Rais Kikwete kuzungumza na wazee wa CCM Dar leo jioni!

Status
Not open for further replies.
natabiri ajenda muhimu itakuwa ni mgomo wa madaktari na hasa kujaribu kuwakalipia kama ilivyokuwa kwa wafanyakazi wakati uleeeee.. tuvute subira!! lakini hili la madaktari halikwepeki. na nionavyo mazungumzo kwa kutumia wazee wa dar ni ishara tosha kuwa hayupo katika kutafuta suluhisho na madaktari (kwa kutekeleza yale yatakwayo na ma Dr), maana kama angetaka suluhisho tungesikia anakutana na madaktari si wazee.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Huyu mtu aliingia madarakani kwa nguvu za vijana, au watu wanasahau? Wanasahau vijana walivyokuwa wakilala barabarani aliporejea toka Dom mwaka 2005 baada ya kuteuliwa kugombea?

Sasa anawatupa vijana, hataki kabisa kuwaona. Anaona wazee ndiyo bora! Kwa nini asiwaite vijana kuongea nao? huyu mjamaa ni wa ajabu kwelikweli.
 
hahahahhahaa anaenda kutangaza kwamba madaktari kutoka cuba na china wanafika kesho! Serikali hii bana inawafanyia wananchi wake checks n balance za matatizo
 
Kesho ni siku ya hotuba kama ile ya mbayuwayu!. Madokta ambao hawatarejea kazini baada ya hotuba ya kesho, chamoto watakiona!. Yaani watakiona kisa cha mtema kuni, kilichomnyoa kanga manyoya!.

Naisubiri kesho kwa hamu kumsikiliza rais wetu JK ambae ili nijue nitaongeza post kwenye thread ya mazuri yake au mabaya yake!.
Sawa mkuu Pasco,, so wazee wa ccm dar ndo audience yake!
 
Angalizo kwa madaktari: jk kashindwa kutafuta audience na madaktari....atataka kupata on paper support ya wazee wa dar(kama kawaida yake)....ikumbukwe kuwa ni katika vikao kama hivi jk alitukana wafanyakazi nchi nzima kabla ya uchaguzi wa 2010 (baadae alijutia maneno yake wakati anatafuta kura)....tujiandae kwa nonsense hiyo kesho........
 
Sina tu pesa za kuwalipa hawa madactari kwa kuwaonyesha njia watanzania walimu mpo wapi wakati wa mitihani ndo wenu nchi hii yetu hakuna wa kumuogopa.

Huyu Kikwete na akina mponda wake sijui ataongea nini na wazee wa ccm wafu.
 
kuna kitu sijaelewa nadhani...
je,ni mwenyekiti wa CCM anakutana na wazee wa CCM? au ni Rais wa JMT anakutana na wazee wa CCM?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Songíto;3459002 said:
natabiri ajenda muhimu itakuwa ni mgomo wa madaktari na hasa kujaribu kuwakalipia kama ilivyokuwa kwa wafanyakazi wakati uleeeee.. tuvute subira!! lakini hili la madaktari halikwepeki. na nionavyo mazungumzo kwa kutumia wazee wa dar ni ishara tosha kuwa hayupo katika kutafuta suluhisho na madaktari (kwa kutekeleza yale yatakwayo na ma Dr), maana kama angetaka suluhisho tungesikia anakutana na madaktari si wazee.

Uko sahihi Mkuu, lets wait and see but thats quite obvious
 
Songíto;3459002 said:
natabiri ajenda muhimu itakuwa ni mgomo wa madaktari na hasa kujaribu kuwakalipia kama ilivyokuwa kwa wafanyakazi wakati uleeeee.. tuvute subira!! lakini hili la madaktari halikwepeki. na nionavyo mazungumzo kwa kutumia wazee wa dar ni ishara tosha kuwa hayupo katika kutafuta suluhisho na madaktari (kwa kutekeleza yale yatakwayo na ma Dr), maana kama angetaka suluhisho tungesikia anakutana na madaktari si wazee.

Yaani wewe unaona manyunyu yameanza na wingu zito halafu unasema unatabiri mvua itanyesha!!!!
 
Wazee wa Dar es salaam au wazee wa c.c.m?na kuna tija gani ya kuongea na taifa kupitia hao wazee wa c.c.m?taifa lipo ktk hali tete ya madaktari,watu wanakufa,zinaletwa propaganda za kuongea na taifa kupitia wazee wa d.s.m,ongea na taifa kutokea ikulu,hatuhitaji kuona hao wazee wakipga makofi kwenye tv,tunahitaji kuona mmefikia muafaka na ma daktari na roho za watanzani haziendelei kupotea
 
Hivi hao wazee ndo wanaongoza nchi? Mana kila kitu kikimuwia vigumu anakimbilia kwa hao wazee.
 
Yaani wewe unaona manyunyu yameanza na wingu zito halafu unasema unatabiri mvua itanyesha!!!!
Mkuu hebu niweke sawa, labda sielewi maana ya neno kutabiri!! kwa fikra zangu ni kubashiri jambo ambalo halijatokea bado... kumbuka mkulu anaweza kuzungumza mengi na inawezekana pia asigusie hilo la madaktari maana hatujui anawaza nn, ila kiupande wangu naona hilo ndo kubwa zaidi kwa wkati huu.
 
Wale wazee ningekuwa daktari siwahudumii wanaenda kujaza ukumbi na wanasinzia wanaashwa pale makofi yanapopigwa nao wanajikuta wanapiga makofi bila kujua wanapigia nn.

Kuna haja ya kuwakusanya wote na kuwatupa mto ruvu

Duh!Kuwatupa mto Ruvu?...Hapana punguza hasira mkuu.
 
Inawezekana akatangaza upya nafasi za udaktari! Hata hivyo niseme kama rais atazungumzia mgogoro wa madaktari kabla ya yeye rais kuongea na madaktari basi litakuwa jambo la kusikitisha sana. Na kwa nini rais anatumia huu mtindo wa zama za ujima wa kuongea kupitia wazee? Hana idea yake mwenyewe ya uongozi badala ya hii tabia ya copy & paste? Waliogoma ni madaktari, wazee wa nini?
 
Kesho ni siku ya hotuba kama ile ya mbayuwayu!. Madokta ambao hawatarejea kazini baada ya hotuba ya kesho, chamoto watakiona!. Yaani watakiona kisa cha mtema kuni, kilichomnyoa kanga manyoya!.

Naisubiri kesho kwa hamu kumsikiliza rais wetu JK ambae ili nijue nitaongeza post kwenye thread ya mazuri yake au mabaya yake!.

Si tayari unajua kha!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom