Cha Ndugai siwezi kukisoma kabisa.
Ila hivi vitabu wanaandika tu yale wanayotaka tuyajue. Mengine wanaficha.
Nyani Ngabu,
..kuna kitabu hiki hapa kiko Amazon ni Memoir ya Maalim Seif.
..Unless unapendekeza aandike Autobiography.
3) Mawazo, Ben Saanane, Mwangosi na Filikunjombe. Hawa nimewaweka pamoja kwa sababu ni marehemu, wengine wanaweza kufanya tafiti na kuandika juu yao.
Hata wakiandika, kuna mambo wataficha kwa maslahi ya Taifa...
Hivi Mkapa kaandika kuwa alitengana na Anna Mkapa ? Walirudiana tu Mkapa alipotaka kugombea Urais. Kama hajaandika hili basi katuficha mengi.
Katika uzinduzi wa kitabu cha Rais mstaafu Benjamin Mkapa uliofanyika mapema leo, Rais John Magufuli amewahimiza viongozi wastaafu kuandika vitabu vya maisha yao.
Hususan, Rais Magufuli amesema atafurahi kusoma kitabu cha Maalim Seif Sharif Hamad.
Kwa kweli hata mimi nitafurahi sana, mno, kukisoma kitabu cha Maalim Seif.
Harakati zake za kupigania demokrasia zimeanzia mbali sana.
Na kilele chake nadhani kilikuwa ni ule uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995!
Naamini Maalim alishinda urais wa Zanzibar.
Ila kwa inda na figisu ambazo inadaiwa ziliongozwa na Rais mstaafu Nyerere, ushindi wa kupikwa akapewa ‘Komandoo’ Salmin Amour! Hivi yuko wapi huyu mtu siku hizi??
Lakini, kweli Maalim anaweza kuandika kitabu chake na kutiririka kwa uhuru bila ya serikali kutaka kumfanyia cencorship?
Nitakitafuta kitabu cha Baba Mkapa nikisome. Najua hajaelezea mara baada yavkuwa rais alivyokataa pongezi za Kitwana Kondo na kumwambia Mzee Kondo aende kuchapisha pongezi gazetini, wakati huo huo akipokea Range Rover Vogue alilooewa kama zawadi na Andy Chande.
Kuhusu Maalim kupoko ywa urais Zanzibar, CCM ikianza kuiba kura Zanzibar tangu enzi ya chama kimoja.
Katika kura za "Ndiyo" au "Hapana" za 1985, Idris Abdul Wakil, mgombea pekee wa chama pekee cha CCM, alishindwa kupata kura za kutosha za "Ndiyo".
Matokeo yakafika mpaka vyombo vya habari.
Watu wa Daily News wakawa wako tayari kuchapisha, wakaambuwa wasubiri.
Matokeo yakageuzwa, Wakil akatangazwa rais.
Kwa aibu, alivyomaliza kipindi chake kimoja, Idris Abdul Wakil hakugombea tena urais wa Zanzibar mwaka 1990.
Kioindi cha 1988 mpaka 1990 tukiwa tunaangalia Televisheni ya Zanzibar tulikuwa tunaona kuna kada mmoja hakosi kwenye kila taarifa ya habari. Kada huyo aliitwa Salmin Amour Juma. Baadaye tukaja kujua kumbe alikuwa anaandaliwa kuwa rais wa Zanzibar mwaka 1990.
Salmin Amour hasikiki siku hizi, amepata matatizo ya macho ni kama kipofu. Ubabe wote kaishia kuwa mtu anayetegemea msaada wa watu tu, na mpaka mke wake amemkimbia.
Hiyu ni mtu aliyesifika kwa jina la "Commando".
Ama kweli, hujafa hujaumbika.
Nitakitafuta kitabu cha Baba Mkapa nikisome. Najua hajaelezea mara baada yavkuwa rais alivyokataa pongezi za Kitwana Kondo na kumwambia Mzee Kondo aende kuchapisha pongezi gazetini, wakati huo huo akipokea Range Rover Vogue alilooewa kama zawadi na Andy Chande.
Umesoma ulichokiandika? Umezingatia misingi ya uandishi kutenga paragraph za kauli za Magufuli na paragraph ya kile unachokiamini wewe?
Ndicho kilichotokea, watu wakamsitiri mzee wa watu wametoka naye mbali sana.Duh!
Sasa kama mgombea ni mmoja tu, kwenye kupiga kura kunakuwa na option ya ‘ndiyo’ au ‘hapana’ na yeye Bw. Idrisa alipata za ‘hapana’ nyingi kuliko za ‘ndiyo’? Au ilikuwaje?
Alimpa Mkapa Range Rover Vogue tulikuwa tunaliona linapaki Sea View pale.Sir Andy Chande....nakumbuka alikuwaga kwenye bodi ya wadhamini wa SRSS...
Alimpa Mkapa Range Rover Vogue tulikuwa tunaliona linapaki Sea View pale.
Nikataka kuona kama Che Nkapa ataligawa au kulirudisha.
Hakugawa wala kurudisha kitu.