Kidudu Mtu
Member
- Nov 7, 2009
- 64
- 0
MBUNGE wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe amesema Rais Jakaya Kikwete ndiye anayefaa kuongoza nchi na ni mhimili mkubwa katika vita ya ufisadi ila baadhi ya wasaidizi wake wanamrudisha nyuma katika vita hiyo.
Alisema hayo jana katika kongamano la miaka 10 Bila ya Baba wa Taifa lililoandaliwa na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini na kufanyika katika Chuo cha Ustawi Jamii (ISW).
Mwakyembe alikuwa akijibu swali la mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anayesoma shahada ya elimu, Chagona Deogratias aliyetaka kufahamu iwapo hoja alizokuwa akitoa Dk. Mwakyembe katika kongamano hilo alikuwa akiogopa kumsema Rais.
Mimi kwangu namuona Rais anafaa kuongoza bali tunapaswa tumuondolee baadhi ya watu wanaomchafua, alisema Dk. Mwakyembe huku akiwataka watu wasimfikirie vibaya anapotoa hoja zake kuwa ni mbwembe bali anajiamini kutokana na elimu aliyonayo na hivyo anajivuna.
Alisema kuwa wananchi kwa ujumla wanapaswa kumsaidia Rais Kikwete katika mapambano ya ufisadi na vitendo vingine viovu katika jamii ili nchi ipige hatua za maendeleo.
Akizungumzia suala la mikataba mibovu, Mwakyembe alidai imekuwa ikisababishwa na ushamba wa wataalamu wetu katika masuala ya mikataba hali ambayo inaigharimu nchi na kuchangia kurudi nyuma kimaendeleo.
Kwa upande wake kada wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) aliyeshiriki katika mkutano huo Nape Nnauye, alisema kuwa kelele za ufisadi zinazopigwa nchini na baadhi ya watu hazimaanishi kwamba nchi nzima imeoza, bali kuna baadhi ya matatizo yanayotakiwa kushughulikiwa ili yasizidi na kuenea na hatimaye kuidhoofisha nchi.
Alisisitiza umuhimu wa kukomesha rushwa wakati wa kugombea nafasi katika uchaguzi mbalimbali la sivyo taratibu za uchaguzi zitaendelea kuharibika na kuwaasa wenye tabia hizo waache.
Mbunge wa Kishapu kupitia CCM Fred Mpendazoe, alisema kuwa umasikini unasababishwa na uongozi mbovu na kushauri miiko ya uongozi ipewe kipaumbele.
Katika hatua nyingine alisisitiza umuhimu wa kuongezeka kwa viwanda vingi vya usindikaji wa vyakula na matunda kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ili falsafa ya Kilimo Kwanza itekelezwe kwa vitendo.
...................................
Is Mwakyembe serious?