Rais Magufuli aagiza Taasisi za Umma zisizo na tija kupunguza wafanyakazi

wafanyakazi waende wapi sasa wakati kuna tatizo kubwa la ajira,watu wapo mtaani wengi hawana ajira!..huku kubana matumizi sasa kutakua ni janga

tanzania kungekuwa na tatizo la ajira wageni hasa wachina wasingejazana humu. tatizo letu sisi wa tz na hata ukilinganisha na nchi jirani tuna nyodo wakati ubavu hatuna. hatupendi kujituma,hatujui thamani ya mteja tumezoea kukaa na kusubiri mishahara bila kujali uhalali wa hiyo mishahara. sasa kazi tu na asiyefanya kazi asitafune wala asimeze.
 
Uko sahihi, hatukatai kuwapunguza... ila MKURUGENZI, msaidizi wa Mkurugenzi na waliolifikisha ATCL wako ktk OFISI, na ndio responsible key people kwanza...

So, aanze kwanza kuwasimamisha au kuwapunguza hao WAKURUGENZI, KISHA KUCHUNGUZWA, huku waliokutwa na tuhuma washitakiwe na kufilisiwa just like TRA style... kisha utakuja kwa wafanya kazi wa taasisi husika...!!!

Unaacha mkuu wa ATCL, kisha unampunguza mfagiaji, imagine just a cleaner wa ofisi, hilo ni KOSA...!!! Aanze na walio tia HASARA hayo mashirika, taasisi, ambao lazima WAKUU WA MASHIRIKA ndio wahusika...!!! Lazima tumshauri Rais hivi,....

Hapo sawa
 
Kazi za sekretari hasa ni nini kwa mfumo wa sasa wa sayansi na teknolojia ambapo watu wengi huchapa kazi zao wenyewe kwenye komputa zao sio kama zamani ambapo mtuanaandika kwa mkono na kumpa sekretari achape kwenye typewritter.

Je, kazi zao ni kukaribisha wageni? hiyo kazi yaweza fanywa na maofisa wenye kazi zingine.
Je, ni kupokea Simu za kikazi? Kazi hizo zaweza fanywa na maofisa wenye kazi husika au na muhusika mwenyewe
Je, ni kuwaandalia mabosi chai? Sio kazi yao kugeuza ofisi kuwa sehemu ya mama ntilie kuzunguka na vibirika au themos kumiminia mabosi vyai ofisini.Masekretari wengi hawana kazi za maana maofisini

Napendekeza pia vyai na vitafunwa viondolewe kabisa maofisini.watu wanywe vyai na vitafunwa makwao wakifika kazini iwe ni Kazi tu hadi muda wa kazi utakapomalizika.Ofisi nyingi ukipita unakuta mtu anazunguka na mabirika akimimina vyai na kugawa vitafunwa kama korosho,nk na kufanya ofisi zionekane kama sehemu ya uswahilini ya akina mama ntilie na baba ntilie.

Kuondoa vyai kutafanya hata wageni wa kiofisi wasikae muda mrefu wale akina penda kula na kunywa.Akifika ni kuhudumiwa na kuondoka.Pia itapunguza gharama za kuajiri wapika chai,n.k

kama ikulu imefuta kitengo cha Lishe hawa wapika chai maofisini wanangoja nini? Maofisi yafute hivyo vitengo vya lishe n.k watu wanywe vyai na kula kwa gharama zao zisiingie kwenye bajeti za walipa kodi ili walau zipunguze mzigo kwa walipa kodi jamani.

Yaani mlipa kodi anabebeshwa mzigo hadi wa mshahara wa mpika chai,chai,vitafunwa n.k tuhurumie walipa kodi jamani.Serikali ifute hizo ajira na gharama za vyai,vitafunwa,maji ya kunywa,na vyakulavitoke visiwemo kwenye bajeti ya serikali kabisa.
 
Air Takeoff Confirmation (ATC). Ina wafanyakazi 200 kati yao ma Air hostess wana makunyanzi kwa uzee na kukaa bure.

Yeyeye! mbona hao cha mtoto! nenda TRL treni nzee, reli mbovu, mwisho wa reli ni huyo TT na station master ni wazee kweli kweli, cha kushangaza hata vitabu vyao vya risiti navyo ni vya zamani kweli sasa sijui walishavitunza majumbani mwao wanachukuaga kimoja kimoja!
 
Rais John Pombe Magufuli aagiza mashirika na taasisi za umma zisizo na tija kupunguza wafanyakazi.

Pia wabunge waondolewe kwenye bodi za taasisi za mashirika na taasisi za umma.

Msajili wa Hazina athibitisha leo Jijini Dar.
Afute na kuwapunguza Askari wa Usalama Barabarani woote
 
Mie wala mnashindwa kuelewa hawa bodi ya sukari wanafanyaga kazi gani? viwanda vyote vilishauzwa wao wako ofisini wanafanya nini? au wanasubiri kutoa vibali vya kuagiza sukari? kazi zao zihamishiwe TDFA
WANA C.C.M MNAFURAHIA WATU KUFUTWA KAZI ...BADALA YA KUMSHAURI HUYO MKURUPUKAJI ABORESHE SHIRIKA LIWEVNA NDEGE ZA KUTOSHA ILI KUPANUA WIGO WA AJIRA!
Hakika tunaelekea kubaya.
 
Na walimu tunapunguzwa?

hawa maprofesa wazee nao wanapaswa waondoke hawana jipya, mtu kama semakafu na semoja sidhani kama wanatija yeyote. kuna prof moja mzee hivi yule mama hatakuongea anaongea kwa tabu kwa ajili ya uzee.
 
Hata kwenye masijala nako hakuna la maana zaidi ya kupoteza mafaili ya watu na kuwataka rushwa ili wayatafute, the only solution ni kudigitize kila kitu ili mambo yaendane na kasi ya Rais
 
Hata mi sionagi haja ya secretary kwa kweli, hata nchi za wenzetu walishaachana na masecretaries kitambo
 
Back
Top Bottom