Rais Magufuli akutana na Mzee Mkapa!

Rais Magufuli akutana na Mzee Mkapa!

Matokeo kubandikwa vituoni hakuondoi kuwa CUF walifanya udanganyifu na ushahidi upo...Pia hujui kuwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi Zanzibar mgombea urais kujitangaza kuwa kashinda ni uhaini??.

Msipende kutaka muhurumiwe na kupewa urais kiujanja ujanja kwa kuaminisha watu sababu za uongo...
Ndugu wewe ni twahil au jahil?
Unajua maana ya uhaini?
Wambie wenye ushahidi wa udanganyifu wauweke wazi. Ni dhahiri wewe hunao,ungekuwa nao ungeuweka hapa ili wanaokusoma hapa wajiridhishe na ushahidi ulionao. Kama una ushahidi uweke,pokea changamoto hiyo,huna ushahidi unaropoka tu. Wingine wanaita kuropoka, domokaya.

Jiongezee maarifa hapa, huku ukijitayarisha kuleta ushahidi wa udanganyifu waliofanya CUF ulionao.

Tembelea Link Tetesi: - Vikwazo vyanukia kumshinikiza Magufuli aingilie kati ili mshindi atangazwe Zanzibar

Mimi sitaki nipewe uraisi au udiwani. Mimi si mwanasiasa. Ninachotaka mimi ni kuheshimiwa maamuzi ya wapiga kura na demokrasia ichukue mkondo wake.

Link Uchaguzi Zanzibar: Hongera Rais Magufuli kwa msimamo sahihi
 
Huyu alisema raisi akipenda ampe kazi yeyote .ampe huo mgogoro wa zanzibar ausuluhishe
nina mashaka kama Mzee mkapa ataweza kutatua mgogoro wa znz ,nahisi kama naye alikuwa nyuma ya uamzi wa jecha
 
kuna umuhimu gani kumfuata Mkapa nyumbani kwake, na kwa nini akutane na hawa wastaafu (Mkapa, JK, Waryoba, etc.) mara nyingi namna hii? watu wanaweza kutafsiri kwamba ni udhaifu na kutojiamini.
Heshima Yako,
Mkuu mi ninavyojua Urais hausomewi!! Uzoefu unasaidia sana kwenye ushauri, Hata Nyerere alikuwa akiomba ushauri,tena wakati mwingine kwa watu wa chini yake. Ukiwa Rais haina maana hutoomba ushauri,lakini kuwa Rais sio kwamba wewe ndio mjuzi wa kila jambo, anayeomba ushauri ni bora sana.
 
Masaki au Masasi? Huwa wanasema wanarudi kupumzika , kumbe bado wapo Dar kwenye vurugu!
 
ha ha ha ha ha unajua amemwambia nn hapo ndio maaana wanacheka? '' eti magu ana mtuma mkapa nenda visiwani kawaambie siku ya tar,20 machi wakavue pweza'' tu ndio maana wanacheka.
 
Ukichungulia kwa Nyuma unaona Bahati ya hindi kumbe Mzee kajenga kwny Fukwe!!!
Shati la Mzee Ben nadhan ni special order!
Kichwani Ben alikuwa vizuri sana kuliko alivyo leo Magu, ila kuishi Dar miaka mingi pamoja na kuoa kule kwa kina Fulani kulimfanya akawa mjanja fulani kitu ambacho hatukitegemei kwa Dr.Pombe aliehamia Dsm kwa mara ya kwanza 1995 alipoteuliwa kuwa Naibu waziri wa Ujenzi kwa vijiwe kama cha Palm beach vya mkapa au Vya saigon kwa kikwete hajawahi kukanyaga hivyo hatutegemei akina Machaprano kwenda kumsalimia Ikulu
Unataka kutuambia kajenga kweye hifadhi ya mikoko?
 
Kwahiyo alikwenda kumuona Mkurugenzi wa AnBen Company Limited na C.E.O wa Kiwira mining siyo?sio mbaya!!!
 
Kwahiyo alikwenda kumuona Mkurugenzi wa AnBen Company Limited na C.E.O wa Kiwira mining siyo?sio mbaya!!!

Kwahiyo alikwenda kumuona Mkurugenzi wa AnBen Company Limited na C.E.O wa Kiwira mining siyo?sio mbaya!!!
036a51c50d5ae932eeefddb395097576.jpg
 
Raisi Magufuli alipokwenda nyumbani kwa Mzee Mkapa Masaki kumtembelea!

DSC_9103.JPG







231.jpg
Huyu Mze si wa kutembelewa, ni fisadi wa hali ya juu na hastahili hata kupewa mkono. Mfungulieni mashitaka yeye na mkewe kwa kujilimbikizia mali za taifa.
 
Huyu mzee alijifanya kuigawa sudani na kuwa sudani mbili.lakini kilichotokea kila mtu anakijua .
 
Mkapa ni janga la kitaifa. Ukiachilia mbali wizi na ubadhirifu mkubwa aliofanya wakati akiwa madarakani (EPA, Meremeta, Deep Green, radar, ndege ya rais), alitekeleza kwa nguvu kubwa sera potofu za kinyonyaji za uliberali mamboleo ambazo lengo lake kubwa ni kupora rasilimali za nchi na kuzimilikisha kwa mataifa ya kibeberu. (Angalia mikataba ya madini). Akiwa ikulu, Mkapa alikuwa tu wakala (comprador) wa makampuni ya kibeberu (multinationals). Alipora kimafia benk ya NBC kutoka umiliki wa umma na kuimilikisha bure kwa kampuni ya Kikaburu ya ABSA. Kama shukrani kwa hatua yake hiyo, ABSA (NBC mpya) ikamzawadia 'mkopo' wa Sh 700m/- ambao auliurudisha kwa katika muda wa miezi 3! Ni kitendawili mpaka leo alifanya biashara gani halali iliyomwezesha kurejesha mkopo kwa muda huo. Kwa vile Mkapa sasa ni mentor wa Magufuli, na kwa vile "Birds of the same feather fly together", basi JPM aamue moja: awe baridi au wa moto. Hawezi kukumbatiana na mhimili mkuu wa ufisadi nchini na hapo hapo atuhadae eti anatumbua majipu!
 
Back
Top Bottom