Rais kumzawadia mtoto pipi alikuwa na maana gani?

Mkuu Kaizer,
Chukua tano kabisa.
Hapa inabidi tu kukubaliana na maneno ya FMes kuwa viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe. Mwakani watu watapewa PIPI za watu wazima (Khanga, ng'ombe, T-Shirt za "Yanga", maneno matamu nk) na jamaa hata kwenye gari hatashuka. Tutafurahia uzuri wa gari lake na maneno yake na uzuri wa mgombea. Tutampa kura zetu huku tukionyesha jino la mwisho mdomoni mwetu.
Kweli Bob Marley alikuwa na akili sana alipoimba "Jikwamueni kutoka kwenye UTUMWA wa ki-akili".

Kuna PIPI za watu wazima zitagawanywa mwakani? ...na kwamba zitagawanywa jamaa akiwa ndani ya gari? Dah!

Sikonge ulichoandika hapo kwenye nyekundu JK hatapendezwa nacho mkuu.
 
Wajibu ni wa kwetu sote kuanzia pale tunapochagua viongozi na kuhakikisha tunapowachagua wanafanya kazi kama walivyoahidi watafanya. Sasa kama mnamwona raisi hafanyi kazi yake kama alivyoahidi na kama anavyopaswa basi alaumiwe na hizo lawama ziendane na makosa yake. Lakini kwa yeye kumpa pipi dogo na nyinyi mnamshikia bango kama vile kalisababishia taifa hasara kubwa sana is beneath contempt!

Na wajibu wa kuleta maendeleo sio wa raisi peke yake bali taifa zima.

NN,
Haya ndiyo maneno. Na ndiyo ninachokisema muda wote. Tangu mwanzo nimesema kuwa mie silaani wala simfagilii kwa hili. Ila ingelikuwa vema kama ....(maelezo yangu ya nyuma).

Kama Rais, awajibike kuhakikisha Wazazi tunakuwa na uwezo wa kuwahudumia watoto wetu. Na sisi Wazazi tuhakikishe tunachangua kiongozi mzuri na mchapa kazi ili aweze kutatua matatizo yetu. Pia na sisi tufanye kazi kwa bidii.

Hebu angalia hiki kituko cha Wakenya kuja kununua vitunguu Tz, na kuvibeba Kenya na wao kwenda kuviuza EU. Hivi kwa nini viongozi wetu wasitutafutie soko la moja kwa moja EU? Wakenya wamepataje? Hapo ndipo unakuja uwajibikaji wa Rais na timu yake. Tukishajaa mapesa, wenyewe tutawanunua pipi wanenu na yeye awe busy na mambo mengine.
 
Tutabishana sana ila ukweli unabaki kuwa:

1. Huyo mtoto alichaguliwa na Walinzi wake na kuletwa pale karibu na gari la Rais.

Hii ni statement of fact. Unajua maana ya statement of fact wewe? Sasa basi kwa vile unasema kama unajua mimi nina swali. Wewe umejuaje kuwa dogo alichaguliwa na walinzi wa raisi na kupelekwa karibu na gari? Ulikuwepo au una guess tu?

Tungeliona kundi la watoto wamezunguka gari tungeliamini kuwa ilikuwa imetokea kibahati.

Kipi ni kipi ndugu Sikonge? Unajua kuwa dogo alichaguliwa na walizni wa raisi kwenda kupewa pipi au unaamini? Hivi unajua maana ya "kujua" na "kuamini"? Maana "tunge" tunge zimeanza kuwa nyingi....ishara ya kutokuwa na uhakika na ukisemacho.

Mwenyewe umesema kuwa kuna mkono wa mtu kavaa Kaunda suti. Kwa hiyo utake usitake, huyu mtoto alichaguliwa (kuandaliwa) na kupelekwa pale kwa Kikwete.

Rejea tena nilichoandika. Sijasema kwa uhakika kuwa ni mkono wa mtu kwenye Kaunda suti. Nime guess tu.

2. Kikwete alikuja na hizo Pipi kutoka huko alikotoka. Hizo pipi hazikuanguka kutoka mbinguni kama Mana.

Unajuaje alikuja nazo na alikuwa ametoka wapi? Au wewe ndio ulimsaidia kuzipakiza kwenye gari? Ukisema ndiyo nitakuacha. Ukinipa source inavyosema unavyodai wewe ubishi utaisha.

Alifahamu kabisa kuwa nabeba Pipi na ntaenda kuzigawa kwa kitoto chenye bahati.

Hehehehehehee...hii kali ya kufunga wiki. Either umekuwa clairvoyant au Kikwete mwenyewe alikuambia. Again, which is which? Lol

3. Alipofika pale akaagiza wamletee huyo mwenye bahati na kijana akaletwa huku wengine wakiambiwa kaeni mbali maana hatuwaoni. Labda mkuu napo hapa utakuja na madai nilete ushahidi. Ushahidi sina na kwa niseme kuwa "wenyewe walijipanga na wakakaa mbali". Dogo akaja na bila kujua kinafanyika nini, Dogo akaona mkono unatoka na MAPIPI kibaooo. "Salaleee, Mungu anipe nini?" Dogo ni kufungua mikono na kumwagiwa mipipi. Hakumuuliza hata kama wazazi wanamruhusu ale Pipi maana anaweza kuwa na kisukari.

Kama hayo maelezo nayo unataka ushahidi, basi na mimi ntaomba ushahidi kama kweli ni wewe leo unaandika au ni nduguyo.

Wheeeeew!! Unajua hapa ninaweza kuwa nabishana na mtu aliyetoka kuzimua wanzuki usiku kucha na kabla ya kuzima kaamua kuingia JF!! Basi bana mimi sitaki tena kubishana na wewe. Ngoja nitafute mwingine wa kubishana naye.
 
[
=Zakumi;559593]Sio wajibu wa rais kuwawezesha watu.
Upo sahihi hapo

Rais anachoweza kufanya ni kukuhamasisha tu au ku-regulate sheria ambazo zitafanya uongeze kipato chako au ujitume zaidi

Contrary to what you have just preached

Vilevile JK alizaliwa kama binadamu wengine. Hivyo yeye kuwa rais, hakufanyi aache yale ubinadamu wake na kuwa super-binadamu.

Sawa kabisa

Kuna kitu sielewi!

Kasi Mpya, Nguvu Mpya, na Ari mpya kama haitoshi maisha bora kwa kila Mtanzania.
 
JF inafurahisha!

Raisi anasafiri na mapipi kwenye gari, mabaki anagawia watoto ambao anajua kabisa kama kiongozi wa nchi wanahitaji zaidi ya pipi....tunatofautiana sana katika kufikiri. Wanaosupport eti kama mzazi well, mimi namwona Kikwete ni zaidi ya hapo kama head wa state.....anamajukumu mengi....sidhani kama Obama anaweza fanya hilo, ama Sarkozy na other serious leaders!

We are too cheap! Nilitegemea JF watu wanafikiria zaidi ya wale walevi wa kangala na wanzuki usukumani kumbe sivyo!

Ulitaka agawe nini? na angegawa kwa wangapi? si ndo watu wangekuwa wanakaa tu na kusubiria zawadi za raisi na ndo ingekuwa JK anapendelea na vitu kama hivyo jamani..
Leave out Sarkozy na huyo Barak, huwezi fananisha na JK pia Tanzania yetu kabisa. Hapo ndo tunapokosea sometimes kwenye mifano.
Sema ulitaka ampe nini huyo mtoto ha hivi ni mpita njia tu?
 
....sidhani kama Obama anaweza fanya hilo, ama Sarkozy na other serious leaders!

Wewe unaishi wapi wewe? Cheki link hiyo ya Obama akienda trick or treating na watoto wake. Kwenye trick or treat watoto huwaga wanapata ni nini kama sio candy? There is absolutely nothing wrong with the president taking a few minutes to mingle with the folks. Huyo Obama wako uliemtolea mfano hafanyi kazi masaa yote. Saa ingine anaenda kucheza basketball. Tena ile tennis lawn ya White House wamei-convert kuwa basketball court sasa hivi na jamaa huwaga ana shoot hoops.

Na huyo Sarkzoy wako juzi juzi kazimia baada ya kutoka kukimbia. So kufanya mazoezi kwa saa moja au mawili kuna tofauti gani kubwa na JK ku mingle na wananchi? Au mbona Obama huwaga anaenda Five Guys kununua burger? Clinton mbona alikuwa anatinga mwenyewe MickeyD's kununua Big Mac...ina maana alikuwa hana kazi ya kufanya? Geeeez

Link hii hapa http://www.huffingtonpost.com/2008/11/01/obama-trick-or-treating-v_n_139965.html
 
JF inafurahisha!

Raisi anasafiri na mapipi kwenye gari, mabaki anagawia watoto ambao anajua kabisa kama kiongozi wa nchi wanahitaji zaidi ya pipi....tunatofautiana sana katika kufikiri. Wanaosupport eti kama mzazi well, mimi namwona Kikwete ni zaidi ya hapo kama head wa state.....anamajukumu mengi....sidhani kama Obama anaweza fanya hilo, ama Sarkozy na other serious leaders!

We are too cheap! Nilitegemea JF watu wanafikiria zaidi ya wale walevi wa kangala na wanzuki usukumani kumbe sivyo!

