Rais Magufuli anamjenga Tundu Lissu kisiasa bila kujua!!

Nimeamini kweli kuna watu ni NYUMBU. nakumbuka lema alifananishwa na Mandela na walitoa povu la kutosha. Lema alipotoka sikuona tena harakati alizokuwa anazpigania kias kufananishwa na Mandela.

Leo hii wamerudia kulekule kumfananisha LISU na Mandela. Sasa hawa watu hivi ubongo wako hauna uwezo wa ku retrieve mambo?Yani kila anaefanya UJINGA huko chadema akipelekwa polisi,wanaanza kumpa mavyeo kibao.

posti fromu Nokia kitochi yuzingi jamii forum
 
Kitendo cha Serikali ya Rais Magufuli kumfuatafuat, kumkamata na kumweka ndani Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania(Tanganyika Law Society) kimeendelea kumjenga kisiasa Tundu Lissu na kumpa heshima kubwa nje na ndani ya Tanzania.

Ni kwa vile Rais huyu hashauriki lakini kama angelirejea hotuba za Baba wa Taifa Mwl J.K Nyerere(RIP) kuhusu upinzani miaka ile ya kuanzia 1992 na kuendelea pale ambapo watu kama Marehemu Mchungaji Mtikila(DP) na Augustine Lyatonga Mrema(NCCR) walivyochomoza kisiasa na kuwa maarufu kwa sababu ya kuwa na wafuasi wengi hasa wanachuo kiasi cha magari yao kuwa yanasukumwa kwa mikono na mshabiki bila kuendeshwa.

Hii ilipelekea Polisi na CCM wakaanza kuwapiga mabomu na kamata kamata za kijinga kama tunavoziona sasa. Baba wa Taifa kwa kuona mbali aliliona hili na aliwakemea Polisi na hata viongozi wa wakti ule na akawaambia, Kama kuna mtu Watanzania wanampenda kiasi cha kulisukuma gari lake na hata kumbeba mabegani wakitaka acha wafanye hivo maana wanatumia uhuru wao wa kidemokrasia.

Mwalimu akaonya kwamba kitendo chochote cha Serikali kuzuia mtu huyo asisukumwe na gari lake, asibebwe mabegani au mgongoni, asifuatwe na mashabiki wake kama wanaandamana ni KUENDELEA KUMWONGEZEA UMAARUFU TU pasi na sababu za msingi. Magufuli halioni yeye anafkiri kupamba na Tundu Lissu nje na ndani ya Bunge ni kumdhoofisha kisiasa ili hali ni kinyume chake. kwa sasa Lissu ndiye Mwanasiasa anaye julikana sana ndani na nje ya nchi kuliko hata Magufuli mwenyewe ambaye hataki kwenda Asia, USA, Europe n.k kwa kisingizio cha kuinyosha nchi kana kwamba wasaidizi wake hawajui lolote kuhusu Tanzania.
Pole sana Rais JPM.
kuna ubaya gani kama anamjenga kisiasa kwa kukaa korokoroni?
 
Utakaa ivoivo coz ww unashangilia lisu aendelee kufanya upuuzi asote rumande ili uendelee kumfaidi mkewe heeh makubwa tumeshakuelewa kumbe ndio zako subiri siku jamaa akitoka lazima apumzikie kwako
Hivi wakati Nape anashikiwa bastola ulikuwa ughaibuni, pia walipokamatwa kina Bashe ulikuwa ndotoni au Mama Nagu alivyokamatwa ulikuwa usingizini? achilia mbali wale ambao wakihoji ukamatwaji wao inasemekana ni uchochezi... Mwalimu alipata kusema "mtu akila nyama ya mtu hawezi kuacha ataendelea tu...." (hapo fikiria kama amekula wa kijiji jirani wameisha inamaanisha nini!?)
 
Nimeamini kweli kuna watu ni NYUMBU. nakumbuka lema alifananishwa na Mandela na walitoa povu la kutosha. Lema alipotoka sikuona tena harakati alizokuwa anazpigania kias kufananishwa na Mandela.

Leo hii wamerudia kulekule kumfananisha LISU na Mandela. Sasa hawa watu hivi ubongo wako hauna uwezo wa ku retrieve mambo?Yani kila anaefanya UJINGA huko chadema akipelekwa polisi,wanaanza kumpa mavyeo kibao


Misuli,
Pole sana for thy shallow mind in thinking things not out of the bo7x! To you any Tanzanian who challenges Magufuli knows noting!!
Just for your info, Lissu na Lema are herois!!!!!
 
Back
Top Bottom