Uchaguzi 2020 Rais Magufuli amepania kurejesha kwa nguvu mfumo wa chama kimoja nchini

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,486
30,166
Tokea mwaka 1992, nchi yetu iliamua kuirejesha nchi hii kwenye mfumo wa vyama vingi na mfumo huo ukaingizwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 3(1) ambayo inatamka wazi kuwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na ni nchi ya vyama vingi" mwisho wa kunukuu

Ingekuwa Rais Magufuli anaurejesha mfumo wa chama kimoja, kutokana na ridhaa ya wananchi wake, kutokana na wananchi hao kupiga kura katika uchaguzi ulio huru na wa haki, mimi nisingekuwa na hoja ya kupinga

Lakini kwa njia hii tunayoiona tunapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, ambapo Rais huyu "analazimisha" ionekane wananchi ndiyo wameupokea mfumo huo wa chama kimoja, ndipo ninapokataa na kuiona njia hiyo ni uhuni wa hali ya juu na uvunjifu wa waziwazi wa Katiba yetu ya nchi!

Dunia nzima imeshuhudia namna ambavyo utawala huu wa awamu ya tano ulivyovunja Katiba ya nchi, kupitia kwa wasimamizi wa uchaguzi, ambao ni makada wa kindakindaki wa CCM, wakionekana kupewa "maagizo" maalum, kutoka juu, kuanzia zoezi la uandikishaji wapiga kura, uchukuaji fomu na urudishaji wa fomu hizo na namna walivyowa-disqualify, wagombea wa vyama vya upinzani, ambapo zaidi ya asilimia 95, wakakatwa majina yao, kwa kile wasimamizi hao wamekiita ni ujazaji mbaya wa fomu hizo za kuomba uongozi wa serikali hizo za mitaa

Wakati hayo yakifanyika kwa upande wa vyama vya upinzani nchini, hali imekuwa tofauti kabisa kwa upande wa Chama tawala cha CCM, ambapo wagombea wake wote wameonekana kama "malaika" kwa asilimia 100 ya wagombea wake kuzijaza kwa usahihi mkubwa na hivyo kuwa- qualify kuwa wagombea waliopita bila kupingwa!

Kutokana na hali hiyo, vyama vinane, vikiongozwa na chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema, kutangaza kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho katika huo "uchafuzi" unaotarajiwa kufanyika hapa nchini, tarehe 24 ya mwezi huu

Kumetolewa miito kadhaa na vyama hivyo vya upinzani, pamoja na viongozi wa dini mbalimbali, kuomba uchaguzi huo ufutwe na upangwe katika tarehe nyingine, chini ya Tume mpya ya uchaguzi iliyo huru, lakini miito yote hiyo, imekuta masikio ya watawala wetu yakiwa yamewekwa "pamba" masikioni na kuamua kuendelea na uchaguzi huo.

Ndipo hapo ninapoona kuwa Rais Magufuli ameamua kuivunja Katiba ya nchi hii waziwazi kabisa kwa kutaka kuurejesja mfumo wa chama kimoja kwa nguvu, bila ridhaa ya wananchi hao.

Je Rais Magufuli aendelee kuchekewa na aendelee kuimbiwa mapambio na wananchi wote wa nchi hii kwa kuungana na kujiunga na "praise and worship team for Magufuli" kwa huu uvunjifu wa Katiba ya nchi wa waziwazi kabisa?

Tunajua kuwa watawala wetu wanakuwa na kiburi na kulewa madaraka kwa kiasi cha kutisha, kwa kuamini kuwa wao ndiyo "wanaolimiliki" Jeshi la Polisi nchini na ndiyo sababu kuu, inayowafanya watishie wananchi wote kuwa atakayeupinga huo UCHAFUZI wao atashughulikiwa ipasavyo!

Nakaribisha maoni katika kuirekebisha hali hiyo ambayo inanyemelea Taifa letu ambapo zoezi muhimu sana la kidomokrasia la kutoa Uhuru kwa wananchi wa nchi hii, kuchagua viongozi wanaowataka wenyewe katika uchaguzi ulio huru na haki, ukiwa umenyongwa.

Nitoe wito kwa watawala wetu walioamua kuweka pamba masikioni na kutotaka kabisa kusikia kilio chao, kuwa zoezi la wananchi kuchagua viongozi wao katika uchaguzi ulio huru na haki, kupitia sanduku la kura, ndiyo njia pekee, inayoweza dumisha AMANI na UTULIVU hapa nchini.

Watawala wetu watakuwa wanajidanganya kupita kiasi kwa kuamini kuwa risasi, magari ya washawasha na mabomu ya machozi ya Jeshi letu la Polisi, ndiyo yatakayowadumisha wao CCM madarakani.

========
Mawazo ya wachangiaji

Usimsingizie, bali ni kutokana na utendaji uliotukuka, Watanzania, tumemkubali, na wapinzania, wameamua kwa ridhaa zao wenyewe, kuviacha vyama vyao na kuunga mkono juhudi.

