SoC03 Rais kuteua Majaji kunaathiri Uhuru wa Mahakama

Stories of Change - 2023 Competition

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
990
1,507
UTANGULIZI
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 109, majaji wote wanateuliwa na Rais ambaye ni kiongozi mkuu wa Serikali na kiongozi mkuu wa chama dola, serikali na Mahakama ni miongoni mwa mihimili mitatu ya serikali bila kulisaghau Bunge, mihimili hii kila mmoja unapaswa kuwa huru kiutendaji na kila mhimili unamfumo wake wa uongozi.

Mahakama ni mhimili nyeti na muhimu sana ambao unagusa Nyanja zote ikiwemo serikali yenyewe hasa katika masuala ya uwajibikaji na utawala bora, sasa Rais kuwa na mamlaka kikatiba kuteua majaji ni dhahiri kwamba serikali imepewa mamlaka kikatiba kuingilia UHURU wa mahakama ambapo kiuhalisia haitakiwi.

Kitendo cha Rais kuwa na mamlaka ya kuteua maafisa wakuu wa mahakama moja kwa moja kina athiri utendaji kazi wa mahakama zote hivyo kuchochea ubora wa mahakama, na utawala wa kisheria kudhorota kwa kuwa maamuzi ama hukumu nyingi zinazo husu serikali na viongozi wa juu wa serikali zitatolewa kwa hofu ama kama zawadi kwa mteule ambaye ndiye mkuu wa serikali. Pia mashauri mengi yanayo muhusu Rais na serikali yake yanakuwa katika nafasi kubwa ya kufutiliwa mbali hata kama ni mashitaka yenye tija sana kwa ustawi wa taifa.

Kitendo cha Rais kuwa mteule wa maofisa wajuu wa mahakama hasa katika nchi inayoendelea ni dhahiri kwamba Rais yupo juu ya sheria na hili lipo wazi kabisa maana mara kadhaa Rais alisikika hadharani katika mikutano yake ya kikazi inayuhusu upinzani akisema “Flani aliniambia kwamba mama naogopa kurudi nina kesi, Nikamwambia rudi Nitazifuta”, unaweza kujenga picha kupitia kauli hii kwamba yaani Rais ana uwezo wakuzifuta kesi mahakamani kama DPP.

Unapokuwa katika mazingirga kama haya mahakama inakuwa butu na inakuwepo kutimizi wajibu na sio usawa wa haki kwa wote.

NINI KIFANYIKE
Majaji kama maofisa wakuu wa mahakama wenye wajibu wa kusimamia haki na usawa wa watu wote wachaguliwe kwa utaratibu maalumu, itungwe sheria ambayo itaelezea mchakato wa kuwapata majaji wa mahakama zote ambapo katika mchakato huo serikali isiwe na nguvu ya kuingilia mchakato huo.

NAMNA WATAKAVYOPATIKANA
Iundwe kamati maalumu ya kuajiri majaji (Judges recruitment committee) wote ambayo itakuwa chini ya Jaji mkuu aliyopo madarakani, kamati iwe na wajibu wa kuaandaa sifa na miongozo ya ziada kwa wale wote wanaotaka kuomba nafasi za kuwa majaji, nafasi za kazi zitatangazwa na wote watakao omba watafanyiwa udahili na kamati husika kwa kuzingatia miiko ya nafasi hiyo na taaluma hiyo udahili utalenga kupata idadi husika inayohitajika kwa wakati huo kwa ajili ya ushindani.

Majina yawatakaopitishwa na kamati yatawekwa hadharani kupitia gazeti la serikali na runinga ya serikali, wagombea hao watakuwa na siku kadhaa za kuomba kura mbele ya majaji wa mahakama zote waliopo madarakani ambao watakusanyika kwa utaratibu utakao wekwa na kamati, wagombea watajinadi mbele ya majaji waliopo na kuulizwa maswali ya wazi ambayo yatajibiwa papo kwa papo.

Baada ya hapo utafanyika uchaguzi wa siri ambapo kutakuwa na viwango flani vya kura ambazo ili mgombea awe amepita ni lazima azifikishe, nje ya hapo hata kuwa amepitishwa kuwa jaji.

Majina ya wale waliofikisha alama stahiki yatawekwa wazi, na baadae wataapishwa kwa mujibu wa sheria ambapo jaji mkuu ndiye atakayekuwa na jukumu hilo kisheria.

Rais atapelekewa nakala ya majina ya majaji wateule na walio apishwa kwa ajili ya kuisaini na kuwatambua rasmi, kusaini ama kuto saini kwa nakala hiyo hakutaweza kuwazuia majaji wateule kuendelea na majukumu yao maana tayari watakuwa wameapishwa wanakiisi kiapo hicho.

Vivyo hivyo hata jaji mkuu atapatikana kwa kuchaguliwa lakini sharti awe amehudumu kama jaji wa mahakama ya juu kwa kipindi kisichopungua miaka kumi.

Kabla ya kupangiwa vituo vyao vya kazi, majaji waeule waende mafunzo maalumu ambayo yatatolewa na wataalamu maalumu ambao wamehudumu kama majaji kwa kipindi kirefu kwa muda usiopungua miezi miwili ndipo wapangiwe vituo vya kazi.

MAJUKUMU NA WAJIBU WA KAMATI YA KUAJIRI MAJAJI
  • Kutunga kanuni, miongozo na vigezo vya mtu kuwa jaji.
  • Kutangaza nafasi za kazi za majaji na utaratibu wa kuomba.
  • Kuchuja majina ya waomba ridhaa ya kuwa majaji.
  • Kusimamia midahalo yote ya waomba ridhaa kipindi cha uchaguzi.
  • Kuhakikisha miongozo na miiko ya uchaguzi inazingatiwa wakati wa uchaguzi.
  • Kusimamia uchaguzi na kutangaza matokeo.
  • Kuaandaa bajeti ya zoezi zima la uchaguzi
  • Kuandaa nafasi za ajira za majaji pale inapohitajika.
  • Kuzuia vitendo vya udanganyifu wakati wa uchaguzi.
ATHARI ZA RAIS KUWA NA MAMLAKA KISHERIA KUTEUA MAJAJI
  • Uhuru wa mahakama unaminywa.
  • Utendaji kazi wa mahakama unadhorota.
  • Usawa katika utoaji wa haki unapungua.
  • Ni chanzo kikubwa cha rushwa katika mahakama.
  • Rais anakua juu ya sheria.
  • Ni chanzo cha ubadhilifu ndani ya serikali maana nguvu ya kuwashitaki wabadhirifu ambao ni viongozi wa juu.
 
Ni sahihi katika mpya inahitajika lkn kabla ya katiba mpya kupatikana swali ni je haya yaliyopo kwenye katiba hii yanafuatwa?
 
yapoyanayofuatwa,na yale yanayopuuzwa lakini hoja yangu imejikita katika namna uhuru wa mahakama unavyonajisiwa nanini kifanyike bila kujali katiba inabadilishwa au laaa
 
Hata speaker wa Bunge na naibu Wake pia

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom