Rais Magufuli alikuja kama Messiah kisha akaondoka na kuacha ujumbe "MTANIKUMBUKA..."

Rais Magufuli alikuja kama Messiah kisha akaondoka na kuacha ujumbe "MTANIKUMBUKA..."

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,563
Reaction score
7,321
Ilikuwa wakati wa jioni huko vijiweni vya kawaida, pale mtaani, ambapo sisi marafiki tulikuwa tumekaa chini ya mti mkubwa, tukinywa chai moto na kutoana hadithi za maisha. Mmoja wetu, yule anayependwa na mazungumzo ya siasa, akaanza kwa sauti ya kushawishi: "Eh, rafiki zangu, mnakumbuka ile siku Magufuli alipotamka maneno hayo, 'Mtanikumbuka'? Alikuwa akizungumza na wananchi wake huko Chato, na leo, kweli tunamkumbuka. Yeye alipigania haki za watu wa hali ya chini, akafanya maendeleo makubwa ndani ya miaka mitano tu—maendeleo ambayo hakuna rais aliyewahi kuyathubutu. Alipambana na mafisadi na wala rushwa mpaka wakamchukia, wakaanza kumuita 'dictator' ili achukiwe na mataifa mengine na kumtoa madarakani. Matajiri waliohujumu mali na rasilimali za taifa walimchukia sana, lakini wananchi wa kawaida walimpenda kwa hali na mali."

Akasisitiza, "Sikieni hii: Alipokuwa rais, alijenga flyovers ili kuondoa msongamano wa magari jijini, akajenga viwanja vya ndege ili usafiri uwe rahisi. Kila baada ya miezi michache, ndege mpya zilikuwa zikinunuliwa—Bombardier, Airbus—mpaka wananchi wakaanza kukariri majina yao kama nyimbo. Sasa hivi, hicho kimekuwa nadra."

Akaanzisha mradi mkubwa wa bwawa la umeme la Nyerere ili kutoa nishati ya kutosha kwa nchi nzima.1ba7ab Alilazimisha serikali kuhamia Dodoma kutoka Dar, na kuifanya Dodoma kuinuka na kupata hadhi ya jiji halisi—sio kama ile ya enzi za Kikwete, ambapo ilikuwa kama iliyosahaulika.

Akaanzisha treni za umeme ili kuunganisha maeneo, akaboresha usafiri wa umma kupitia gari za mwendokasi huko Dar es Salaam. Jijini Mwanza, alijenga daraja refu zaidi Tanzania na Afrika Mashariki, likapewa jina lake—Daraja la Magufuli. Akajenga meli mpya kwa Ziwa Victoria, ikaitwa MV Mwanza Hapa Kazi Tu.

Huko Mtwara, akaweka usimamizi wa serikali katika uuzaji wa korosho ili wakulima wapate haki.e3af09 Mererani, akazungushia uzio, ulinzi mkali na CCTV ili kuzuia utoroshaji wa madini.

Katika viwanja vya ndege, akaimarisha ulinzi na ukaguzi ili mali na nyara za serikali zisitoroshwe. Alidhibiti rushwa mpaka ikawa ngumu kuhonga ofisa wa serikali, na TAKUKURU walichachamaa vibaya mno wakati huo. Elimu bora ilionekana kama ni kitu hakiwezekani, lakini yeye alikifanikisha kwa kutoa elimu bure na kuongeza madarasa mengi nchini. Kuna kipindi cha utawala wake hata Kiswahili kilipiga hatua kubwa Afrika kiasi kwamba nchi mbalimbali zikaanza kutaka kufanya Kiswahili kuwa lugha ya kielimu, pia uchumu akapanda mpaka "Lower Middle Income" kutokana na Juhudi za mwamba Magufuli. Lakini tunasikia leo hii uchumi umedhorota tena na hatupo hata kwenye hiyo "Lower Middle Income"

Alizuia misafara mikubwa ya viongozi isiyokuwa ya lazima, safari zisizohitajika, na matumizi makubwa kwenye sherehe za kitaifa—badala yake, akasema pesa zielekezwe kwenye maendeleo. Yeye mwenyewe hakuwa mtu wa kusafiri nje ya nchi mara kwa mara; alitumia muda mwingi kufanya ziara za kushitukiza kwenye miradi na kuwatembelea wananchi. Ilifika kipindi ambapo anapohutubia, kila mtu anawasha TV au redio kumsikiliza—hata wasiopenda siasa wakaanza kufatilia. Tukio lisilosahaulika ni wakati wa COVID-19 iliposhambulia dunia; yeye kwanza alipima uwezo wa maabara ya taifa, akatuma sampuli zisizo za binadamu bila wao kujua ili waone majibu ni ya kweli.

Hakufunga nchi kama wengine, bali aliwaamsha watu kuendelea kufanya kazi huku wakitumia mimea asili, kusali na kujikinga, akisema 'Lockdown itawazuia maskini kutafuta chakula—watakula wapi?'

Alituvusha katika kipindi hicho cha giza. Ni kama Mungu alimleta kwa miaka michache ili tuone nguvu ya kuwa na viongozi makini na shupavu wanaotetea maslahi ya wananchi, si familia zao au marafiki. Alinukuliwa akisema alikataa kufadhiliwa kwenye kampeni na matajiri ili wasije kumdai fadhila wakati atakapowawajibisha wakivunja sheria.

"Lakini sasa, baada ya Magufuli kuondoka miaka michache iliyopita, mambo yamebadilika," akaendelea rafiki yetu, sauti yake ikishuka kidogo. "Ufisadi umerudi upya chini ya utawala wa Mama Samia; vigogo waliohujumu mali wakati wa Magufuli na kushitakiwa, sasa wamerejea na wanapiga pesa bila hofu." Rais Mstaafu Kikwete, ambaye wakati wa Magufuli alikuwa hajihusishi na siasa za hamasa, sasa anahusika sana—kama yeye ndiye anashika usukani wa siasa za Tanzania, anahudhuria kila mahali na kushawishi maamuzi. Miradi mikubwa ambayo kipindi cha Magufuli ilitizamiwa sana, sasa ni kama haisikiki tena, wananchi hana taarifa kuhusu miradi mipya hata ile haliyoiacha Magufuli. Sana sana labda ujenzi wa uwanja wa mpira Arusha na Dodoma, kwa sababu wakoloni walitumia sana michezo kuwanyamazisha watu ikiwemo kuwajengea majukwaa ya michezo kuwasahaulisha kuhusu maendeleo. Hata viwanja vyenyewe ni vya Simba na Yanga timu zinazotumika kuwanyamazisha na kuwasahaulisha wananchi kuhusu maendeleo yao.

Mwingine akachangia: "Changamoto zilizojitokeza sasa chini ya utawala wa Mama Samia ni nyingi, hasa karibu na uchaguzi wa Oktoba 2025. Kuna malalamiko ya kurudi kwa udikteta, na kushitakiwa au kuzuiliwa kwa viongozi wa upinzani kama Tundu Lissu ambae ameonekana kuwa tishio kwa viongozi walioko madarakani." Ripoti zinasema kuna utekaji nyara, mateso, na kufungwa kwa wanaharakati na wakosoaji wa serikali. Mageuzi yaliyotarajiwa yamesimama, na kuna hofu ya kurudi kwa udhalimu wa zamani, ikiwemo kuwepo kwa vizuizi vya uhuru wa kujieleza na maandamano. Kiuchumi, kuna matatizo kama ukosefu wa ajira, mfumuko wa bei, na malalamiko ya ufisadi unaoongezeka, ingawa serikali inasifu maendeleo. Upinzani unaongezeka tena kwa wanachama wa CCM wao kwa wao, na kuna wanaosema hali ya mageuzi inaporomoka, hasa baada ya kushitakiwa kwa wakosoaji na kuwepo kwa utekaji husioeleweka. Hii inaonyesha wakati mgumu mbele, wakati uchaguzi unakaribia."

Sisi wengine tulikubali kwa vichwa, tukikumbuka mazuri ya Magufuli na kutazama sasa na matumaini kidogo. "Kweli, 'Mtanikumbuka'—na tunamkumbuka kwa mazuri yake."
 
Mambo aliyo yasema mgombea ni mepesi sana ambayo anaweza yafanya hata kwa miezi hii ,
 
Pumzika Mao, ila huku Kiziga na Masela Mafia wanakwangua Hadi Ukoko.
 
Back
Top Bottom