kijana mdogo wa sekondari anaujua ukabila anaoonyesha Magu, kama wewe huuoni basi pengine ni kwa vile umakuhusu
 
Kitendo cha Serikali ya Rais Magufuli kumfuatafuat, kumkamata na kumweka ndani Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania(Tanganyika Law Society) kimeendelea kumjenga kisiasa Tundu Lissu na kumpa heshima kubwa nje na ndani ya Tanzania.

Ni kwa vile Rais huyu hashauriki lakini kama angelirejea hotuba za Baba wa Taifa Mwl J.K Nyerere(RIP) kuhusu upinzani miaka ile ya kuanzia 1992 na kuendelea pale ambapo watu kama Marehemu Mchungaji Mtikila(DP) na Augustine Lyatonga Mrema(NCCR) walivyochomoza kisiasa na kuwa maarufu kwa sababu ya kuwa na wafuasi wengi hasa wanachuo kiasi cha magari yao kuwa yanasukumwa kwa mikono na mshabiki bila kuendeshwa.

Hii ilipelekea Polisi na CCM wakaanza kuwapiga mabomu na kamata kamata za kijinga kama tunavoziona sasa. Baba wa Taifa kwa kuona mbali aliliona hili na aliwakemea Polisi na hata viongozi wa wakti ule na akawaambia, Kama kuna mtu Watanzania wanampenda kiasi cha kulisukuma gari lake na hata kumbeba mabegani wakitaka acha wafanye hivo maana wanatumia uhuru wao wa kidemokrasia.

Mwalimu akaonya kwamba kitendo chochote cha Serikali kuzuia mtu huyo asisukumwe na gari lake, asibebwe mabegani au mgongoni, asifuatwe na mashabiki wake kama wanaandamana ni KUENDELEA KUMWONGEZEA UMAARUFU TU pasi na sababu za msingi. Magufuli halioni yeye anafkiri kupamba na Tundu Lissu nje na ndani ya Bunge ni kumdhoofisha kisiasa ili hali ni kinyume chake. kwa sasa Lissu ndiye Mwanasiasa anaye julikana sana ndani na nje ya nchi kuliko hata Magufuli mwenyewe ambaye hataki kwenda Asia, USA, Europe n.k kwa kisingizio cha kuinyosha nchi kana kwamba wasaidizi wake hawajui lolote kuhusu Tanzania.
Pole sana Rais JPM.
Mtoa hoja,
Wengine wanapinga kwa kuwa pengine hawakuwepo wakati huo, au labda walikuwepo ila kwa vile hawampendi Lissu, au labda hawajui katiba ya nchi inavyosema, au pengine wanajua, walikuwepo na wameamua tu hivyo wanaona ni vyema kupinga. Poleni sana.

Nendeni Kenya muone Raila Odinga jinsi anayoitwa '' FATHER OF DEMOCRACY'' na msisahau, aliwekwa kizuizini kwa miaka 9, na bado alipoyoka, mpaka leo ni msiba mkali kwa watawala.

Tusisahau Mandela hapo Afrika Kusini. Miaka 27, jela, lakini alipotoka bado akawa rais wa nchi. Hakuna jela, polisi, mahakama wala kitu chochote kinachoweza kuzuia wananchi waliofanya maamuzi ya dhati ndani ya nchi yao. Well, ''muda'' ndiye mwalimu tosha wa kila kitu. Sisi yetu macho, muda ukifika, kitaeleweka tu.

Si kwamba Lissu yuko sahihi kwa 100%, hapana. Lakke tunapotumia nguvu kubwa ya dola juu yake hivi, anapata huruma zisizo na ulazima kwa wananchi kulikoni ambavyo tungemwangalia tu kama mpumbavu na tukampuuzilia .bali siku zikapita. Kwani tungekufa???? Au tusingeedelea kutawala miaka yetu mitano????

Anyway, sijui maana mi si mjuzi wa hayo mambo ya siasa. Ngoja wajuzi waendelee. Muda ukifika kitaeleweka tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa acha waendelee kumvimbisha likichwa aendelee kunyea debe huku wao wanalala na wake zao majumbani mwao na mpaka sasa ni yeye na kunguni na chawa chezea rumande ww
 
Kweli kabisa acha waendelee kumvimbisha likichwa aendelee kunyea debe huku wao wanalala na wake zao majumbani mwao na mpaka sasa ni yeye na kunguni na chawa chezea rumande ww

Hujitammbui wewei!!
Let be assured tomorrow will be your turn to be in remand!!!
 
Utakaa ivoivo coz ww unashangilia lisu aendelee kufanya upuuzi asote rumande ili uendelee kumfaidi mkewe heeh makubwa tumeshakuelewa kumbe ndio zako subiri siku jamaa akitoka lazima apumzikie kwako
 
Na wataendelea kufanya hivyo ili kuleta mgogoro mkubwa ndani ya Chadema ifikapo 2020 maana chama kitakuwa na tajiri mwenyewe uchu wa ikulu na maskini jeuri ila maarufu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitendo cha Serikali ya Rais Magufuli kumfuatafuat, kumkamata na kumweka ndani Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania(Tanganyika Law Society) kimeendelea kumjenga kisiasa Tundu Lissu na kumpa heshima kubwa nje na ndani ya Tanzania.

