Rais Magufuli amteua Prof. Sylvester Mpanduji Mkurugenzi SIDO

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
593
1,712
Uteuzi.jpg


Rais wa Jamhwi ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Sylvester Michael Mpanduji kuwa Mkwllgenzi Mk.uu wa Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO).


Ta:uifa iliyotolewa leo Ikulu Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Sylvester Michael Mpanduji umeanzia leo tarehe 18 Julai, 2016.


Kabla ya uteuzi huu Prof. Sylvester Michael Mpanduji alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu

cha Sokoine cha Kilimo (SUA).


Prof. Sylvester Michael Mpanduji alichukua nafasi iliyoachwa na Mhandishi Omary Jumanne Bakari ambaye uteuzi wake umetenguliwa.


Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Winnie Mpanju Shumbusho kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa - Dodoma.


Kabla ya Uteuzi huo, Dk Winnie Mpanju Shumbusho alikuwa Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Afya Duniani (VVHO) lenye makao yake makuu Mjini Geneva nchini Uswisi na alimaliza mkataba wake tangu Mwezi Desemba 2015.


Uteuzi wa Dk Winnie Mpanju Shumbusho umeanza leo tarehe 18 Julai 2016.


Dk. Winnie Mpanju Shumbusho atachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Donan William Mmbando ambaye ameomba kupumzika kutokana na sababu binafsi.
 
Mbona anateua sana kila siku inayoenda kwa Mungu lazima ateue
Zamani kwani hawa watu walikuwa wanapatikanaje mbona nilikuwa sisikii kuteuateua!

Siasa umeanza kuzijua lini.?
 
Mi nasema simungu'nyi maneno sehem ambazo zikipewa kazi zinaisimamia vema
Kanda ya kaskazini, moshi. Arusha na manyara kidogo
Kanda ya ziwa, kagera , mwanza na. Kigoma, Shinyanga na tabora
Ukanda wa mbeya, na mtwara kidogo,
Lakin pwani siwafichi , na wazawa wa Dar es salaam huwa mnatuangusha sana sana
 
Back
Top Bottom