Rais Magufuli ahimiza viongozi kuandika vitabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,001
112,647
Katika uzinduzi wa kitabu cha Rais mstaafu Benjamin Mkapa uliofanyika mapema leo, Rais John Magufuli amewahimiza viongozi wastaafu kuandika vitabu vya maisha yao.

Hususan, Rais Magufuli amesema atafurahi kusoma kitabu cha Maalim Seif Sharif Hamad.

Kwa kweli hata mimi nitafurahi sana, mno, kukisoma kitabu cha Maalim Seif.

Harakati zake za kupigania demokrasia zimeanzia mbali sana.

Na kilele chake nadhani kilikuwa ni ule uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995!

Naamini Maalim alishinda urais wa Zanzibar.

Ila kwa inda na figisu ambazo inadaiwa ziliongozwa na Rais mstaafu Nyerere, ushindi wa kupikwa akapewa ‘Komandoo’ Salmin Amour! Hivi yuko wapi huyu mtu siku hizi??

Lakini, kweli Maalim anaweza kuandika kitabu chake na kutiririka kwa uhuru bila ya serikali kutaka kumfanyia cencorship?

Tafsiri rahisi ni kuwa Watanzania tumekumbushwa kutunga na kusoma vitabu ili kuandaa kizazi cha kesho kitakacho jifunza na kujisahihisha yale yaliyokwisha fanyika kwa makosa.
Hata hivyo tunakumbushwa kuwa hakuna binadamu aliyemkamilifu ila kwa msaada wa Mwenyezi Mungu.
Amani na utulivu tulionao ni kwa sababu ya sisi kama Watanzania kukumbuka tabu,mateso,udhalilishaji na utumwa mamboleo kuwa si kigezo cha kuivunja amani na utulivu tulionao hata kama tunatofautiana kiitikadi.
Huu ni wito na wigo mpana kwa watunzi wa vitabu na majarida kuchangamkia fursa hii hadimu.
 
Umesema kweli. Maalim akiandika kitabu na akawa na uhuru wa kuelezea yale mambo yaliyo nyuma ya pazia basi kitakuwa kitabu kizuri sana. Na nia hasa ya kuandika vitabu kama hivi ni kusimulia yale mambo ambayo hayajulikani au hayajawekwa hadharani.
 
JK hana cha kuandika, sana sana ataandika jinsi timu yake ya Totteringham jinsi inavofungwa baada ya kuwapiga chenga Watanzania waliokuwawa na hamu ya kufahamu nini kilichokuwa kinajiri nyumbani Tanzania. Lingine analoweza kuandika ni lile la kuvinjari kama kapagawa kwa pesa za walipa kodi.
 
Shida kubwa waandishi wa vitabu wanahitaji kitu kinaitwa INTELLECTUAL FREEDOM. Hiki ni adimu sana hapa Tanzania. Ni Nyerere tu alithubutu kuandika kitabu kinachokosoa sana serikali, UONGOZI NA HATIMA YA TANZANIA, lakini sina hakika kama kinaruhusiwa kuuzwa hapa nchini.

Kikwete, angalia kwenye kitabu chako usiambiwe UNAWASHWAWASHWA.
 
Mimi ningefurahi sana kusoma vitabu vya hawa:
1) Freeman Mbowe
2) Tundu Lissu
3) Mawazo, Ben Saanane, Mwangosi na Filikunjombe. Hawa nimewaweka pamoja kwa sababu ni marehemu, wengine wanaweza kufanya tafiti na kuandika juu yao.
 
JK hana cha kuandika, sana sana ataandika jinsi timu yake ya Totteringham jinsi inavofungwa baada ya kuwapiga chenga Watanzania waliokuwawa na hamu ya kufahamu nini kilichokuwa kinajiri nyumbani Tanzania. Lingine analoweza kuandika ni lile la kuvinjari kama kapagawa kwa pesa za walipa kodi.

..Nadhani Kikwete ameandika kitabu hivi karibuni.

..I thought alikuwa ughaibuni hivi karibuni ku-introduce kitabu chake.
 
..Nadhani Kikwete ameandika kitabu hivi karibuni.

