Rais Magufuli afanya uteuzi wa Makamishina wa Jeshi la Polisi

Ufipa wanakusanya hela wawe na kituo cha uhakika kuliko kuwa na hicho cha kuchafulia jina.
Kajengeni kwanza Makao Makuu ya chama chenu yenye hadhi halafu ndo mkusanye fedha za kuanzisha kituo cha runinga. Msisahau pia kwamba mwaka huu ni uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwakani ni Uchaguzi Mkuu ni kipindi cha mwenyekiti kukikopesha chama. Sasa akianza kujilipa sijui mtapata wapi hizo fedha za kuanzisha kituo cha runinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa Majeshi ya Polisi, IGP akutana na wanahabari muda huu, fuatilia kinachojiri.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro amefanya mabadiliko ya kiuongozi kwa maofisa wa jeshi hilo baada ya Rais John Magufuli kufanya uteuzi wa makamishna wapya.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Machi Mosi, IGP Sirro amewataja makamishna walioteuliwa na Rais Magufuli kuwa ni Charles Mkumbo ambaye anakwenda kuongoza kamisheni ya intelijensia na Liberatus Sabas ambaye anakuwa mkuu wa operesheni na mafunzo.

Wengine ni Leonard Lwabuzala ambaye ataongoza kamisheni ya fedha na logistics na Benedicto Wakulyamba ambaye anakuwa mkuu wa kamisheni ya utawala na menejimenti ya utumishi na Shaaban Mlai ambaye ataongoza kamisheni ya maabara ya uchunguzi wa kisayansi.

Mbali na makamishna hao, Sirro amefanya mabadiliko ya kiutawala kwa maofisa wa jeshi hilo; James Mushi ambaye alikuwa kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma anakuwa Mkuu wa Chuo cha Polisi (CCP) Moshi wakati RPC wa Njombe, Renata Mzinga akirudishwa Makao Makuu.

Sirro amewataja makamanda wapya wa mikoa kuwa ni Amon Kakwale (RPC wa Temeke), Jonathan Shana (RPC Arusha), Marwa Mahiga (RPC Ruvuma), Salum Hamduni (RPC Njombe) na Zuberi Chembela (RPC Ilala).

Viongozi wengine waliohamishwa vituo vya kazi ni Mihayo Nsekela (ofisi ya operesheni na mafunzo), Simon Haule ambaye alikuwa RPC wa Shinyanga anarudishwa Makao Makuu na Yusuph Sarungi ambaye alikuwa RPC Songwe anakuwa mkuu wa kitengo cha kushughulikia wizi wa mifugo (SPU).

Benedict Mapugila ameteuliwa kuongoza kikosi cha bandari wakati Michael Marwa anapelekwa makao makuu Zanzibar. Sirro amesema Albert Nyamhanga na Nsato Marijani wanakwenda Idara ya Wakimbizi ambayo iko chini ya Idara ya Uhamiaji.
Ndugu zetu katika Imani mpooo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CP Nsato Marijani alikua hafananii kua Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kabisa...bora wamemuondoa aende kupiga jaramba na wakimbizi!
 
Hongereni Wateuliwa, Poleni mliorudishwa Makao Makuu jifunzeni na mbadilike!
 
CP Nsato Marijani alikua hafananii kua Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kabisa...bora wamemuondoa aende kupiga jaramba na wakimbizi!

Kamishna yupi mwenye weledi labda? Usimshambulie huyo wakati wengi wa makamishna kwa rank zote tokea ACP sio watu wa weledi

Professionalists kama kina Rtd IGP Mangu, Rtd IGP Mwema, DCP Ahmed Msangi, CP Diwani Athumani, DCP Charles Kenyela n.k wapo wachache sana

Usimshambulie Nsato tu
 
Kajengeni kwanza Makao Makuu ya chama chenu yenye hadhi halafu ndo mkusanye fedha za kuanzisha kituo cha runinga. Msisahau pia kwamba mwaka huu ni uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwakani ni Uchaguzi Mkuu ni kipindi cha mwenyekiti kukikopesha chama. Sasa akianza kujilipa sijui mtapata wapi hizo fedha za kuanzisha kituo cha runinga

Sent using Jamii Forums mobile app

Ccm Wana ofisi mbona ni mpaka waibe kura ndio watangazwe washindi? Hizo ofisi kuna kipi cha maana zaidi ya kujaza majobles waendekeza ushirikina, Majungu na fitina? Dunia ya sasa tunatumia vifaa vya kielektroniki kuwasiliana kiasi kwamba majengo sio muhimu tena. Sasa hivi kuna online TV za kumwaga hazihitaji watu wengi wala ofisi kubwa zaidi ya laptop na huduma ya internet. Huduma zote ni online, hiyo kwenda maofisini ni mambo outdated.
 
Sawa Kamanda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamishna yupi mwenye weledi labda? Usimshambulie huyo wakati wengi wa makamishna kwa rank zote tokea ACP sio watu wa weledi

Professionalists kama kina Rtd IGP Mangu, Rtd IGP Mwema, DCP Ahmed Msangi, CP Diwani Athumani, DCP Charles Kenyela n.k wapo wachache sana

Usimshambulie Nsato tu
Hujanielewa Mkuu....huyo Nsato alikua anapwaya kwenye iyo nafasi.....

Operesheni na Mafunzo mfano wake ni kipindi kile cha Venance Tossi....field sana sasa huyu Nsato kweli.....?
 
Hujanielewa Mkuu....huyo Nsato alikua anapwaya kwenye iyo nafasi.....

Operesheni na Mafunzo mfano wake ni kipindi kile cha Venance Tossi....field sana sasa huyu Nsato kweli.....?

Of course amepwaya sana sababu tangia yupo pale hatujaona hata operations kubwa kubwa. Ngoja tuone anaeingia, lakini suala la ubunifu ni tatizo sana katika nchi yetu. Watu wabunifu ni Wachache sana sehemu zote hapa nchini
 
Nimefurahi sana kusikia Kamanda Shana kahamishiwa Mkoa wa Arusha. Nimemfahamu Kamanda huyu tangu alipokuwa RPC Pwani kiukweli ni Kamanda anayejua kuhamasisha wale anaowaongoza,akiwa Mwanza kwenye tukio moja la uhalifu nilimsikia akisema kikosi chake ni kabambe kitawasaka wahalifu hao nyumba kwa nyumba,uvungu kwa uvungu na kwa kipindi kifupi alichokaa Mwanza alifanikiwa kuongoza mapambano dhidi ya majambazi na kuyaua majambazi nane.Wale vibaka vibaka na wahalifu wote wa Arusha wanaopenda kujipatia mali kwa njia isiyo rasmi wajipange Kamanda Shana anakuja huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom