Rais kumzawadia mtoto pipi alikuwa na maana gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais kumzawadia mtoto pipi alikuwa na maana gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by munguatubariki, Aug 21, 2009.

 1. m

  munguatubariki Member

  #1
  Aug 21, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Kiukweli mimi binafsi, nimeshitushwa na nimeshangaa na kujiuliza maswali mengi mno baada ya kuona picha ya Rais akimzawadia mtoto Pipi. nimejiuliza maswali mengi kuwa kwa mfano huo anataka sisi tujifunze nini? au alikuwa na maana gani? na kwanini afanye hivyo.... na je alikuwa na uhakika kama huyo mtoto alikuwa amekwisha kula chakula ama anauhakika wa chakula baada ya hapo? Vp kuhusu afya yake namuona kama anamapunye kichwani kama nimeona vizuri, vp kuhusu uhakika wake wa elimu? mimi nahisi mtoto kama huyo anatakiwa kuzawadiwa uhakika wa elimu na sio pipi kama alivyo fanya rais. Na kwa mtizamo huu hivi kweli matabaka yatakwisha , hivi kweli jamani maisha bora kwa kila mtanzania yanaletwa kwa kugawa pipi?
   

  Attached Files:

 2. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Hayo maswali anatakiwa aulizwa mzazi na sio mpita njia. Mnazidisha sana hisia kiasi cha kupoteza rationally za kufikiri sasa.
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii unaenda mbali sasa. I think Mr president is Baba as well, akivua huo urais wake ataendelea kuwa baba. That is baba in him. Hata kama wewe ukikutana na mtoto mdogo mwenye umri kama huo njiani ukiwa na peremende unaweza kumpa. Au kwa mani yako ulitaka ampe nini? Penseli, Manoti, kitabu, soda? Kama angempa soda tungejifunza nini??
   
 4. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  My thing is rais anakaaje mbele kwenye gari hilo? Hiyo si security concern?
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Aug 21, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Na wewe bana.....nani anataka kumuua Kikwete?
   
 6. S

  Shamu JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo mtoto alitakiwa awepo darasani anasoma; na si kupokea pipi. Hiyo picha inaonesha INEQUALITIES ni tatizo linalokuwa kwa kasi sana ndani ya TZ. Rais yupo kwenye gari la kifahari + msafara wa wapambe; halafu huyo mtoto hata viatu hana. Sasa hivi kuna tofauti kubwa sana kati ya maskini (mlalahoi) na mtu wa middle class ndani ya TZ.
   
 7. m

  munguatubariki Member

  #7
  Aug 21, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu, nashukuru kwa kuona mtazamo wangu umekwenda mbali zaidi ya mtazamo wako.. ni sahihi kabisa kuangalia maswala kama haya kiundani zaidi kuliko kijuu juu.

  Ni kweli kiupande mwingine rais ni baba, lakini baba mzuri ni yule anaempa mtoto wake pipi? Au ni yule anaye zawadi ya penseli, kitabu kama ulivyosema? Hivi hiyo pipi itamsaidia nini huyo mtoto? angalau ingekuwa chungwa nisinge sema.

  Kumbukeni hizi staili za pipi ndo mwanzo wa mimba za umri mdogo kwa mabinti, kumbukeni tena sasa tunaelekea kwenye uchaguzi, sasa watoto tunawapa pipi, watu wazima kofia, khanga, na pilau.

  Halafu kumbukeni huyo ni rais kwanini atembee na pipi? Kwa hiyo anamakusudi yake! Pia kumbukeni hata ukoloni uliingia kwa staili ya kupewa pipi sasa wale walikuwa baba zetu?

  Fikiria kwa undani mzee huyo mtoto anahitaji msaada na sio pipi!
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu naona una philosophical view point ya hii picha. Ni kweli kuwa watoto wanahitaji mengi sana zaidi ya pipi. Lakini kitu cha haraka kabisa ambacho unaweza kumfurahisha mtoto mdogo unayekutana nae ni kumbeba, na kumpa zawadi ndogo ndogo. Lakini ni kweli isiwe ndio ikawa kama ile janja ya wakoloni, kulambisha watu asali na kuwasainisha mikataba.
   
 9. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  This is too low to be discussed! Mbona sioni ubaya wowote wa mzazi au mpita njia kumpa mtoto pipi? Jamani kumbukeni pipi zipo na watoto kupewa pipi sio kosa kisheria. Au unataka kuturudisha kile kipindi cha ujima. Ok, ondoeni pipi, muziki, soda, TV; kwa sababu watu wanahitaji kalamu, daftari, majembe, nk.

  Tunahitaji kuishi ndani ya jamii tuliyomo na sio kujifanya tupo kusikofikirika ili tuonekane tunajua kukata ishu hapa jamvini! arghhhh
   
 10. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2009
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kwa Rais wetu mambo ya kugawa pipi kwa watoto, kumwaga minoti mikoani (mabilioni ya Kikwete), kutoa pesa kwa disable (sometimes back around Samora or somewhere else in Dar) na mengineyo ndiyo style ya mkuu wetu. Kwa mtizamo wangu naona mambo kama haya hayasaidii kuondoa matatizo ya msingi yanayoikabili jamii bali ni njia ya kujipata umaarufu ama kulazimisha kupendwa.

  Kama Rais wa nchi ama baba wa familia unayejali unatakiwa kufikiria mbali zaidi ya kupita njiani na kuanza kugawa pipi and the like.
   
 11. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rais kama baba ana haki ya kufurahi na watoto, alichokuwa anataka kutuonyesha pale ni kuwa karibu na watoto wetu na kuonyehsa upendo wa dhati kwa familia zetu.