..I thought alikuwa ughaibuni hivi karibuni ku-introduce kitabu chake.
Kilizinduliwa kimya kimya hicho, JK hachoki kwa vituko, Mwenyezi Mungu amjalie Maisha mema na starehe zake, hakuwajali kabisa Watanzania masikini.
 
Mimi ningefurahi sana kusoma vitabu vya hawa:
1) Freeman Mbowe
2) Tundu Lissu
3) Mawazo, Ben Saanane, Mwangosi na Filikunjombe. Hawa nimewaweka pamoja kwa sababu ni marehemu, wengine wanaweza kufanya tafiti na kuandika juu yao.

Siyo kila mtu tu anaweza/stahili kuandika biography, sasa Tundu Lisu aandike kuhusu nini? Bora hata Mbowe ana historia kidogo lkn bado hana cha kuandika, labda historia ya Wamachame.
 
..Kikwete naye ameandika.

..ila sijakiona amazon.

Kumbe alizindua kitabu chake Marekani. Zaidi ameandika kuhusu familia yake na maisha yake kama rais. Lakini amekiri kwamba kuna mengi hakuandika ambayo hayasemeki. Sasa rais mstaafu anaogopa nini kuandika baadhi ya mambo? Maybe ni siri za taifa. Je, hizo ni siri kweli au udaku? JK hawezi kukuangusha jinsi unavyomfikiria.
 
Katika uzinduzi wa kitabu cha Rais mstaafu Benjamin Mkapa uliofanyika mapema leo, Rais John Magufuli amewahimiza viongozi wastaafu kuandika vitabu vya maisha yao.

Hususan, Rais Magufuli amesema atafurahi kusoma kitabu cha Maalim Seif Sharif Hamad.

Kwa kweli hata mimi nitafurahi sana, mno, kukisoma kitabu cha Maalim Seif.

Harakati zake za kupigania demokrasia zimeanzia mbali sana.

Na kilele chake nadhani kilikuwa ni ule uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995!

Naamini Maalim alishinda urais wa Zanzibar.

Ila kwa inda na figisu ambazo inadaiwa ziliongozwa na Rais mstaafu Nyerere, ushindi wa kupikwa akapewa ‘Komandoo’ Salmin Amour! Hivi yuko wapi huyu mtu siku hizi??

Lakini, kweli Maalim anaweza kuandika kitabu chake na kutiririka kwa uhuru bila ya serikali kutaka kumfanyia cencorship?

Cha Ndugai siwezi kukisoma kabisa. Ila hivi vitabu wanaandika tu yale wanayotaka tuyajue. Mengine wanaficha.
 
JK hana cha kuandika, sana sana ataandika jinsi timu yake ya Totteringham jinsi inavofungwa baada ya kuwapiga chenga Watanzania waliokuwawa na hamu ya kufahamu nini kilichokuwa kinajiri nyumbani Tanzania. Lingine analoweza kuandika ni lile la kuvinjari kama kapagawa kwa pesa za walipa kodi.

Ataandika kuhusu bembea za Jamaica 🇯🇲
 
"Kuandika kitabu", au "kuandikiwa kitabu."
Hao mawaziri hata makala tu magazetinihawawezi wataandika vitabu kweli?
Tanzania tunatabia mbaya sana ya kutopenda kujisomea na kuandika kuhusu mambo mbalimbali.

Nionyeshe waziri mmoja, hata hao maprofesa, aliyeandika tu makala kuhusu mambo yanayohusiana na wizara yake ili watu wayasome.
Sio mawaziri tu, Makatibu wakuu, Wakurugenzi, n.k.; huko mawizarani, hakuna anayeandika chochote.

Daily News ipo hapo, ulishaona makala yoyote ya hawa watu?

Huko Vyuo vikuu, kwenye wasomi, ndio acha kabisa. Hata kama wanachapisha kwenye vijarada vyao ili wapandishwe vyeo, ni vipi wasitafsiri habari hizo hizo ili hata raia wa kawaida azisome magazetini?

The whole thing is sanitized. 'Uongozi Institute' compiled the information through interviews.

Mkapa was a journalist, he is in a position to pen down his own thoughts with little help and we will read what is written down by him.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom