Rais Magufuli amtaka Mkurugenzi wa DAWASA Eng. Archard Mutalemwa, kujistaafisha kazi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,507
55,021
Heshima kwenu mkuu,

Leo rais Magufuli amezindua Mradi wa Maji wa Ruvu. Katika Hotuba yake, amemtaka Mtendaji mkuu wa DAWASA kujistaafisha kama vipi atatumika kwenye kazi nyingine. Mutalemwa kwa kihaya ni mtu ambaye hakataliki. Sasa Mimi ni Mzilankende na ni Muyango sasa usije ukasubiri hadi ukakatalika(Ukalemwa). amesema Magufuli.
DC2SlVFXsAEuGDm.jpg

Mimi nina data zako zote ndo maana nazungumza kwa polite language hapa. Inawezekana Waziri akawa rafiki yako kama Mawaziri wote walivyokuwa marafiki zako, hilo nalo ninalijua. Lakini Muzilankende this is your time. Umefanya kazi nzuri, Waachie vijana ili tudeal nao, tufukuzane nao, Nadhani umenielewa. Usije ukasema (ubwato bufa magoba au kasukamile ibale katalasyaka kasumbikumgurusi?) sina uhakika na maneno.

"Lakini wapo watu wanauliza, Mutalemwa atasitaafu lini? Mimi Mutalemwa nmeanza kumsikia nafikiri bado nikiwa Sekondari. Waziri, mimi napenda kuzungumza kwa Uwazi tu, ndugu yangu mzilankende Mutalemwa, jiandae kustaafu Unaweza ukawa na umbo zuri ambalo halizeheki, lakini Umri huwa unaenda, angarau tukutumie katika majukumu mengine. Unajua jina nalo likizoeleka mahali fulani hata kama ulikuwa mzuri unaweza ukatafutiwa dhambi.

Sasa nikuombe ndugu yangu Mutalemwa with due respect kwa kazi nzuri uliyoifanya, Jiandae kustaafu haraka kabla mabaya hayajakufuata hapo" amesema rais Magufuli. Mimi nazungumza haya naomba mnisamehe ndugu zangu kama ntawakwaza lakini napenda nizungumze ukweli.

My take:

Huyu Eng Archard Mutalemwa amewahi kuwa na kashifa nyingi sana. Aliwahi kushutumiwa kusambaza maji yasiyo na dawa (1993) wakati akiwa NUWA akaundiwa tume na kuthibitishwa ni kweli. Waziri wa Maji wakati huo alikuwa JK, afya akiwa Meghji.

Aliwahi kushutumiwa kusasababisha NUWA kufunguliwa kesi na wakazi wa Sinza baada ya taarifa hizo? Wakazi hao walitetewa na Wakili (sasa marehemu Julius Ndyanabo)?

Wakati akiwa NUWA ilikuwa inatuhumiwa kununua madawa ya maji yasiyofaa mara kwa mara na tuhuma za ubadhirifu lukuki.

NB: Baada ya kuon watu wakiulizia sana, nmeona nitoe ufafanuzi kidogo tofauti iliyopo kati ya DAWASCO na DAWASA.

DAWASCO na DAWASA zinafanya kazi kwa ushirikiano katika utoaji wa huduma ya maji katika jiji la Dar es Salaam na miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani. DAWASCO ni mwendeshaji wa Miundombinu yote ya Majisafi na Majitaka wakati DAWASA ni mmiliki na msimamizi wa miundombinu hiyo.

Dawasco ni Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam na Pwani; na Dawasa ni Mamlaka ya Majisafi na Majitaka.

Kampuni na Mamlaka, vyote vya umma. Vina wafanyakazi “wengi tu.” Vina mfumo wa utawala unaofanana. Vina matumizi kama kampuni nyingine nchini

* DAWASA – Dar es Salaam Water & Sewerage Authority

* DAWASCO - Dar es Salaam Water and Sewerage Corporation.
 
Hvi kustaafu ni kwa mujibu wa sheria au ni neno la mkuu.

Au mi sijaelewa nini?
Kustaafu ni kwa mujibu wa sheria ambapo ukiwa na 55 years ni ruksa kustaafu kwa hiari ila ukifika 60 years sheria inakulazimisha kustaafu kwa lazima. Kwa case ya huyu kuna harufu ya kutumbuliwa sasa hapa mkulu ameamua kumpa kijembe kiaina cha kutafakari kama anaona anatosha kwenye hiyo nafasi wakati sheria inamtaka kustaafu kwa hiari (assuming ni 55years - 60years).

Japokuwa mkulu nae anawapa wakati mugumu sana kwa kauli zake hizo
 
Mhe. Rais alipokuwa akihutubia pale Mlandizi katika uzinduzi wa mradi wa maji alimtaja ndugu Mutalemwa akimwambia asitafu kwa nini?
Mwenye ufahamu atueleweshe tujue maana yaonekana ana dosari.
 
Back
Top Bottom