Msiwe Obsessed na Obama wengine tunabeba mabox karibu WH. Obama anacheza na watoto. Na anapokuwa na watoto anakuwa sio serious kabisa.

slide_396_10523_large.jpg
http://images.huffingtonpost.com/gadgets/slideshows/396/slide_396_10523_large.jpg
 
Ulitaka agawe nini? na angegawa kwa wangapi? si ndo watu wangekuwa wanakaa tu na kusubiria zawadi za raisi na ndo ingekuwa JK anapendelea na vitu kama hivyo jamani..
Leave out Sarkozy na huyo Barak, huwezi fananisha na JK pia Tanzania yetu kabisa. Hapo ndo tunapokosea sometimes kwenye mifano.
Sema ulitaka ampe nini huyo mtoto ha hivi ni mpita njia tu?

Sorry

JK gawa pipi kwa wingi hakuna tunachohitaji kwako Mr presidaaa! Nina mtizamo tofauti sana hili ....msinigawanye vipande vipande...
 
Rais na serikali yake wanajukumu la kuhakikisha mazingira bora kiuchumi,kisiasa na kijamii kwa wananchi wao. Mtoto wako anaumwa, haendi shule, hana pa kulala unataka rais aje achukue majukumu yako kaka baba wa familia.

Watanzania tubadilike serikali na rais wake haiwezi kutufanyia kila kitu, sisi wenyewe ndiyo kiini cha maendeleo yetu binafsi.

Nampongeza rais wetu Kikwete kwa kujitahidi kwa nia moja kutoonyesha binadamu hasa baba wa familia anatakiwa awe mfano wa upendo, amani na utulivu.

Nyuki uko Tanzania au nje ya nchi? Hayo mazingira bora unayosema wewe ni hayo ya shule watoto 600 wasio na madawati mwalimu mmoja? Na kina mama 500 wanaokufa kila siku kwa kutopata matibabu wa kujifungua?
 
Msiwe Obsessed na Obama wengine tunabeba mabox karibu WH. Obama anacheza na watoto. Na anapokuwa na watoto anakuwa sio serious kabisa.

slide_396_10523_large.jpg

Ewaaaaaaa....heheheheee...huyu Obama huyu hayuko serious huyu. Yaani badala ya kufanya kazi zenye tija kwa taifa anaenda Advetntureland kuchezea vigari na mtoto wake. Hafai huyu...Lol
 
Hii ni statement of fact. Unajua maana ya statement of fact wewe? Sasa basi kwa vile unasema kama unajua mimi nina swali. Wewe umejuaje kuwa dogo alichaguliwa na walinzi wa raisi na kupelekwa karibu na gari? Ulikuwepo au una guess tu?

Kipi ni kipi ndugu Sikonge? Unajua kuwa dogo alichaguliwa na walizni wa raisi kwenda kupewa pipi au unaamini? Hivi unajua maana ya "kujua" na "kuamini"? Maana "tunge" tunge zimeanza kuwa nyingi....ishara ya kutokuwa na uhakika na ukisemacho.

Rejea tena nilichoandika. Sijasema kwa uhakika kuwa ni mkono wa mtu kwenye Kaunda suti. Nime guess tu.

Unajuaje alikuja nazo na alikuwa ametoka wapi? Au wewe ndio ulimsaidia kuzipakiza kwenye gari? Ukisema ndiyo nitakuacha. Ukinipa source inavyosema unavyodai wewe ubishi utaisha.

Hehehehehehee...hii kali ya kufunga wiki. Either umekuwa clairvoyant au Kikwete mwenyewe alikuambia. Again, which is which? Lol

Wheeeeew!! Unajua hapa ninaweza kuwa nabishana na mtu aliyetoka kuzimua wanzuki usiku kucha na kabla ya kuzima kaamua kuingia JF!! Basi bana mimi sitaki tena kubishana na wewe. Ngoja nitafute mwingine wa kubishana naye.

NN,

Ile habari ya mwanzo umeandika hadi tumekubaliana. Ila hii umevuruga tena.
- Sawa mkuu, yule mtoto hakuchaguliwa na alizuka tu.
- Ule haukuwa mkono wa mtu ila ulikuwa mkono wa ....... (who knows?)
- Hizo pipi nazo zilizuka tu ghafla mtoto alipozuka mlangoni mwa gari.
- Sina source kwa hiyo habari yangu yote na Ku-guess kama wewe....
- Kuzimua huwa ni asubuhi baada ya kupata kinywaji usiku kucha.
- Kama napata kinywaji usiku kucha sizimui.
- Umejuaje nilikuwa nakunywa Wanzuki na si Machicha?
- Kwa taarifa yako jana nilikuwa napata ..............enheee Wanzuki.
 
Na huyo Sarkzoy wako juzi juzi kazmia baada ya kutoka kukimbia. So kufanya mazoezi kwa saa moja au mawili kuna tofauti gani kubwa na JK ku mingle na wananchi?

