LazyDog
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 2,473
- 189
Kiukweli mimi binafsi, nimeshitushwa na nimeshangaa na kujiuliza maswali mengi mno baada ya kuona picha ya Rais akimzawadia mtoto Pipi. nimejiuliza maswali mengi kuwa kwa mfano huo anataka sisi tujifunze nini? au alikuwa na maana gani? na kwanini afanye hivyo.... na je alikuwa na uhakika kama huyo mtoto alikuwa amekwisha kula chakula ama anauhakika wa chakula baada ya hapo? Vp kuhusu afya yake namuona kama anamapunye kichwani kama nimeona vizuri, vp kuhusu uhakika wake wa elimu? mimi nahisi mtoto kama huyo anatakiwa kuzawadiwa uhakika wa elimu na sio pipi kama alivyo fanya rais. Na kwa mtizamo huu hivi kweli matabaka yatakwisha , hivi kweli jamani maisha bora kwa kila mtanzania yanaletwa kwa kugawa pipi?
Anagawa pipi ili apendwe.
Ni dhahiri hafikirii au kujiuliza maswali uliyoyaweka hapo juu. Yeye hayuko hivyo ambavyo ungemtegemea awe. This displays who he really is.