Rais Magufuli amtaka Mkurugenzi wa DAWASA Eng. Archard Mutalemwa, kujistaafisha kazi

Rais anajua sheria na anajua kilichoendelea na kinachoendelea.Maneno yake "najua unajuana na Mawaziri" yana maana kubwa.Muache afanye kazi.

Huyu bwana huko nyuma alikuwa na kashfa nyingi sana,lakini yupo kwa sababu "anajuana na mawaziri!"Kwa sasa hayo hayapo tena. Yakimkuta ya kumkuta bado akiwa kazini anaweza akakosa hata retirement benefits zake.It will be wise for him to quit.
 
Hata mkimuweka malaika dawasco/dawasa serikali na wizara zisipoamua kufumua mfumo wa zamani wa maji wa jiji mtakuwa mnafanya kazi bure.... Unahitaji uwekezaji wa pesa nyingi sana.
Ni hivi, mkuu alisema wakimaliza uhakiki wa vyeti wanaanza uhakiki wa umri. Yeye keshahakiki umri wa Mtalemwa kasema umeenda hata kama ana umbo zuri.
 
Amepewa heshima aondoke kwa amani apate mafao badala ya kuwa fired.

Wewe una akili ndogo kama Profesa Muhongo, Rais akikupa fursa hiyo kama upo karibu mkabidhi baruwa hapohapo ya kujiuzuru, au omba mic ujiuzulu kwa mdomo hadharani then baruwa ifuate.

Hapo umenena. Asije akawa na akili dogo kama ya Profesa Muhongo. Ukipewa muda utumie
 
Kwa hiyo jamaa ufisadi wote wa DAWASCO anaujua mwanzo mwisho.!
Nitashangaa kama kesho ataingia ofisini kufanyakazi badala ya kukabidhi resignation letter with immediate effect.

Nitaamini kweli sisi ngozi hii tulianzia kwenye manyani. Huyu Mutalemwa ni kati ya viumbe wachache sana wenye bahati na mood ya Mkuru, aondoke tu hamna namna, ni kichekesho leo tukiambiwa hakujiandaa.
 
Hapa ndipo utaona ujinga wa Magufuli.

Yeye rais, ana nguvu zote za kiserikali kumuondoa Mutalemwa.

Au kama anataka kuongea naye kidiplomasia, ana nguvu zote za kiserikali kuongea naye Mutalemwa kidiplomasia privately.

Anawezakumpigia simu, anawezakumuita ikulu, anawezakumtembelea ofisini kwake etc.

Katika kazi za serikali, unaposikia fulani kajiuzulu, wengi wa hao watu wanaojiuzulu wanakuwa wameombwa na wakubwa zao kujiuzulu, ili kuondoka kazini bila kashfa ya kufukuzwa.

Magufuli angeweza kumuomba Mutalemwa kujiuzulu privately bila kumvunjia heshima kwa umma.

Sasa kwanini huyu mtu mwenye nguvu zote hizi bado analialia majukwaani?

Kama si kutafuta kiki za kijinga tu?
 
Heshima kwenu mkuu,

Leo rais Magufuli amezindua Mradi wa Maji wa Ruvu. Katika Hotuba yake, amemtaka Mtendaji mkuu wa DAWASA kujistaafisha kama vipi atatumika kwenye kazi nyingine. Mutalemwa kwa kihaya ni mtu ambaye hakataliki. Sasa Mimi ni Mzilankende na ni Muyango sasa usije ukasubiri hadi ukakatalika(Ukalemwa). amesema Magufuli.
View attachment 528238
Mimi nina data zako zote ndo maana nazungumza kwa polite language hapa. Inawezekana Waziri akawa rafiki yako kama Mawaziri wote walivyokuwa marafiki zako, hilo nalo ninalijua. Lakini Muzilankende this is your time. Umefanya kazi nzuri, Waachie vijana ili tudeal nao, tufukuzane nao, Nadhani umenielewa. Usije ukasema (ubwato bufa magoba au kasukamile ibale katalasyaka kasumbikumgurusi?) sina uhakika na maneno.

"Lakini wapo watu wanauliza, Mutalemwa atasitaafu lini? Mimi Mutalemwa nmeanza kumsikia nafikiri bado nikiwa Sekondari. Waziri, mimi napenda kuzungumza kwa Uwazi tu, ndugu yangu mzilankende Mutalemwa, jiandae kustaafu Unaweza ukawa na umbo zuri ambalo halizeheki, lakini Umri huwa unaenda, angarau tukutumie katika majukumu mengine. Unajua jina nalo likizoeleka mahali fulani hata kama ulikuwa mzuri unaweza ukatafutiwa dhambi.

Sasa nikuombe ndugu yangu Mutalemwa with due respect kwa kazi nzuri uliyoifanya, Jiandae kustaafu haraka kabla mabaya hayajakufuata hapo" amesema rais Magufuli. Mimi nazungumza haya naomba mnisamehe ndugu zangu kama ntawakwaza lakini napenda nizungumze ukweli.

My take:

Huyu Eng Archard Mutalemwa amewahi kuwa na kashifa nyingi sana. Aliwahi kushutumiwa kusambaza maji yasiyo na dawa (1993) wakati akiwa NUWA akaundiwa tume na kuthibitishwa ni kweli. Waziri wa Maji wakati huo alikuwa JK, afya akiwa Meghji.

Aliwahi kushutumiwa kusasababisha NUWA kufunguliwa kesi na wakazi wa Sinza baada ya taarifa hizo? Wakazi hao walitetewa na Wakili (sasa marehemu Julius Ndyanabo)?

Wakati akiwa NUWA ilikuwa inatuhumiwa kununua madawa ya maji yasiyofaa mara kwa mara na tuhuma za ubadhirifu lukuki?

Hivi huyu ni Archard Mutalemwa yupi DAWASCO?

Kweli Mhe.Rais "Bagambila balinsi balikugwilu bahulila", nitasema kweli na mbinguni ni mashahidi.
 
Mkulu hata kama angekuwa yeye,JK anamwambia mbele za watu kuwa kakaa sana wizara ya ujenzi hivyo sasa aondoke aachie vijana,angejisikiaje,kuna Vitu vingine JPM anakosea kwa kweli,Mutalemwa leo lazima yupo down,yaani si kwa kuambiwa ajiondoe kila baada ya dakika tano jina lake linatajwa akiambiwa kazeeka jamani,nikimwangalia hata 60 hajafika yule.
Halafu ukimuangalia jpm ndo inaonekana Mzee kuliko Jamaa!
Ila maajabu zaidi anasema ameanza kumsikia toka akiwa primary
 
Mkulu anajua Mutalemwa ni CEO mzuri, mtu yoyote wa DAWASA aje hapa abishe, la sivyo Mkulu angemtumbua. Watu wanachanganya DAWASCO na DAWASA! Mkulu hapo ame-hit below the belt very unfair kum-treat CEO kama Mtalemwa namna hiyo.
 
Amepewa heshima aondoke kwa amani apate mafao badala ya kuwa fired.

Wewe una akili ndogo kama Profesa Muhongo, Rais akikupa fursa hiyo kama upo karibu mkabidhi baruwa hapohapo ya kujiuzuru, au omba mic ujiuzulu kwa mdomo hadharani then baruwa ifuate.
Mkuu ukiomba MIC utatisha sana
 
Back
Top Bottom