Uchaguzi huu wa serikali za mitaa, ndio kazi inaanza rasmi na kumalizia 2020!.
Tulisema na kumsifu Magufuli ni kama Nyerere, ni kama Nyerere kweli hadi kwenye vyama!.

Hakuna kitu ambacho wapinzani hawakukijua kumhusu rais Magufuli, kwababu alipoingia tuu, mtaalamu huyu wa sayansi ya siasa, alitoa somo hili
P
 
Sioni tofauti au faida itakayotokana na kuwa au kutokuwa na upinzani.
Hata sasa hivi anafanya kazi kama upinzani haupo. Sasa hapo atakapoufuta rasmi, kutatokea faida gani kwake?

Bila shaka ataendelea kutafuta wapinzani hata huko ndani ya CCM ambayo yeye ni mwenyekiti.

Aina ya uongozi wake ulivyo, hata angebaki yeye na mtu wa pili pembeni, bado ataona kwamba upinzani upo, na ataushughulikia kama tunavyoona akiushughulikia huu anaotafuta kuufuta.
 
Sioni tofauti au faida itakayotokana na kuwa au kutokuwa na upinzani.
Hata sasa hivi anafanya kazi kama upinzani haupo. Sasa hapo atakapoufuta rasmi, kutatokea faida gani kwake?

Bila shaka ataendelea kutafuta wapinzani hata huko ndani ya CCM ambayo yeye ni mwenyekiti.

Aina ya uongozi wake ulivyo, hata angebaki yeye na mtu wa pili pembeni, bado ataona kwamba upinzani upo, na ataushughulikia kama tunavyoona akiushughulikia huu anaotafuta kuufuta.
Umeongea ukweli mtupu Mkuu Kalamu

Kwa mtu yeyote mwenye kutafakari mambo kwa kina, namna hulka aliyo nayo Magufuli atabaini kuwa hata kama ataua vyama vya upinzani nchini na kubaki na chama chake cha CCM, basi ataendelea na kutotaka upinzani wa aina yoyote ndani ya chama chake cha CCM

Hivyo kumfanya yeye kuwa mungu-mtu!
 
Nakaribisha maoni katika kuirekebisha hali hiyo ambayo inanyemelea Taifa letu ambapo zoezi muhimu sana la kidomokrasia ya kupewa Uhuru wananchi wa nchi hii, kichagua viongozi wanaowataka wenyewe katika uchaguzi ulio huru na haki, ukiwa umenyongwa
Wananchi ndo wenye nguvu zote kuliko jeshi na utawala wowote katika nchi zote.
Laiti kama wananchi hawa kwa umoja wao wangekataa mbinu hizi hawa watawala wasingeweza kuthubutu kulazimisha wanayolazimisha sasa hivi.

Tatizo lipo kwenye kuwaunganisha wananchi wayakatae haya yote. Wamekwishaona kwamba njia yao nzuri ya "kupiga kura" kwa uhuru na haki, nayo sasa wanapokonywa kwa mabavu.

Bila shaka, kutokana na vitisho vinavyofanywa sasa, wanapewa onyo, wakiendelea kutafuta haki hiyo kwa njia nyingine, kama maandamano, nako watashughulikiwa.

Dunia imebadilika sana enzi hizi. Kuna watawala sasa wanaoua watu wao kwa mamia, lakini husikii dunia ikipaza sauti. Mfano wa sasa hivi ni Iran. Bila shaka, watawala wanapoona hivyo, inawapa nguvu ya kuona kwamba hata wao wakiua mia kadhaa, dunia haitajisumbua na mambo yanayotokea nchini kwao.

Mifano kama hii inapotolewa, sio kuwatisha wananchi wasitafute haki zao kwa njia zozote wanazoona zinafaa. Hii ni kutahadharisha tu uwezekano unaoweza kutokea.

Na bado zipo njia nyingi nyingine wanaozoweza kuzitumia wananchi kuleta mabadiliko bila ya kulazimisha kuondoa uhai wa waTanzania.

Hivi wananchi wakigoma kutoa ushirikiano wowote kwa watawala kwa mambo mengi wanayotaka wananchi washiriki, bado watachukua bunduki na risasi kuwafuata wananchi huko waliko na kuwaua?
 
Miaka 50+ baada ya uhuru tunatakiwa kuichagua CCM na kumpigia magoti mtukufu ili tupate maji safi na salama. Tena kwa kiburi kabisa tumeambiwa tusipoichagua CCM maendeleo hatupati na la kuwafanya hatuna.
Eeenh, inaumiza sana.
Ukikosea, nenda 'katubu', utasamehewa! Miaka zaidi ya 50, tukiwa huru!
 
