Rais Kikwete ndani ya Karatu, akielekea Monduli

ANKOJEI

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
996
742
HABARI ZA SASA IVI KABISA

Mheshimiwa raisi wa Jamuhuri wa Mungano wa Tanganyika na Zanzibar -JK.....Yupo Karatu saa hii anaelekea monduli kutoa ng'ombe kwa wamasai wale waliokufa kwa ajili ya ukame mwake ule wa kampeni. watu wengi balaa nimeshindwa kupiga picha.

source mimi mwenyewe niko eneo la tukio.

Na Eliya Mbonea, Arusha


FAMILIA zaidi ya 125 wilayani Monduli na Ngorongoro mkoani Arusha zinatarajiwa kupokea msaada wa ngo'mbe 500, baada ya kukumbwa na ukame uliokumba maeneo ya malisho ya familia hizo mwaka 2009.



Ahadi hiyo iliyoanza kutekelezwa tangu Februari, 2012 na Rais Jakaya Kikwete katika wilaya ya Longido, sasa inaelekezwa katika wilaya hiyo na Rais Kikwete ndiye anatarajiwa kuwakabidhi wafugaji hao.


Tukio hilo ambalo huvuta hisia za wafugaji wengi linatarajiwa kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa maeneo hayo, akiwamo Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa na Saning"o ole Telele wa Ngorongoro.


Akizungumzia sherehe hizo zinazotarajiwa kuanzia leo wilayani Monduli, Mkuu wa wilaya hiyo, Jowika Kasunga, alisema wafugaji watakaonufaika na msaada huo ni wale waliopoteza ng'ombe wao wakati wa ukame mkali ulioyakumba maeneo ya wafugaji hao katika mwaka 2009 na kusababisha maelfu ya mifugo ikiwamo ng'ombe na mbuzi kufa kwa kukosa malisho na maji.


"Ugawaji huo wa mifugo hii ni muendelezo wa mradi wa ugawaji wa mifugo kwenye wilaya tatu za Monduli, Ngorongoro na Longido. Kama utakumbuka tayari Wilaya ya Ngorongoro ilishakabidhiwa mifugo 11,000 ya wananchi wake Februari mwaka huu," alisema Kasunga.


Alisema Rais Kikwete atagawa mifugo 500 kwa familia 125 za wilayani humo, ambapo kila familia inayohusika inatarajiwa kufaidika na mifugo minne. Baadaye ugawaji wa ng'ombe na mbuzi wengine wapatao 6,000 kwa familia 1,400 utaendelea wilayani Monduli.


Akizungumzia kuhusu ugawaji wa mifugo hiyo katika Wilaya ya Ngorongoro, alisema mpango huo utafanyika katika Kata ya Loliondo ambako jumla ya mifugo
7,400 itagawanywa kwa familia 1,850.


Katika ukame huo uliotokea mwaka 2009 takriban mifugo 700,000 ilikufa kwa njaa, kutokana na kukosa malisho na maji ya kunywa.


Kuendelezwa kwa ahadi hiyo sasa kunafanya ahadi hiyo kufikia kiasi cha Sh bilioni 11.2 kwa wilaya tatu ambazo ni Ngorongoro, Longido na Monduli.

Chanzo: Mtanzania
 
Ameshukia kiwanja cha mbugani pale manyara nini??kazi ipo mwaka huu mkumbusheni kuwa hajalipa mishahara bado.....
 
Muulize vip hana mpango wa kuwafukuza walimu wote kama alivyofanya kwa mdr
 
Mwambie hasisahau kufika na kwenye olympics ila aangalie mavazi ya wanamichezo yasije yakaharibu saum!
 
Yaani yupo Karatu njiani kuelekea Monduli? Sasa katua kale kauwanja kadogo badala ya Arusha Airport? Kweli uwoga kitu kibaya sana
 
Hivi wale wafugaji wa kiti moto kule mbeya ambao mifugo yao ilipuputika kwa ugonjwa nao walipewa fidia?
 
yap yap kilichonishangaza ni nyomi ya umma, na wanamsubiri akiruka tena kuelekea loliondoi
 
mbona sijaona msafara wake bado mimi niko hapa barabarani kumpa hai nimesubiri weee hola eti kapitia wapi mheshimiwa
 
Back
Top Bottom