Rais Kikwete na mazungumzo na ujumbe wa CHADEMA

Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,503
1,722
Wakuu JK amekubaliana na ujumbe wa CHADEMA kukutana tena kesho asubuhi ili kumpa nafasi kutafakari yale waliyo yazungumza leo. Tutarajie nini watanzania?

UNITED REPUBLIC OF TANZANIADIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

PRESIDENT'S OFFICE,
THE STATE HOUSE,

P.O. BOX 9120,

DAR ES SALAAM
.
Tanzania
.
Telephone: 255-22-2114512, 2116539

E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wa Serikali yake leo, Jumapili, Novemba 27, 2011, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, yamefanyika katika mazingira ya urafiki na ujumbe wa CHADEMA umewasilisha mapendekezo yake kuhusu mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya Tanzania. Serikali imepokea mapendekezo hayo.
Hata hivyo, pande zote mbili zimekubaliana kukutana tena asubuhi ya kesho, Jumatatu, Novemba 28, 2011, ili kuipa nafasi Serikali iweze kutafakari mapendekezo hayo.

Lakini pande hizo mbili zimekubaliana kuwa Katiba ya sasa ni Katiba nzuri iliyolilea Taifa kwa miaka 50 iliyopita kwa sababu ni Katiba ya sasa iliyoliwezesha Taifa la Tanzania kuwa na amani, utulivu na kupata maendeleo makubwa ambayo nchi yetu imepata mpaka sasa.

Pia pande zote mbili zimekubaliana kuhusu umuhimu wa kutunga Katiba Mpya kama Mheshimiwa Rais Kikwete alivyoliahidi taifa wakati wa salamu zake za mwaka mpya Desemba 31, mwaka jana, 2010, Katiba ambayo italiongoza Taifa la Tanzania kwa miaka mingine 50 ijayo.

Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Rais aliwahakikishia wajumbe hao wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Mheshimiwa Freeman Mbowe kuwa ni dhamira yake na ya Serikali yake kuhakikisha kuwa Tanzania inapata Katiba mpya.

Katika mkutano huo, pande zote mbili zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu sana kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba Mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa.

Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa mchakato huo uendeshwe kwa kuzingatia misingi ya mambo mengine muhimu kwa taifa la Tanzania kama vile kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, kuligawa Taifa kwa misingi ya udini na ukabila ama kutugawa kwa misingi ya maeneo.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,
DAR ES SALAAM.
27 Novemba, 2011
 
Wakuu Source ni taarifa ya habari TBC1 inayo endelea sasa hivi
 
Hii ni muhimu sana, anatafakari walichopendekeza ili naye ashauriane na timu yake, kesho asubuhi awape Chadema maamuzi yake!.
 
Wakuu jk amekubaliana na ujumbe wa chadema kukutana tena kesho asubuhi ili kumpa nafasi kutafakari yale waliyo yazungumza leo.Tutarajie nini watanzania?Nawasilisha.

Hapo Mkuu wa kaya anaenda kutafuta ushauri kwa akina kingunge! Ngoja tusubiri atakuja na nini kesho!
 
Haya, wameshika mpini lazima tukubali kwa sasa, katiba tuliyonayo na nzuri sana tena mno, hata kama ni ya hovyo.
 
Nimefurahi sana kuona hii movement.CCM na CDM vinaunganika pamoja kuitengeneza tanzania tuitakayo. Mwanzoni hili waliliweza CUF na sasa naona CDM wameingia. Kwa mantiki hii upinzani Tanzania sasa basi.
 
CHADEMA kaibuka kidedea dhidi ya NEC ya CCM!! Wamefanya mkutano na Rais kama walivoomba na kukubaliwa!! Kwa upande mwingine JK kaonesha heshima kwa Taasisi ya Urais kwa kukataa ushauri wa NEC ya CCM wa kukutana na vyama vingine vya siasa. Nisichokielewa ni kumwona Dr. Nchimbi, wakati ni waziri katika serikali kupitia Vijana na Michezo. Nilitegemea serikali iwakilishwe na Wizara ya Katiba na Sheria, Attorney General na hata Chief Justice. Pingamizi la CHADEMA ni la kisheria, si la kimtazamo!!

Tuendelee kusikiliza lakini tayari political scoreboard inaonesha CHADEMA wako juu.
 
Hizo ni pumba za vitengo vya habari vya habari vya serikali. Si ajabu ilitayarishwa toka jana; tusubiri hiyo kesho
 
Hizo ni pumba za vitengo vya habari vya serikali. Si ajabu ilitayarishwa toka jana; tusubiri hiyo kesho
 
Lakini pande hizo mbili zimekubaliana kuwa Katiba ya sasa ni Katiba nzuri iliyolilea Taifa kwa miaka 50 iliyopita kwa sababu ni Katiba ya sasa iliyoliwezesha Taifa la Tanzania kuwa na amani, utulivu na kupata maendeleo makubwa ambayo nchi yetu imepata mpaka sasa.
Wameanza kutunga makubaliano sioni mbele kuna nini. Siamini Ujumbe wa CDM unaweza kukubali uzuri wa katiba hii ya mkoloni.
 
Hawa viongozi wa CHADEMA wamenihuzunisha sana leo. Yaani wanapiga picha na Rais wasiyemtambua huku wanacheeeeeeka meno yote 32 nje. Hapo unategemea nini zaidi ya kushuhudia ndoa nyingine ya mke wa pili wa CCM mwaka 2015. Kweli siasa za Tz ni vichekesho tupu.
 
Hata mkifanya maombi na kwa wale wanaofanya matambiko mtachoka na mnachosha akili zenu mnaoota eti CDM watafunga ndoa na CCM akili zenu zimekaa kushoto kushoto sana tulichotakiwa kukiona ni kujulishana au kuulizana ni kitu gani kimejadiliwa sasa watu kama Rejao unakuja na ndoto za alinacha,hivi ni unadhani CDM ina-mind ubwabwa
 
Back
Top Bottom