Rais Magufuli ahimiza viongozi kuandika vitabu

Lingine analoweza kuandika ni lile la kuvinjari kama kapagawa kwa pesa za walipa kodi.

Mkwere ataandika jinsi alivyokutana na BOYS TO MEN na kubenbea huko Carribean!!! Atawasifia pia wabia wake wa kibiashara HOME SHOPPING CENTRE.!!!
 
Hicho yaonekana kimeandikwa na mtu mwingine...

..kweli.

..moja ya mambo niliyosikia kuwa yako ktk kitabu hicho ni jinsi Mzee Mwinyi "alivyowapiga chenga" Dr.Salim na Maalim Seif kuhusu Uraisi wa muungano wakati Mwalimu anastaafu.

..kama kumbukumbu zangu ziko vizuri kitabu hicho kilizinduliwa na Dr.Salim Salim.
 
JIWE anahimiza watu kuandika vitabu!!! Kama watu hawana utamaduni wa kusoma vitabu itawawia vigumu waandishi kuandikka kwani hata wakiandika hakutakuwa na wasomaji. Tuanzie na Jiwe mwenyewe , yeye mwaka huu amesoma vitabu vingapi na vitabu gani?
 
Katika uzinduzi wa kitabu cha Rais mstaafu Benjamin Mkapa uliofanyika mapema leo, Rais John Magufuli amewahimiza viongozi wastaafu kuandika vitabu vya maisha yao.

Hususan, Rais Magufuli amesema atafurahi kusoma kitabu cha Maalim Seif Sharif Hamad.

Kwa kweli hata mimi nitafurahi sana, mno, kukisoma kitabu cha Maalim Seif.

Harakati zake za kupigania demokrasia zimeanzia mbali sana.

Na kilele chake nadhani kilikuwa ni ule uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995!

Naamini Maalim alishinda urais wa Zanzibar.

Ila kwa inda na figisu ambazo inadaiwa ziliongozwa na Rais mstaafu Nyerere, ushindi wa kupikwa akapewa ‘Komandoo’ Salmin Amour! Hivi yuko wapi huyu mtu siku hizi??

Lakini, kweli Maalim anaweza kuandika kitabu chake na kutiririka kwa uhuru bila ya serikali kutaka kumfanyia cencorship?

Hivi jana au leo niko Tanzania hii hii?
Tanzania inayopiga kufuli magazeti tu kwa kuandika juu ya harakati za akina S. S. H.
Tanzania inayowakamata na kuwashitaki waandishi wa habari za siku hadi siku kuhusu haki za binadamu na utawala bora?
Halafu SSH aandike kitabu na JPM akibariki!
Labda naota!
Vinginevyo labda SSH anapewa ujumbe kwamba 'na wewe kaa kando kama huyu mstaafu uandike "WIMBO".
Sio kitabu!
 
Kumbe alizindua kitabu chake Marekani. Zaidi ameandika kuhusu familia yake na maisha yake kama rais. Lakini amekiri kwamba kuna mengi hakuandika ambayo hayasemeki. Sasa rais mstaafu anaogopa nini kuandika baadhi ya mambo? Maybe ni siri za taifa. Je, hizo ni siri kweli au udaku? JK hawezi kukuangusha jinsi unavyomfikiria.
Kwa mfano kumuamuru Jecha afute uchaguzi halali ambao mshindi tayari anajurikana wewe unaweza kuyaandika haya?
 
Hivi jana au leo niko Tanzania hii hii?
Tanzania inayopiga kufuli magazeti tu kwa kuandika juu ya harakati za akina S. S. H.
Tanzania inayowakamata na kuwashitaki waandishi wa habari za siku hadi siku kuhusu haki za binadamu na utawala bora?
Halafu SSH aandike kitabu na JPM akibariki!
Labda naota!
Vinginevyo labda SSH anapewa ujumbe kwamba 'na wewe kaa kando kama huyu mstaafu uandike "WIMBO".
Sio kitabu!
Kama JPM amedhamiria kweli SSH aandike kwa uhuru na uwazi kuhusu maisha yake nampongeza sana. Kwasababu wapo wengi kama SSH ambao pia wangependa kuandika lakini sote tunajua kwanini hawaandiki.
Kuna wakati JPM akiamua anasema toka moyoni. Tuzidi kumuombea kwa Mungu atuunganishe tena.
 
Siyo kila mtu tu anaweza/stahili kuandika biography, sasa Tundu Lisu aandike kuhusu nini? Bora hata Mbowe ana historia kidogo lkn bado hana cha kuandika, labda historia ya Wamachame.
Hayo ni maoni yako. mbona wengi wanataka kusikia/kusoma kuhusu maisha yake? kama mtu amealikwa HARD TALK na pia vyombo mbalimbali vya kimataifa, ni wazi anajulikana duniani kuliko wengi unaowafikiria wewe. usichanganye ushabiki wako na chuki zako, na ukweli. wewe unamdharau Tundu Lissu lakini wapo wengi wanaompenda. hiyo ni haki yao huna haki ya kuwaingilia.
Kila mtu anaweza na anastahili kuandika BIOGRAPHY. sema labda kutakuwa na tofauti ya idadi ya wasomaji. ya kwako utasoma wewe peke yako. hata mkeo sidhani kama ataisoma
 
Siyo kila mtu tu anaweza/stahili kuandika biography, sasa Tundu Lisu aandike kuhusu nini? Bora hata Mbowe ana historia kidogo lkn bado hana cha kuandika, labda historia ya Wamachame.
Wewe je, unaweza kuandika hata kuhusu hicho kijiwe chako walau..??
 
