Rais Magufuli akutana na Maalim Seif Ikulu leo

Hatimaye Viongozi wandamizi wa Chama Cha Wananchi CUF wametangaza kutambua rasmi ushindi alioupata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Joseph Pombe Magufuli.

Ikumbukwe awali CUF wakiwa miongoni mwa washiriki wa umoja wa Ukawa waliutangazia umma wa Watanzania kutokubaliana na matokeo lkn kwa nyakati tofauti viongozi watendaji wa Chadema na CUF wameonekana kufurahia kasi ya mabadiliko yanaofanywa na Dr Magufuli pamoja na Serikali yake.

Ni busara kwa wananchi kuwa na uzalendo katika kukubaliana na wakati katika kujikwamua kimaendeleo kuanzia ngazi ya familia. Kukubali kuyumbishwa na wanasiasa ni kupoteza muda wako wa kutafuta riziki kwa ajili ya familia yako, tufanye kazi kwa bidii na hatimaye tutapata mafanikio makubwa.
sio magufuri ametambua CUF baada ya kiboko cha wamerekani si alijifaya kichwa ngumu
 
Kuna siku walishakataa kutambua kuwa Mh JPJM ni Rais wa JMT? kama kweli walikataa kumtambua basi hawajui katiba ya JMT
Sina uhakika kama CUF wanamtambua Magufuli kama raisi lakini nadhnai wanatambua kiti Magufuli inajulikana aliwekwa kwa kura zisizo halali tofautisha
 
Mbona mimi sielewi wajameni ! si mlisema Zanzibar ni Nchi sasa Magufuri anafuatwa kufanya nini ? Anaendea kusuruhisha ugomvi kwa Jamhuri ya Zanzibar , kwani wameshindwa kumalizana wenyewe

Mbona Tanzania wanakwenda Burundi???????

Yaani unauliza majibu badala ya kuuliza swali!!!!
 
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo juu ya hali ya siasa ya Zanzibar na makamu wa kwanza wa rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharifu Hamad Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Maalim Seif ni makamo wa kwanza wa Rais wa Serikali iliyomaliza muda wake. Kwa sasa labda umuite Rais a SMZ aliyechakachuliwa
 
Wale wenzangu na mimi waliokuwa wanachonga sana "kuhusu Kusitishwa kwa Misaada ya Wamarekani MCC"

Wasubirie sasa waone kama Mgogoro wa ZNZ hautapata mwafaka muda huu.

Mnachezea pesa ya misaada nyie, eti oooohhhh!!!! tumekusanya pesa nyingi ndani ya mwezi mmoja!!!!!!

Acheni maneno ya vijiwe vya kahawa nyie ushabiki kama wa Yanga na Simba unaweka katika maisha!!!!!!
 
Kama Mtanzania Mzalendo kwanza Nianze Kwakukupongeza Kwajinsi Ulivyoanza Kazi Yakuliongoza Taifa Letu... Rais Wangu Natamani Mungu Akupe Busara na Hekima zakumaliza Mgogoro wakisiasa Wa Zanzibar na Mshindi Wa Uchaguzi Huru na Wakidemokrasia Wa October 25 Atangazwe Ili Wazanzibar Kwa Umoja Wao Waanze Mchaka mchaka Wakujiletea Maendeleo.

Pia Kwahamu kubwa nasubili Kuona Ziara zako za Ndani nawe Utafanya Kama Mtangulizi Wako Kuingia Mtego wawamiliki Wa Mahotel Nchini Kila Kukicha nikubadili Hotel Leo Ngurudoto, Kesho Serena na Keshokutwa M't Meru Hotel Wakati Majengo ya Serikali yakiachwa Kuendelea kuchakaa Kwa Kukosa Ukarabati.

Mwisho Kumulika Utitiri Wawageni Nchini Wanaoletwa Kufanya Kazi zakawaida ambazo zingefanywa na Wazalendo.
 
SEIf mwanamaridhiano sana..... .Mtu safi sana Seif.Mungu akutie nguvu kwenye Uraisi wako hapo January 2016.
 
Ili La Utitiri wa Wageni Kujaa Bongo Na Kuchukua Ajira za Wazawa (ie Yaani Hata Kazi za Ulinzi Wanaajiliwa Makaburu toka

South Africa); Ifike Maala Tusema Sasa Basi.
 
Wampe Seif urais wake mambo yaishe waendelee kujenga nchi.

ahaaaa......kikao cha kumpa shavu maalimu kikiendelea ngurdoto
avatar47491_13.gif
 
Back
Top Bottom