Kalamu Nzito
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 318
- 662
Rais Magufuli ameshinda vita dhidi ya Corona. Ndio, ameishinda kisiasa. Lakini tufahamu kua Vita dhidi ya Corona sio Vita ya kisiasa. Ninasikitika sana matabibu hawajapewa nafasi kuzungumza hali halisi ya suala hili.
SIASA IMEVAA KOTI LA KITABIBU. Nafahamu wazi kuwa jukumu la kutangaza hali halisi ilikua juu ya wizara ya afya, waziri mkuu na msemaji mkuu wa serikali.
Lakini ukitazama hawa wote wako chini ya mwamvuli wa siasa. Nasikitika tena sana kuona matabibu hawajapewa nafasi kabisa kutueleza ukweli.
Nafahamu wafanyakazi wa Serikali hula kiapo kulinda siri za serikali, lakini sifahamu kama takwimu halisi za maambukizi ya gonjwa la corona ni siri za serikali au la?!
Kusimamishwa kazi kwa wanamaabara katika maabara kuu kupisha uchunguzi ni ushindi kwa mwanasiasa. Ataonekana anachapa kazi hasa pale atakapokimbilia vyombo vya habari kulieleza hili katika upande wake tu.
Lakini je, tumepewa nafasi kuwasikiliza wanamaabara wale wana nini cha kueleza? Tuendelee kuchukua tahadhari. Kisiasa Corona tumeishinda.
Kitaalamu bado tuna vita ya kupambana.
Mungu ibariki Tanzania!