  Jukumu la elimu, afya, malazi na mavazi kwa mtoto ni la mzazi mwenyewe,je mzazi wa huyo mtoto alikwenda kwenye vituo vya afya hakakosa dawa ya mapunye?

  Rais na serikali yake wanajukumu la kuhakikisha mazingira bora kiuchumi,kisiasa na kijamii kwa wananchi wao. Mtoto wako anaumwa, haendi shule, hana pa kulala unataka rais aje achukue majukumu yako kaka baba wa familia.

  Watanzania tubadilike serikali na rais wake haiwezi kutufanyia kila kitu, sisi wenyewe ndiyo kiini cha maendeleo yetu binafsi.

  Nampongeza rais wetu Kikwete kwa kujitahidi kwa nia moja kutoonyesha binadamu hasa baba wa familia anatakiwa awe mfano wa upendo, amani na utulivu kwenye familia yake.
   
 12. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2009
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa hili nafikiri hana kosa...sasa kama hakukuwa na machungwa humo ndani ya gari angeyapata wapi ili ampe? Naamini hizo pipi walikuwa nazo na akaona angalau huyu bwana mdogo nae apate hapo.

  Huu ni ubinadamu. Na nafikiri ni bora zaidi kuliko kumpa pesa, kwa mtoto wa umri huu ukimpa pesa barabarani unamfundisha nini?

  Kesho akija kusimama kwenye makutano ya barabara utamlaumu...si umemuonyesha mradi wa kupata pesa? Tena mwalimu wake ni rais wa nchi...hapa Kikwete jamani hebu tumtafutie jingine si hili.
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,780
  Trophy Points: 280
  Mr.President hajakosea kitu pale...wewe unafikiri yule mtoto angepewa penseli au kalamu si angeipoteza tu lakini pipi ataila na ataiona tamu kishenzi..kwanza lile ni tukio la kihistoria kwake ..na suala la shule ni la mzazi wa yule mtoto la wala sio la Rais.
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa, mimi wala sihusiki... lol
  Lakini ni kweli sasa kufikiri kwetu kunazidi mipaka, tunasahau kuwa rais naye ni mtu kama mimi na wewe
   
 15. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  hahahaaa! kweli mjomba nani atamuua huyu!
   
 16. M

  Mwebrania Jimmy Member

  #16
  Aug 21, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza mzazi mwenye kumfundisha maadili mazuri mwanae ni kumzuia kupokea vijizawadi vidogo vidogo njiani kama pipi,jojo,soda chips, pesa nk. Sasa inakuwaje kwa kiongozi wa mkuu wa Taifa kuweka kipaumbele cha kutoa vizawadi kwa watoto tena njiani?

  Pamoja na hayo kiongozi badala ya kutembea na note book kwa ajili ya ku note vitu vya msingi for further action unatembea na mifuko ya peremende!!!
   
 17. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #17
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Wakoloni nao waliwahadaa mababu zetu perememende, shanga, sahani, vikombe, you name all in return they enjoyed fertile land, etc!!! Sasa kwa huyu presidaa wetu siju alijua mtoto ana njaa na anahitaji kula na akampa pipi kama chakula akitimiza ahadi yake kwa maisha bora kwa kila mtanzania!!! Kwa hiyo presidaa gari yake inakuwa na sweets??? Kazi nzito!!!
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Naona wadau mnasahau kuwa rais wetu ni mkwere..
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  Aug 21, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sioni ubaya wowote kumzawadia pipi huenda kwa wakti huo ndio kitu alichokuwa nacho na pengine ndicho yeye anachopenda kumung'unya awapo kwenye misafara ,wengine hupenda chewing gum.

  Aidha naweza kusema ni mwanzo wa Raisi kuweza kufikiria kutoa misaada mikubwa zaidi ya pipi ,pengine kwa kuwezesha kujengwa vituo vya kuburudisha watoto kwa kila mkoa na baadae kila wilaya ,vituo ambavyo kwa upande fulani vitawezesha wilaya na mikoa kupata mapato na pia kuweza kuajiri wafanyakazi katika kushughulikia na kuvitunza vituo hivyo.

  Kila siku za mapumziko na siku za sherehe za serikali au kidini vituo hivyo vitakuwa vikifunguliwa na kutozwa ada ndogo sana tuseme shilingi kumi tu hakuna haja ya kufanya tamaa na ndani ya kituo mtakuwa na vipando vya kitoto ambavyo navyo pia vitalipiwa ada hiyo hiyo ya shilingi kumi,sasa ikiwa kituo kitaingiza watoto 5000 kila jumamosi na jumapili utaona kitakusanya laki moja ,kila wiki hivyo kwa mwezi na mbali ya siku za sherehe na hicho ni kiingilio cha mlangoni mbali ya vipando ambavyo navyo vitahitajia shilingi kumi,na zaidi wazazi ambao watawapeleka watoto wao nao watalipa ,tunapenda kuona Tanzania inapiga hatua kila sehemu ,hongera Kikwete huo ni mwanzo mzuri ila fikiria mbele zaidi maana wewe ni mpanda madege na hivyo unaona huko nchi za wenzako. watoto watafurahi zaidi kuliko zawadi ya pipi wanahitaji zawadi za mawazo ili kuwaweka wenye furaha na nchi yao na kiongozi wao.
  Wamepita viongozi kibao sijawahi kuona kama hii ya Kikwete.
   
  Last edited: Aug 21, 2009
 20. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #20
  Aug 21, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Tusisahau Mzee Mwinyi alifanywaje! Binadamu wana mengi vichwani mwao.
   
Loading...