Asante sana kwa kuleta hii andiko hapa, ni kweli kabisa taifa letu linazidi kutawaliwa kwa nguvu za jeshi la polisi, utekaji, mauaji, na kunyimwa haki ya vyombo vya habari , na haki ya raia kuongea bila uogo ni mambo ambayo hii serikali imeumiza kabisa,lakini niseme hivi kwa ufupi, binadamu hupanga naye mungu binguni hucheka, zaburi 2. misitari 1-5. hakuna binadamu ajuae kesho, hakuna mtu mjinga duniani hii kaa mtu ambae anajiona kaa ndie anafahamu au anajua kila kitu,

La pili hakuna kitu ukiangalia au kusoma katika bibilia kinachomukwaza mungu kama mtu ambae anaumiza binadamu wenzake kwa kuwa yeye ako na nguvu, na hao binadamu hawajakosea lolote, tuko katika janga kubwa katika hii taifa letu, ukiona hata maaskofu kama wale wa kanisa katoliki wanaunga mkono unyama na ukatili unaotendwa na hii serikali, basi ujue shetani ametamalaki hapa kwetu.

Mimi kama mtu ambae anaamini katika yesu siwezi hata sekunde moja nikaombea mtu mabaya hata kaa ni mkatili vipi, lakini ikubukwe kuwa unachopanda ndicho utakachovuna, wako wapi leo kina Iddi Amin, Mobutu Seseseko, Bukassa, Sadam, Gadafi na wengine na juzi tumeshuhudia yaliyojili kule Sudan, ni muda tu mungu aseme ENOUGH IS ENOUGH, watu watamutafuta huyu mkubwa lakini atakuwa yuko motoni na shetani anayemutumikia kwa sasa hivi
 
THE SEAL,
Hakika inaumiza sana kwa mtu tuliyempa madaraka na kuamini kuwa ataiongoza nchi yetu kwa kufuata Katiba ya nchi yetu, ndiyo huyo huyo anatawsla kwa kutumia utashi wake binafsi na kwa kutumia upanga, huku tukiwaona hao tunaowaita watumishi wa Mungu wakijiunga na ile "Praise and worship team for Magufuli"

Hakika kama ulivyosema, siyo kwamba Mungu aliyetuumba, na ndiye aliyemuumba na yeye huyo anayetamba kwa hivi sasa, akiiamini kuwa Mungu aliye hai kuwa amelala fofofo........

La hasha, tumuhakikishie kuwa Mungu wetu tunayemwanini kuwa hiivi sasa ana-monitor kila kitu kinachoendea ndani ya nchi hii kwa ukaribu sana kwa vitendo vya watawala wetu kuamrisha majeshi yetu, ambayo tunayahudumia kwa kodi zetu wananchi wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa, kwa kuyaamrisha "yaue" raia yeyote anayepinga udhalimu wao!

Lakini wanachokisahau hao watawaka wetu.kuwa Mungu wetu ni mkuu kuliko kitu chochote na halinganishwi na kitu chochote hapa duniani na kazi yake hufanya kwa wakati anaoamini yeye kuwa ni muafaka, kwa hiyo tuwaamche hao watawala wetu na upofu wao na ulevi wa madaraka uliopitiliza na kuamini kuwa wao ndiyo "Miungu" wapya ambao wanastahili kuimbiwa mapambio ya kusifiwa na kuabudiwa kwa kila walitendalo!
 
Usimsingizie, bali ni kutokana na utendaji uliotukuka, Watanzania, tumemkubali, na wapinzania, wameamua kwa ridhaa zao wenyewe, kuviacha vyama vyao na kuunga mkono juhudi.

Uchaguzi huu wa serikali za mitaa, ndio kazi inaanza rasmi na kumalizia 2020!.
Tulisema na kumsifu Magufuli ni kama Nyerere, ni kama Nyerere kweli hadi kwenye vyama!.

Hakuna kitu ambacho wapinzani hawakukijua kumhusu rais Magufuli, kwababu alipoingia tuu, mtaalamu huyu wa sayansi ya siasa, alitoa somo hili
P
 
Pascal Mayalla,
Kama kweli tumemkubali watanzania wote, ni kwanini basi anaogopa uchaguzi ulio huru na wa haki, ili wananchi ndiyo wachague viongozi wao wanaowataka katika uchaguzi ulio huru na haki??

Utasemaje kuwa watanzania ndiyo tulioamua kurudi kwenye mfumo wa chama kulimoja, wakati figisu figisu zikionekana dhahiri kwa wagombea wa upinzani zaidi ya asilimia 95, fomu zao zikikataliwa na hao wasimamizi wa uchaguzi, ambao ni makada kindakindaki wa CCM, kuwa eti zimejazwa vibaya, wakati wenzao viongozi wa CCM wakiwa wamejaza kwa usahihi wa asilimia 100??

Hivi figisu figisu zote hizo, unataka kuniambia Mkuu Pascal, umetiwa upofu na umeamua kutoziona??
 
Back
Top Bottom