Rais Magufuli afanya uteuzi wa Makamishina wa Jeshi la Polisi

Muanze na jengo la ofisi kwanza!

Wazee ndio wanaabudu ofisi, ofisi zetu watu wa kizazi kipya ni kiganjani. Jaribu kuangalia hata wanamuziki wa sasa utakuta yuko mmoja au wawili tu, zamani ilikuwa convoy la watu 40+ Kama TP Ok jazz. Dunia imebadilika sana.
 
Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama amefanya uteuzi wa Makamishna wa Jeshi la Polisi.
IMG_20190301_142307.jpeg
IMG_20190301_142312.jpeg

Dar es Salaam. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro amefanya mabadiliko ya kiuongozi kwa maofisa wa jeshi hilo baada ya Rais John Magufuli kufanya uteuzi wa makamishna wapya.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Machi Mosi, IGP Sirro amewataja makamishna walioteuliwa na Rais Magufuli kuwa ni Charles Mkumbo ambaye anakwenda kuongoza kamisheni ya intelijensia na Liberatus Sabas ambaye anakuwa mkuu wa operesheni na mafunzo.

Wengine ni Leonard Lwabuzala ambaye ataongoza kamisheni ya fedha na logistics na Benedicto Wakulyamba ambaye anakuwa mkuu wa kamisheni ya utawala na menejimenti ya utumishi na Shaaban Mlai ambaye ataongoza kamisheni ya maabara ya uchunguzi wa kisayansi.

Mbali na makamishna hao, Sirro amefanya mabadiliko ya kiutawala kwa maofisa wa jeshi hilo; James Mushi ambaye alikuwa kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma anakuwa Mkuu wa Chuo cha Polisi (CCP) Moshi wakati RPC wa Njombe, Renata Mzinga akirudishwa Makao Makuu.

Sirro amewataja makamanda wapya wa mikoa kuwa ni Amon Kakwale (RPC wa Temeke), Jonathan Shana (RPC Arusha), Marwa Mahiga (RPC Ruvuma), Salum Hamduni (RPC Njombe) na Zuberi Chembela (RPC Ilala).

Viongozi wengine waliohamishwa vituo vya kazi ni Mihayo Nsekela (ofisi ya operesheni na mafunzo), Simon Haule ambaye alikuwa RPC wa Shinyanga anarudishwa Makao Makuu na Yusuph Sarungi ambaye alikuwa RPC Songwe anakuwa mkuu wa kitengo cha kushughulikia wizi wa mifugo (SPU).

Benedict Mapugila ameteuliwa kuongoza kikosi cha bandari wakati Michael Marwa anapelekwa makao makuu Zanzibar. Sirro amesema Albert Nyamhanga na Nsato Marijani wanakwenda Idara ya Wakimbizi ambayo iko chini ya Idara ya Uhamiaji
 
Hongera nyingi ziwafikie wateule wote. Na pole kwa wale wanaotoka mikoani na kurudishwa makao makuu ingawa kimsingi maisha yataendelea kama kawaida.
 
Naona huyo wa Njombe mauaji ya watoto yamemrudisha makao makuu kusoma magazeti.
 
Back
Top Bottom