Rais Magufuli amrudishia Ubalozi Prof. Costa Mahalu baada ya kushinda kesi ya uhujumu uchumi

Prof. Mahalu ndiye alimpeleka Magufuli kwa Mkapa baada ya kushinda ubunge na kumwomba amlee. Mkapa akampa kuwa naibu waziri.

Magufuli kakaa kwa prof. Mahalu alipojiunga udsm. Kuna kipindi alikuwa anakaa kwa Mahalu kama mdogo wake.

Undugu wao ni kuanzia kule Sengerema. Hao ni ndugu kabisa.

Mkapa na Mahalu ni kitu kimoja. Urafiki wao ulianza pale wizara ya elimu ya juu. Wakati Mkapa ni waziri na Mahalu ni mkurugenzi wa elimu ya juu.
Kulikuwa na nguvu kubwa ya Wazanzibari pale. Katibu mkuu akiwa Bilali alikuwa na nguvu kuliko waziri kwasababu alikuwa na access ya moja kwa moja kwa rais Mwinyi. Hata Idara ya elimu ya juu ilijaa Wazanzibari. Mkapa na Mahalu wakawa pamoja.
Kwa kifupi ni hivyo.
 
Kwahiyo unataka kusema mramba na yona hawakustahili kupandishwa mahakamani?

Ndiyo! hawakustahili. Aliyestahili alikuwepo lakini kutokana na katiba yetu hawezi kupanda kizimbaani hata angeuza robo tatu ya nchi maadam alifanya hilo akiwa Rais. Wale walitekeleza maagizo ya bosi wao ambaye ndiye mkuu wa nchi. Ndo ahata vifungo vyenyewe vilikuwa vya kisanii. Vya kutoka nyumbani kwenda kufagia na kurudi nyumbani.
 
Prof. Mahalu ndiye alimpeleka Magufuli kwa Mkapa baada ya kushinda ubunge na kumwomba amlee. Mkapa akampa kuwa naibu waziri.

Magufuli kakaa kwa prof. Mahalu alipojiunga udsm. Kuna kipindi alikuwa anakaa kwa Mahalu kama mdogo wake.

Undugu wao ni kuanzia kule Sengerema. Hao ni ndugu kabisa.

Mkapa na Mahalu ni kitu kimoja. Urafiki wao ulianza pale wizara ya elimu ya juu. Wakati Mkapa ni waziri na Mahalu ni mkurugenzi wa elimu ya juu.
Kulikuwa na nguvu kubwa ya Wazanzibari pale. Katibu mkuu akiwa Bilali alikuwa na nguvu kuliko waziri kwasababu alikuwa na access ya moja kwa moja kwa rais Mwinyi. Hata Idara ya elimu ya juu ilijaa Wazanzibari. Mkapa na Mahalu wakawa pamoja.
Kwa kifupi ni hivyo.

Kuwepo Wazanzibari wengi kwenye kile kitengo. Ulikuwa ni mpango malum ambao Mzee Ruksa aliuubuni kwa mazumuni ya kuhakikisha wazanzibari wengi wapate elimu zao za juu kwenye nchi za ulaya magharibi na marekani ( ilionekana wazanzibari wengi walikuwa wanaishia mlimani na nchi za kijamaa) na kwa kiasi fulani ulifanikiwa.
 
Rais John Magufuli amemrudishia hadhi ya ubalozi Profesa Costa Mahalu kuanzia leo, Katibu Mkuu Mambo ya Nje, Adolf Mkenda amesema.

Katika taarifa aliyoitoa, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amemrudishia Profesa Costa Ricky Mahalu hadhi ya ubalozi kuanzia leo tarehe 17 Machi, 2018. Profesa Mahalu alisimamishwa kazi na kuvuliwa hadhi ya ubalozi mwaka 2007 kufuatia kufunguliwa mashtaka ya jinai na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo mwaka 2012 mahakama ilitoa hukumu kwamba Profesa Mahalu hakuwa na hatia.

Kulingana na taratibu za utumishi mtu yeyote ambaye amewahi kutumikia katika cheo cha balozi anaendelea kupewa hadhi ya kuitwa balozi maisha yake yote. hata baada ya kustaafu kwenye utumishi wa umma. Kufuatia uamuzi wa Mheshimiwa Rais, Profesa Mahalu sasa ataendelea kuwa na heshima ya kuitwa balozi.

Profesa Costa Mahalu alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Kabla ya kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya TSh 2 bilioni kesi ambayo alishinda.

Habari zaidi, soma=>(Docs): Siri ya Kesi ya Mahalu: Ununuzi wa Jengo la Ubalozi Italia

Benjamini Mkapa atinga mahakamani kutoa ushahidi kesi Ya Balozi Profesa Costa Mahalu

Profesa Costa Mahalu aibwaga serikali kortini

Msukuma mwenzake huyo lazma akumbukwe
 
Silaha kubwa ambayo JK ameitumia kwa wabaya wake ni kuwaweka karibu yake huwa haonyeshi hisia zake waziwazi kuwa amegombana na mtu na hii imemfanya JK kuwashinda wengi sana.Mwandosya alipewa hadi wizara maalum

Mkwere alimthibiti na kumneutralize Mwandosya kwa kumuweka karibu yake hivyo kujua movements zake zote!!! Njaa ilimponza Mwandosya ama sivyo kama alikuwa ameshiba asingekubali teuzi zile!!!
 
wanadiplomasia naomba ufafanuzi hapa Nimesikia kwenye media Mh toka kwenye ofisi namba moja amemrudishia hadhi ya ubalozi ndugu Mahalu. Je ukishakuwa balozi unaendelea kuwa balozi hata ukistaafu?
 
Back
Top Bottom