Rais kuna jambo inabidi aelezwe(aelimishwe)

Rais kuna jambo inabidi aelezwe(aelimishwe)

Unamwelimisha Rais? Mm nionavyo kwa katiba yetu Rais ndio mwalimu wa kila mtu. Haelimishiki labda anashauriwa
 
Hakuna kama magufuli tanzania watu walirembwa sana magu piga kazi
ni kweli hakuna kama magufuli maana toka dunia imeumbwa huyu ndiye rais pekee ambaye amekiri hadharani kuwa ni kichaa na anachagua vichaa wenzie kuwa viongozi
 
Ziara hii ratiba inaonyesha asilimia kubwa atapita kwenye maeneo yenye upinzani mkubwa, hivyo jiandae kusikia mengi.

Bado tunasubiri Mbeya na Songwe huko ndio hatari zaidi jamaa anahasira nako vibaya.

Ukizingatia Mbeya walimwimbisha pipooooooooozzzzz kwa lazima....hatujui nini kitatokea.
 
Tatizo kubwa ni kwamba hana mpangilio wa hotuba, toka Chato hadi Musoma hotuba ni hiyo hiyo anarudia rudia tu maneno.
 
mie namcheki mheshimiwa live tu hapa mana sina la kuongea,jamaa kashatuwahi, no way out
 
Naamini ukipewa mitihani waliyoifanya watoto wa darasa la saba jana na leo,wewe sekondari huwezi kwenda kwani kufikisha hata wastani wa 50 utashindwa maana wewe kichwa maji sana..
Kama aliyeongea ana PHD nitashindwaje mimi kufaulu la saba,
 
Tatizo kubwa ni kwamba hana mpangilio wa hotuba, toka Chato hadi Musoma hotuba ni hiyo hiyo anarudia rudia tu maneno.
Sasa kama hana mpangilio - Imekuwaje aongee hayohayo ziara nzima? Si angekuwa anachanganyachanganya?
 
Atwange tu iko siku tutaelewana. Tiini mamlaka iliyowekwa na Mungu
 
Naona katika ziara hii kichaa kimekuwa kikubwa sana kama kile cha wakati wa tetemeko la Bukoba


Kiuhalisia sasa hivi ni mwezi mchanga nadhani hata madaktari wake walitakiwa wamwambie sio muda muafaka wa kufanya ziara kabisa... maana sio kwa ukichaa huo aisee sasa hivi kiko mahali kwake... na ukiangalia hata vichaa mtaani sasa hivi wako juu sana hata kama alikuwa havui nguo sasa hivi ndio kimepamba moto haswa
 
Narudia Tena. Tunahitaji formula/utaratibu wa kugawana pesa za maendeleo. Maendeleo yasipelekwe kwa hisani ya Rais au waziri. Wenzetu wakenya wameweza hili. Kwasasa serikali inablackmail wananchi kuwa mkichagua upinzani basi msahau maendeleo.
 
Rais Magufuli amekuwa akihutubia mara kadhaa na kuacha maswali mengi kwa hadhira anayoihutubia.
Awali kulikuwa na kauli "wakati nakulipa mshahara". Alikuwa akiitumia kufanya watumishi wafuate mawazo yake tu. Mfn. Unamtangaza mpinzani kashinda uchaguzi wakati nakulipa mshahara.
Pili, "nimewapa hela wakati hawakustahili". Hii imetokea huko Ukerewe akifafanua kuwa Ukerewe hawakustahili mradi wa maji ila ni hisani zake.
Tatu, akiwa Musoma anasema anawajengea barabara "kwa heshima ya Wasira", na sio sababu Bulaya amewasilisha hoja bungeni.

Katika utata kama huu utaona anajisifu kuwa yeye ndo anaamua fedha iende wapi na sio bajeti inayopitishwa na bunge.
Pili anazifanya fedha za Tanzania kuwa kama mali yake kuwa atoe kama fadhila.
Naomba waliokaribu nae wamwambie, kazi yake ni kuleta maendeleo na sio kujifanya anatoa msaada. Na akizingua tutamtoa tutaweka mwingine.
Pia asitugawe maana watu wa Ukerewe wanastahili kama wanavyostahili watu wa Chato au Mwanza maana wote ni raia wa Tanzania na wanalipa kodi kwa mujibu wa sheria kwahiyo maendeleo yoyote ni haki yao kupata.
Wito akiendelea na kauli hizi TRA watapata shida sana kukusanya kodi maeneo ambayo "hayastahili".
Hivi ilani inayotekelezwa Tazania ni ya chama gani.
 
Mi naona mzee kama anajuta hivi,
Na hii 'kisaikolojia inaitwa defensive mechanism, ameshaona amekula wa chuya ila anatoa kauli kama hizi akiona kama watanzania wanamsonga kwa makosa yake, lipo jambo la kumsaidia ni kumshauri, angalia papara zilivyotufanya tunalipa madeni leo hii, 🙁🙁 ona kauli zake zinavyompinga leo hii, ameona na yeye awe mlalamikaji sasa, ishu ya sisi kuibiwa gesi na mabepari nani tumempa nguvu ya kupambana na hilo? kama hana njia ya kupambana nao kwa nini asituombe ushauri., mbona tuna wana diplomasia wengi tuuu, au nao hawaamini? mbona tuna wanasheria wengi tuu? hawaaminiki?


suala la kusema kwamba ameshughulikia suala ukerewe kwa hisani yakee, ina maana hawastahili kupata hiko alicho kifanya?
tujitafakari kwa kweli
 
Bulaya hakupaswa kupiga kura ya hapana kwa bajeti ambayo anategemea ikamilishe miradi aliyotumia kuombea kura.

Rais amefanya vyema kuweka rekodi sawa, kuwa fedha za utekelezaji wa mradi huo umetokana na nini, ili asije wahadaa wananchi kuwa mradi umekamilishwa kwa kujudi zake kumbe yeye ndiye alikuwa kikwazo kwao.
 
Si halali kusema wanaoishi sehemu zinazoongozwa na upinzani hazina haki ya kupata maendeleo,. Kama ni hivyo na kodi wasilipe . Maana kodi ndiyo inayoleta maendeleo na hakuna kinachoonesha wanachama Wa CCM na majimbo yao ndiyo wanaolipa kodi kuliko wapinzani . Huo ndio ukweli na kamwe haubadiliki. Matamshi kinyume hapo ni vitisho batili na kunyanyasa watu kwa Sera zao. Mwalimu alituasa kuwa ubaguzi ukiuanza hakuna mwisho. Mkimaliza wapinzani mtabaaguana hata ndani ya CCM wenyewe kwa wenyewe. Dunia ya Mungu tembea polepole hakuna mwenye haki zaidi ya mwingine , mwenye imani ya ubaguzi acha , mwisho wake itakutafuna hata kama si Leo , ni kesho ukitoka madarakani,. Rais alisema msemakweli ni mpenzi Wa Mungu na huo ndio ukweli bila chenga.
 
Back
Top Bottom