Rais Magufuli amfananisha Museveni na Mwalimu Nyerere. Je hii ni sawa?

Bavicha wanatatizo la kuwa na kumbukumbu fupi. Si ndio nyie mlikua mnatuambia kuwa Lema ni Mandela wa Tanzania au mlikua mnatania??

Kwa hiyo baada ya bavicha kumlinganisha Lema na mandela rais Magufuli amewajibu kwa kumlinganisha Nyerere na Mseven??

Kosa halijibiwi na kosa. Hasa kwa mtu mwenye hadhi kama ya Magufuli. Sio mbaya sehem nyingine ukakaa kimya kuliko kila uz kumtetea mtakatifu huyu.
 
Mwl. Nyerere ni level ya akina Nkrumah , Mandela, Kaunda and the likes.
Museveni size yake ni akina Mugabe na watu wa aina hiyo.
 
Mwl. Nyerere ni level ya akina Nkrumah , Mandela, Kaunda and the likes.
Museveni size yake ni akina Mugabe na watu wa aina hiyo.

Naam hujakosea. Museven kabadili katiba mara tatu ili tu abakie madarakan , et ndio wa kumlinganisha na Nyerere!! Hii aibu kubwa sana
 
BAVICHA Mnamfaamu Nyerere? Kwani ni wenu? Si wa CCM. Mnajitia kumpenda wakati nyinyi ni wakabila, mabepari, wezi, nk..
 
Museveni alishafeli mtihani wa Unyerere! Afadhali Mzee Mwinyi yeye alisema JKN ni Mlima na yeye ni Kichuguu.
 
Katika pita pita ya hapa na pale nimekutana na twiti ya mtu mmoja akiwa amemnukuu rais wetu JPM akimsifia mseven kuwa kama nyerere baba wa Taifa letu. Heshima aliyo nayo nyerere kwa watanzania walio wengi ni kubwa sana. Sijui kama wana JF tunakubaliana na hoja hii kwamba tukimwona Mseven tuwe kama tumemwona nyerere.

Hii kauli angekua ameongea raia wa kawaida binafsi ningemwambia atuombe radhi watanzania. Nyerere kumfananisha na watu wa ajabu ajabu si sawa. Ila kwa vile kaongea raia namba moja. Ngoja niweke akiba ya maneno ila nimekelwa sana ila sina namna kuwakilisha hisia zangu kwa ninavyo mfahamu Mseven harafu nimfananishe na Mwalimu Nyerere

View attachment 628423

Lionel Messi wa FC Barcelona anaweza kufananishwa na Juma Makapu wa Yanga SC?
 
Museveni hana sifa za kulinganishwa na Nyerere. Au sababu kampa tender ya bomba ya mafuta sasa anampa sifa zisizo lingana nae?
 
Back
Top Bottom