Rais Kikwete ndani ya Karatu, akielekea Monduli

hivi wamasai pekee yao ndo walikuwa wahanga wa ukame? Vp kuhusu wakulima? Au kuna mkakati wa kuwafidia wakulima walioadhirika?
 
Kama kawaida yake JK hukimbilia kufanya mambo mepesi na huku mambo magumu na nyeti akiyakimbiza mahakamani. Leo JK alikuwa Makuyuni mjini Arusha akigawa ng'ombe kwa wamasai kazi ambayo angeweza kufanya hata mkuu wa Wilaya.

Ninapata maswali mengi kuhusu unyeti wa hiyo shughuli kufanywa na kiongozi mkubwa wa nchi kama rais huku akishindwa kutatua mgomo ambao umewaacha waalimu wakilia kwa kupuuzwa huku akijua hukumu ya kibabe itakayotolewa na mahakama kuu kitengo cha kazi.

Safari ya kugawa ngombe imeanzia Dar ambapo ndege ya rais na wasaidizi wake ilipaa kwa gharama kubwa za walipa kodi kuja Arusha kugawa ngo'mbe!!!!

Mimi nafikiri kuna mambo mengi muhimu sana ya vipaumbele ambayo rais anapaswa kuyashughulikia lakini cha kushangaza anatumia muda wake muhimu sana kuja kuvaa mgorori kugawa ngombe

HV dume la ngombe lingefwatuka likavunja jukwaa na kumwangusha rais bodyguard wako equiped kiasi gani kuzuia asidhurike?.

Mi nafikiri rais ajaribu kupriotize shughuli zake na shughuli nyepesi kama hizi aachie wengine kwani kwa maoni yangu zinamshushia hadhi
 
Ukienda Monduli huwezi kamwe kupita Karatu

Mkuu hata mimi hii ramani imenichanganya ile mbaya!

Yaani Unaenda Monduli unapitia kwanza Karatu? Au kaja na vile vindege vidogo na kutua uwanja wa pale Ngorongoro njia panda ya Serengeti/Endureni? Kwa kweli shule zetu za Kata hazitusaidii, maana hiyo ramani ya huyu zoba hailipi hata kidogo.
 
[h=3][/h]Na Eliya Mbonea, Arusha


FAMILIA zaidi ya 125 wilayani Monduli na Ngorongoro mkoani Arusha zinatarajiwa kupokea msaada wa ngo’mbe 500, baada ya kukumbwa na ukame uliokumba maeneo ya malisho ya familia hizo mwaka 2009.



Ahadi hiyo iliyoanza kutekelezwa tangu Februari, 2012 na Rais Jakaya Kikwete katika wilaya ya Longido, sasa inaelekezwa katika wilaya hiyo na Rais Kikwete ndiye anatarajiwa kuwakabidhi wafugaji hao.


Tukio hilo ambalo huvuta hisia za wafugaji wengi linatarajiwa kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa maeneo hayo, akiwamo Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa na Saning”o ole Telele wa Ngorongoro.


Akizungumzia sherehe hizo zinazotarajiwa kuanzia leo wilayani Monduli, Mkuu wa wilaya hiyo, Jowika Kasunga, alisema wafugaji watakaonufaika na msaada huo ni wale waliopoteza ng’ombe wao wakati wa ukame mkali ulioyakumba maeneo ya wafugaji hao katika mwaka 2009 na kusababisha maelfu ya mifugo ikiwamo ng’ombe na mbuzi kufa kwa kukosa malisho na maji.


“Ugawaji huo wa mifugo hii ni muendelezo wa mradi wa ugawaji wa mifugo kwenye wilaya tatu za Monduli, Ngorongoro na Longido. Kama utakumbuka tayari Wilaya ya Ngorongoro ilishakabidhiwa mifugo 11,000 ya wananchi wake Februari mwaka huu,” alisema Kasunga.


Alisema Rais Kikwete atagawa mifugo 500 kwa familia 125 za wilayani humo, ambapo kila familia inayohusika inatarajiwa kufaidika na mifugo minne. Baadaye ugawaji wa ng’ombe na mbuzi wengine wapatao 6,000 kwa familia 1,400 utaendelea wilayani Monduli.


Akizungumzia kuhusu ugawaji wa mifugo hiyo katika Wilaya ya Ngorongoro, alisema mpango huo utafanyika katika Kata ya Loliondo ambako jumla ya mifugo
7,400 itagawanywa kwa familia 1,850.


Katika ukame huo uliotokea mwaka 2009 takriban mifugo 700,000 ilikufa kwa njaa, kutokana na kukosa malisho na maji ya kunywa.


Kuendelezwa kwa ahadi hiyo sasa kunafanya ahadi hiyo kufikia kiasi cha Sh bilioni 11.2 kwa wilaya tatu ambazo ni Ngorongoro, Longido na Monduli.

Chanzo: Mtanzania
 
Yeah, Kweli hawa Viongozi walipatana Wakiwa LONDON...

Sasa Wanafanya Harambee Pamoja??

2015 Njia Nyeupe kwa Lowassa kugombea Urais...
 
HABARI ZA SASA IVI KABISA

Mheshimiwa raisi wa Jamuhuri wa Mungano wa Tanganyika na Zanzibar -JK.....Yupo Karatu saa hii anaelekea monduli kutoa ng'ombe kwa wamasai wale waliokufa kwa ajili ya ukame mwake ule wa kampeni. watu wengi balaa nimeshindwa kupiga picha.

source mimi mwenyewe niko eneo la tukio.

32.jpg


WABABE ...
 
37.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigawa Ng'ombe kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
 
38.jpg

Wananchi wa Kijiji cha Makuyuni wakifatilia zoezi la ugawaji wa Ng'ombe.
 
Dah!!! Siku hizi kununua KULA shurti kwa ng'ombe!!!! Kazi ipo 2015.
 
Dhaifu sasa anawasafisha mafisadi wote. Yaani anapruvu Mnyika was right. Alianza na Chenge, sasa huyu na whos next ?
 
Huu mgawo ndio utakaoiangusha ccm 2015. as we all know ng'ombe watagawanywa kwa upendeleo
 
Back
Top Bottom