Rais Magufuli amrudishia Ubalozi Prof. Costa Mahalu baada ya kushinda kesi ya uhujumu uchumi

..ile kesi yake haikuhusu UFISADI?

..binafsi naiheshimu hukumu ya mahakama dhidi yake.

..lakini sikubaliani na hukumu ile.

..hivyo nishikilia msimamo wangu kwamba Prof ni fisadi.
Hata mi naamini hivyo,
Ile kesi ilianza kua ngumu kwa Upande wa washitaki pale tu BWM alipoingilia kati.
Regardless of content ya Utetezi wake BWM, ile tu kwamba ye ni shahidi wa Mahalu tayari inampa nguvu mahalu dhidi ya Upande wa Serikali
 
ww umezaliwa juzi, uliza kwa unyenyekevu ujibiwe

Hajawahi kuvuliwa Ubalozi

Alisimamishwa hadhi ya Ubalozi kufuatia tuhuma zile ambazo ilikuwa dhahiri zinampeleka Gerezani ikabidi Mkapa amuokoe Kwa kusema Yeye ndie alimuagiza akiuke taratibu za Manunuzi kununua Jengo la Ubalozi na Mkapa alifanya vile Kwa kuwa alijua Yeye ana kinga ya kutoshtakiwa!

Hadhi ya Ubalozi hakuvuliwa Bali alisimamishwa kutumia status hiyo na hiyo Ni taratibu ya kidiplomasia ukiwa na tuhuma zenye nature ya kazi yako

Baada ya kushinda kesi ile automatic hadhi ile huwa anarudishiwa na kilichofanyika Leo Ni Kick ambayo imewazoa vilaza wengi ukiwemo Wewe

Alisimamishwa kutumia hadhi hiyo 2007
 
Hata mi naamini hivyo,
Ile kesi ilianza kua ngumu kwa Upande wa washitaki pale tu BWM alipoingilia kati.
Regardless of content ya Utetezi wake BWM, ile tu kwamba ye ni shahidi wa Mahalu tayari inampa nguvu mahalu dhidi ya Upande wa Serikali


Mkapa aliulizwa Na Wakili kuna Document yoyote ulimpa yenye Maelekezo hayo ya kukiuka taratibu za Manunuzi, Che Nkapa akacheka Kwa dharau Mahakamani kisha akasema Rais chochote amachosema utekelezaji huanza Mara Moja bila ya kujali nimeandika au laa

Kwa Kifupi Mkapa alilazimika auvae ule Ufisadi kuwa kafanya Yeye ili amuokoe Kijana wake
 
Hajawahi kuvuliwa Ubalozi

Alisimamishwa hadhi ya Ubalozi kufuatia tuhuma zile ambazo ilikuwa dhahiri zinampeleka Gerezani ikabidi Mkapa amuokoe Kwa kusema Yeye ndie alimuagiza akiuke taratibu za Manunuzi kununua Jengo la Ubalozi na Mkapa alifanya vile Kwa kuwa alijua Yeye ana kinga ya kutoshtakiwa!

Hadhi ya Ubalozi hakuvuliwa Bali alisimamishwa kutumia status hiyo na hiyo Ni taratibu ya kidiplomasia ukiwa na tuhuma zenye nature ya kazi yako

Baada ya kushinda kesi ile automatic hadhi ile huwa anarudishiwa na kilichofanyika Leo Ni Kick ambayo imewazoa vilaza wengi ukiwemo Wewe

Alisimamishwa kutumia hadhi hiyo 2007
sijaona ulichoandika ambacho sikifahamu, fuatilia nyuzi ambazo mleta uzi amezipin, zipo ambazo niliwasilisha mwenyewe kwa account nyingne
 
Prof. Mahalu anastahili kurudishiwa hiyo hadhi yake. Suala la ukabila nadhani haina maana katika hili. Kama mtakumbuka baada ya Mhe. Kikwete kuingia madarakani ama kwa kile kinaitwa waliokuwa nje mtandao wake wa vinginevyo, vigogo wengi wa Zama za Mr. Mkapa walifunguliwa mashtaka mbalimbali mojawapo ni huyu Prof. Mahalu ambapo baadaye ilidhihirika hakuwa na makosa na wala hakuwa mhusika katika sakata la kununua jengo la ubalozi. Wengine walioonja joto la Kikwete ni Mzee wa mtakula Nyasi aka Basil Pesambili Mramba na Mhe. Daniel Yona. Siasa wakati mwingine ni mbaya sana. Mkishatofautiana katika kambi zenu kabla ya uchaguzi basi kambi itakayoshinda isipikuwa na busara basi ni mshikemshike kwa kwenda mbele. Nadhani mliona mbinyano wa Kambi ya Membe na Lowassa wakati tunaelekea uchaguzi wa 2015. Mungu alisaidia hizi kambi zote mbili kuangukia pua.
 
Rais John Magufuli amemrudishia hadhi ya ubalozi Profesa Costa Mahalu kuanzia leo, Katibu Mkuu Mambo ya Nje, Adolf Mkenda amesema.

Katika taarifa aliyoitoa, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amemrudishia Profesa Costa Ricky Mahalu hadhi ya ubalozi kuanzia leo tarehe 17 Machi, 2018. Profesa Mahalu alisimamishwa kazi na kuvuliwa hadhi ya ubalozi mwaka 2007 kufuatia kufunguliwa mashtaka ya jinai na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo mwaka 2012 mahakama ilitoa hukumu kwamba Profesa Mahalu hakuwa na hatia.

Kulingana na taratibu za utumishi mtu yeyote ambaye amewahi kutumikia katika cheo cha balozi anaendelea kupewa hadhi ya kuitwa balozi maisha yake yote. hata baada ya kustaafu kwenye utumishi wa umma. Kufuatia uamuzi wa Mheshimiwa Rais, Profesa Mahalu sasa ataendelea kuwa na heshima ya kuitwa balozi.

Profesa Costa Mahalu alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Kabla ya kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya TSh 2 bilioni kesi ambayo alishinda.

Habari zaidi, soma=>(Docs): Siri ya Kesi ya Mahalu: Ununuzi wa Jengo la Ubalozi Italia

Benjamini Mkapa atinga mahakamani kutoa ushahidi kesi Ya Balozi Profesa Costa Mahalu

Profesa Costa Mahalu aibwaga serikali kortini
ccm na upuuzi
 
Aisee natamani angekuwa ametokea one kanda isiyotakiwa. Ile ameoa huko.
 
Prof Mahalu amshukuru Mkapa maisha yake yote. Bila Mkapa kutinga mahakamani, kesi ilikuwa ishamdodea Prof Mahalu na Mkapa ndiye alikuwa turufu ya mwisho.
 
Yule mswahili wa Msoga alimpokonya kwa hila
Mnafiki sana yule mzee,anajifanyaga ye ni full anacheka cheka tu.

Halafu balozi Mahalu aliposhinda Kesi Mahakamani kakaona aibu ikabidi ampe Ukuu wa Chuo "Bagamoyo University"
 
Back
Top Bottom