Nchini Marekani rais baada ya kustaafu huandika kitabu na baadaye hutumia proceeds ya mauzo kama pension yake na hivyo kuachana na ile pension ya serikali.

Hapa itakuwa tofauti kwa kuwa uandishi utakuwa wa kuchuja mambo mengi ambayo rais mstaafu anaona ni siri kwake hivyo asingependa watu wayafahamu jambo ambalo linapelekea kitabu kutouzika sana.

Hii ndio hali iliyopo ktk muktadha huu unaozungumziwa kwani akina Mkapa kando ya kutokuwa waungwana kwa kuomba radhi kwa maovu waliyowafanyia watanzania lkn bado tu hawako tayari kuweka wazi jinsi walivyotumia vibaya madaraka yao ili iwe kielelezo kwa vizazi vijavyo.

Sasa basi na wengine walioko madarakani tutarajie kuona watakavyo-struggle kutueleza kilichowasibu akina Azory Gwanda, Beny Saanane, Tundu Lissu pia kuhusu Clandestine Government Procurements ambazo wamekuwa wakifanya wao pamoja na Cronies wao nk. Wasife kwanza kabla hawajatueleza hayo.
 
Mimi ningefurahi sana kusoma vitabu vya hawa:
1) Freeman Mbowe
2) Tundu Lissu
3) Mawazo, Ben Saanane, Mwangosi na Filikunjombe. Hawa nimewaweka pamoja kwa sababu ni marehemu, wengine wanaweza kufanya tafiti na kuandika juu yao.
Hao hawana chochote cha kuandika.
 
Ngabu,
In between, will you be my author as am thinking about writing my Memoirs or Autobiography...
 
Ni ushauri mzuri kwa viongozi wastaafu kuandika vitabu. Lakini ni muhimu zaidi kwa viongozi waliopo madarakani kuvisoma hivyo vitabu between the lines ili kujifunza kutokana changamoto walizozipitia wenzao. Pamoja na mengi aliyoyasema Mzee Mkapa lakini tahadhari yake juu ya taifa kuanza kumeguka katika misingi ya udini, ukabila na ukanda ni suala la kutafakari kwa kina.
 
Hivi Mkapa kaandika kuwa alitengana na Anna Mkapa ? Walirudiana tu Mkapa alipotaka kugombea Urais. Kama hajaandika hili basi katuficha mengi.
That's more personal ma'am! Hata wewe huwezi kusimulia yote uliyopitia maishani. Oligwa hene?
 
"Kuandika kitabu", au "kuandikiwa kitabu."
Hao mawaziri hata makala tu magazetinihawawezi wataandika vitabu kweli?
Tanzania tunatabia mbaya sana ya kutopenda kujisomea na kuandika kuhusu mambo mbalimbali.

Nionyeshe waziri mmoja, hata hao maprofesa, aliyeandika tu makala kuhusu mambo yanayohusiana na wizara yake ili watu wayasome.
Sio mawaziri tu, Makatibu wakuu, Wakurugenzi, n.k.; huko mawizarani, hakuna anayeandika chochote.

Daily News ipo hapo, ulishaona makala yoyote ya hawa watu?

Huko Vyuo vikuu, kwenye wasomi, ndio acha kabisa. Hata kama wanachapisha kwenye vijarada vyao ili wapandishwe vyeo, ni vipi wasitafsiri habari hizo hizo ili hata raia wa kawaida azisome magazetini?

The whole thing is sanitized. 'Uongozi Institute' compiled the information through interviews.

Mkapa was a journalist, he is in a position to pen down his own thoughts with little help and we will read what is written down by him.

Kuna mwanahabari mmoja mkongwe alipata kutukushangaa jinsi tulivyozuzuliwa na mwanasiasa mmoja ambaye hajapata kuandika mawazo kwenye karatasi watu wakasoma na angalau kujua huwa anaweza nini. Hivyo ndivyo wanasiasa wetu wengi walivyo.
 
Mimi ningefurahi sana kusoma vitabu vya hawa:
1) Freeman Mbowe
2) Tundu Lissu
3) Mawazo, Ben Saanane, Mwangosi na Filikunjombe. Hawa nimewaweka pamoja kwa sababu ni marehemu, wengine wanaweza kufanya tafiti na kuandika juu yao.
Kwa taarifa yako Mbowe ni mwandishi mzuri sana
 
Back
Top Bottom