Rais Magufuli amrudishia Ubalozi Prof. Costa Mahalu baada ya kushinda kesi ya uhujumu uchumi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,493
54,900
Rais John Magufuli amemrudishia hadhi ya ubalozi Profesa Costa Mahalu kuanzia leo, Katibu Mkuu Mambo ya Nje, Adolf Mkenda amesema.

Katika taarifa aliyoitoa, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amemrudishia Profesa Costa Ricky Mahalu hadhi ya ubalozi kuanzia leo tarehe 17 Machi, 2018. Profesa Mahalu alisimamishwa kazi na kuvuliwa hadhi ya ubalozi mwaka 2007 kufuatia kufunguliwa mashtaka ya jinai na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo mwaka 2012 mahakama ilitoa hukumu kwamba Profesa Mahalu hakuwa na hatia.

Kulingana na taratibu za utumishi mtu yeyote ambaye amewahi kutumikia katika cheo cha balozi anaendelea kupewa hadhi ya kuitwa balozi maisha yake yote. hata baada ya kustaafu kwenye utumishi wa umma. Kufuatia uamuzi wa Mheshimiwa Rais, Profesa Mahalu sasa ataendelea kuwa na heshima ya kuitwa balozi.

Profesa Costa Mahalu alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Kabla ya kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya TSh 2 bilioni kesi ambayo alishinda.

Habari zaidi, soma=>(Docs): Siri ya Kesi ya Mahalu: Ununuzi wa Jengo la Ubalozi Italia

Benjamini Mkapa atinga mahakamani kutoa ushahidi kesi Ya Balozi Profesa Costa Mahalu

Profesa Costa Mahalu aibwaga serikali kortini
 
Rais John Magufuli amemrudishia hadhi ya ubalozi Profesa Costa Mahalu kuanzia leo, Katibu Mkuu Mambo ya Nje, Adolf Mkenda

Profesa Costa Mahalu alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Kabla ya kufunguliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh2 bilioni kesi ambayo alishinda.
chezea poti!
 
Rais John Magufuli amemrudishia hadhi ya ubalozi Profesa Costa Mahalu kuanzia leo, Katibu Mkuu Mambo ya Nje, Adolf Mkenda

Profesa Costa Mahalu alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Kabla ya kufunguliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh2 bilioni kesi ambayo alishinda.
Huyo professor ni mtu wa wap? Ni yule aliye wait kugombea jimbo la Lushoto kule tanga?
 
Back
Top Bottom