Ni kwa vile Rais huyu hashauriki lakini kama angelirejea hotuba za Baba wa Taifa Mwl J.K Nyerere(RIP) kuhusu upinzani miaka ile ya kuanzia 1992 na kuendelea pale ambapo watu kama Marehemu Mchungaji Mtikila(DP) na Augustine Lyatonga Mrema(NCCR) walivyochomoza kisiasa na kuwa maarufu kwa sababu ya kuwa na wafuasi wengi hasa wanachuo kiasi cha magari yao kuwa yanasukumwa kwa mikono na mshabiki bila kuendeshwa.

Hii ilipelekea Polisi na CCM wakaanza kuwapiga mabomu na kamata kamata za kijinga kama tunavoziona sasa. Baba wa Taifa kwa kuona mbali aliliona hili na aliwakemea Polisi na hata viongozi wa wakti ule na akawaambia, Kama kuna mtu Watanzania wanampenda kiasi cha kulisukuma gari lake na hata kumbeba mabegani wakitaka acha wafanye hivo maana wanatumia uhuru wao wa kidemokrasia.

Mwalimu akaonya kwamba kitendo chochote cha Serikali kuzuia mtu huyo asisukumwe na gari lake, asibebwe mabegani au mgongoni, asifuatwe na mashabiki wake kama wanaandamana ni KUENDELEA KUMWONGEZEA UMAARUFU TU pasi na sababu za msingi. Magufuli halioni yeye anafkiri kupamba na Tundu Lissu nje na ndani ya Bunge ni kumdhoofisha kisiasa ili hali ni kinyume chake. kwa sasa Lissu ndiye Mwanasiasa anaye julikana sana ndani na nje ya nchi kuliko hata Magufuli mwenyewe ambaye hataki kwenda Asia, USA, Europe n.k kwa kisingizio cha kuinyosha nchi kana kwamba wasaidizi wake hawajui lolote kuhusu Tanzania.
Pole sana Rais JPM.
Tunatakiwa tuambizane ukweli kwa faida ya taifa letu

Lisu anafanya kila kitu kwa Uhuru kama mtanzania kisheri na kikatiba anaruhusiwa .lkn pombe anaona kukosolewa ni uchochezi

Najiuliza Uhuru uliopo marekani kwa watu na vyombi vya habari sijui kama angeongoza hata miezi miwili

Akili yangu ndogo kabisa uchochezi unahusiana nini na mkojo kweli kwann watu wasimfuatilie lisu kwa jinsi anavyoweza kujieleza kwa hoja

Leo mawakili Wa Afrika mashariki wanajipanga kumtetea lisu hapo tu anazidi kupanda juuuu kisiasa

Pigo LA kwanza lilikuwa kwenye uchaguzi Wa rais Wa mawakili Tanganyika alipita pamoja na mkwara mkubwa hikusaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watawala waliopo na wale wastaafu wanawabeza na kuwadhihaki Watanzania wanaowalisha na kuwavisha kwa kodi zao kuwa ni MALOFA, VILAZA, WAVIVU na kila aina ya maneno ya kuudhi lakini wanashindwa kujitambua wao wenyewe wako kwenye nafasi gani katika kutumia hekima na busara japo kidogo waliyojaliwa na MWENYEZI MUNGU pale wanaposhindwa kujibu hoja na changamoto wanazokumbana nazo kwa njia sahihi badala yake wanatumia mitutu ya bunduki, mabomu na marungu wakifikiri wanatoa majibu kwa yale wanayokumbana nayo.

HOJA HUJIBIWA KWA HOJA NA PALE INAPOONEKANA HAKUNA HOJA AMA HAKUNA MAJIBU KWA WAKATI HUO NI BUSARA ZAIDI KUKAA KIMYA BADALA YA KUTUMIA MABAVU.
 
Tanzania tuna bahati mbaya sana ya kutawaliwa na hiki chama cha Makinikia(CCM).
Kwa vile hawa watawala wa chma hiki wamekuwa wakipokezana vijiti wao kwa wao kwa kupanga matokeo na kupeana mamlaka na madaraka basi wanawaona Watanzania wote ni MALOFA, VILAZA na WAVIVU WA KUFIKIRI. Haya ni matusi makubwa sana kwa Wananchi waliokupa ridhaa uwatumikie!!

Haya matusi hayajaanza kwa Magufuli, yameanza kitambo baada ya Baba wa Taifa kuondoka yakaingia manyang'au(fisi) wenye tamaa na uchu wa madaraka. Mwalimu enzi za uhai wake alikuwa akisema, KUONGOZA NI KUONYESHA NJIA na ndiyo maana hasa ya Kiongozi. Lakini kwa sasa nchi haina Viongozi baali ina Watawala wasiojua maana ya kuongoza na kuongozwa. Wako pale kujinufaisha na kuhakikisha kuwa Mtanzania mwingine yeyote aliye nje wa mfumo wao(CCM na UKADA) hapati nafasi ya kuongoza!!!

Ni bahati mbaya sana kwa Watanzania lazima waombe sana Mungu ili afanye mabadiliko kwa nguvu zake bila kutumia Wanadamu. The Bible says, ''cursed is the one who trusts in man'' Kwamba amelaaniwa yule amtegemea mwanadamu. Kuna watu nchi hii hasa ndani ya CCM na Serikali yake wanaishi kwa nguvu ya mtu na pasipo huyo mtu wamekwisha!!! Kulingana na Mungu hawa wamekwisha kulaaniwa. Je, tunategemea nini kuongozwa na watu walio laaniwa kama siyo laana juu ya laana?
 
Back
Top Bottom