Rais kufia madarakani na kumpata Rais Mwanamke kwa mara ya kwanza, hii inaashiria nini?

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Salaam,

Ramadhan Maqbul.

Wanajamvi naomba kuongea haya na labda kuibua hoja. Kama nilivyoanza kwenye kichwa cha Habari hivi Katika historia ya nchi hii ni mara ya kwanza Rais anafariki akiwa Madarakani na Kwa Mara ya kwanza tunapata Rais ambaye ni Mwanamke; hii inaashiria nini?

Kwanza kwetu limekuwa jambo geni sana, ndiyo maana uliona kunakuwa na sintofahamu nyingi! Pia kuona tunafanya transition kwa amani haikutegemewa ndiyo maana wale walioishi kwa kumtegemea mtu na siyo uwezo wao kwa sasa wametahayuri.

Pia Makamu wa Rais kuwa Rais na kujiamini ni kukomaa kwa siasa ninaona mbeleni kuna mabadiliko mengi katika medani ya siasa.

Mwisho.

Naomba utupe mawazo yako hapa.

Kazi iendelee.
 
Mbona CCM kwenye kampeni walisema Lowassa ndiye mgonjwa hawezi kwenda ikulu kwakuwa ile siyo wodi kwamba angekufa si zaidi ya miezi mitatu sasa imekuwaje tena ikawa kinyume chake?
 
Ni ishara kwamba Mungu aliamua kuingilia kati ! vilio vilikuwa vingi kutoka kwa wadhulumiwa. Hakuna kitu kibaya kama dua ya aliedhulumiwa! Wengine wa dini nyengine huita karma!
Umesema kweli, na KIfupi inaashiria mwanzo wa demokrasia kamili, na kushindwa kwa udikiteta.
 
Inaashiria kuwa yule Mwendazake hakuwa kiongozi sahihi kwa nchi yetu na alipatikana kwa udhaifu wa Kikwette kutaka kumuengua Lowassa huku akimg'ang'ania Membe. Ile chuki, utekaji, uuaji, kudharau Katiba, kutofuata Utawala wa Sheria, kupendelea kwao na wizi siyo tabia ambayo ilikuwa imampendeza Mungu

Kuja kwa Samia ni dalili kuwa nchi yetu inapaswa kuendelea na misingi ya amani, upendo, mshikamano na umoja. Vilevile kudumisha Utawala wa Sheria. Mungu hataki turudie kukurupuka kuchagua kiongozi
 
Ni ishara kuwa ushindi ulikua ni wa Chadema 2020
CCM bado ina uwezo wa kushinda kihalali kabisa ila siyo kwa kimbunga kama hivyo.

Mgombea akiwa mpya na anaekubalika anaweza kupata mpaka 75+

Mgombea akiyevuruga sana, anaweza kushinda kwa 51+

Tatizo la CCM hawajiamini tu na wamekuwa na uwoga sana wa kupoteza kiasi kwamba wamekuwa WAPORAJI wa kura.

CCM bado ina machinery kubwa ya ushindi: Wanawake, wazee, wahanga wa propaganda.

Vyama vya upinzani vinakubalika mostly kwa vijana tu ambao nao wengi ni mashabiki tu bendera fuata upepo kwasababu ya NJAA. Wanakata tamaa kirahisi
 
Back
Top Bottom