Kiongozi, hii naona haihusiani kabisa na JK kugawa pipi kwa mtoto yeye akiwa kwenye official duty ziarani huko aliko kuwa. Link yako ya Barak inaonyesha yuko na familia yake happily na wala hajasimamisha baracade yake kugawa candies labda kama nimekosea kuangalia.
 
Kumbukeni hizi staili za pipi ndo mwanzo wa mimba za umri mdogo kwa mabinti, kumbukeni tena sasa tunaelekea kwenye uchaguzi, sasa watoto tunawapa pipi, watu wazima kofia, khanga, na pilau.

Halafu kumbukeni huyo ni rais kwanini atembee na pipi? Kwa hiyo anamakusudi yake! Pia kumbukeni hata ukoloni uliingia kwa staili ya kupewa pipi sasa wale walikuwa baba zetu?

Fikiria kwa undani mzee huyo mtoto anahitaji msaada na sio pipi!
yah man point taken.....

alafu lol heading ya thread "raisi amzawadia pipi......." kiswahili kimekua ati....
 
NN,

Ile habari ya mwanzo umeandika hadi tumekubaliana. Ila hii umevuruga tena.
- Sawa mkuu, yule mtoto hakuchaguliwa na alizuka tu.
- Ule haukuwa mkono wa mtu ila ulikuwa mkono wa ....... (who knows?)
- Hizo pipi nazo zilizuka tu ghafla mtoto alipozuka mlangoni mwa gari.
- Sina source kwa hiyo habari yangu yote na Ku-guess kama wewe....
- Kuzimua huwa ni asubuhi baada ya kupata kinywaji usiku kucha.
- Kama napata kinywaji usiku kucha sizimui.
- Umejuaje nilikuwa nakunywa Wanzuki na si Machicha?
- Kwa taarifa yako jana nilikuwa napata ..............enheee Wanzuki.

Heheheheee...wee bana tumeshamalizana. Hakuna ubishi tena. Safari ijayo unambie basi una wanzuki...uchoyo si mzuri ndugu yangu
 
Nyuki uko Tanzania au nje ya nchi? Hayo mazingira bora unayosema wewe ni hayo ya shule watoto 600 wasio na madawati mwalimu mmoja? Na kina mama 500 wanaokufa kila siku kwa kutopata matibabu wa kujifungua?

Je kuna correlation gani hapa kati ya kumzawadia mtoto utamu na matatizo uliyotaja hapa?
 
...zawadi ni zawadi, huwezi kumchagulia mtu atoe/apokee zawadi gani au yenye thamani gani.

mbona hamumpongezi binti Makamba na Vodacom kwa zawadi zao? ...msijitie upofu kwenye sera (indirectly) za CCM.
Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba akimwambia jambo mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi kilimani iliyopo kitunda wilaya ya Ilala alipotembelea shule hiyo na kutoa msaada wa madawati 70 ikiwa ni kampeni ya mfuko huo wa kutoa msaada wa madawati 400 katika shule za msingi mkoa wa Dares Salaam wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 32.
 
Kiongozi, hii naona haihusiani kabisa na JK kugawa pipi kwa mtoto yeye akiwa kwenye official duty ziarani huko aliko kuwa. Link yako ya Barak inaonyesha yuko na familia yake happily na wala hajasimamisha baracade yake kugawa candies labda kama nimekosea kuangalia.

Pointi bado ni ile ile. Ubaya uko wapi hapo ku take time na kujumika na wananchi? Iwe familia yako au wananchi wengine? Kwani alivyomgawia dogo hizo pipi ilichukua muda gani, siku nzima? Na nini kilichoenda mrama kwa sababu ya yeye kumgawia dogo pipi?

Halafy "baracade" ndio nini?
 
JF inafurahisha!

Raisi anasafiri na mapipi kwenye gari, mabaki anagawia watoto ambao anajua kabisa kama kiongozi wa nchi wanahitaji zaidi ya pipi....tunatofautiana sana katika kufikiri. Wanaosupport eti kama mzazi well, mimi namwona Kikwete ni zaidi ya hapo kama head wa state.....anamajukumu mengi....sidhani kama Obama anaweza fanya hilo, ama Sarkozy na other serious leaders!

We are too cheap! Nilitegemea JF watu wanafikiria zaidi ya wale walevi wa kangala na wanzuki usukumani kumbe sivyo!

Are you serious kwamba viongozi uwatajao (serious leader by your definition) hawawezi kuwapa watoto pipi wakiwa kwenye ziara ya kuwatembelea wananchi? Naamini kweli tunatofautiana sana katika kufikiri!!! si mchezo.. ila tu kunakitu kinaitwa public relation.. maybe we have to think that way before we say G8 leaders can't do that
 
Back
Top Bottom