Rais Kikwete ndani ya Karatu, akielekea Monduli

Hongera sana JK kwa kutimiza ahadi.

Kugawa ng'ombe ilikuwa ahadi? hizi akili zilizoshikwa na Nape zina matatizo sana, kila wanasifia ili mradi mvute posho pale Lumumba kwa kumfurahisha Nape kuwa mmepost JF
 
Na Ulimboka atafidiwa nini na uharibifu wenu serikali mlioufanya kwake? Mwaka huu Mbeye ni bora msahau kabisa kura. Wageni wa Mby labda ndo watawapa.
 
Na ahadi za "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana" "Tutaipitia tena mikataba ya madini ili iwe na maslahi kwa Tanzania na Watanzania" "Tutaigeuza Kigoma ili iwe Dubai ya Afrika." n.k. zitatimizwa lini?

Watu wanatimiza ahadi sio kununua kula...
 
Huyo ndio Baba Mwanaasha bwana..kazi yakumsafisha mzee Mamvi imeanza,ni mpango mkakati wa siku nyingi sana huu.
 
Roho mbaayaaaa, kama unahasira kalia chupa ya fanta kama ulimboka.
We nafikiri umeisha ikalia chupa ya JACKDANIEL siku nyingi ndo maana hata hiyo ID yako ni Ecoli ikimaanisha unaharisha damu tayari
 
Ikumbukwe kwa kadri ya miezi kadhaa mfululizo, hata juzi rais JK amekwenda monduli kugawa ngombe kwa jamii ya wamasai ambao mifugo yao ilikufa kwa ajili ya ukame.Wakati ule wa ukame jamii kubwa ya wamasai ilikuwa inaishi na kufanya shughuli zao karibu na kitalu cha ortelo ltd cha mfalme wa UAE ambacho serikali imemuuzia kuwinda na kuhamisha twiga kupeleka arabuni.Kwa miaka mingi wamasai hao walikuwa wakiendesha shughuli za ufugaji karibu au ndani ya kitalu hicho bila matatizo.wakati wa ukame mwarabu aliamrisha serikali kwa kutumia polisi na uongozi wa mkoa wa arusha kuwaondoa wamasai hao kwenye kitalu hicho.Kwa kipindi hicho polisi pamoja na ffu walichoma maboma, wanawake walibakwa, chakula kiliungua, na mifugo iliondoshwa kwenda kwenye sehemu ya ukame.Wanaharakati wengi walilaani kitendo hicho ambacho kilipelekea serikali na kamati ya bunge enzi za waziri shamsa mwagunga kuwa , hao walioondolewa na kuchomewa maboma walikuwa wakenya.watu na wadau wengi walipinga mpaka akina mama wakimasai wakafunga safari kuja ikulu kulaani na kupinga kuwa wao si wakenya ila walichomewa maboma yao na pia kubakwa kimakosa na askari hao wakati wakiwahamisha kutoka kitalu cha mwarabu.Iweje leo JK akatoe ng'ombe kwa jamii hiyo hiyo ambayo ni wakenya kama kauli ya waziri wake haijapingwa? kama kweli kauli hiyo haikuwa sahihi, bac hata hiyo operesheni haikuwa sahihi.hivyo kugawa n'gombe ni kama rushwa kupoza uovu wa operesheni hiyo.
 
Back
Top Bottom