Umeongea kwa uchungu mkubwa , kwa kweli kubeba passport ya Tanzania ni matatizo kwa wengi wetu, na yamenikuta mara nyingi sana nikiwa safarini nje ya nchi. nchi nyingi wanafahamu wabeba unga ni watanzania , airports ukikaa na wasafiri wenzako wakajua wewe ni mtanzania wanakuwa na wasi wasi .
Mwaka jana nilisachiwa zaidi ya mara tatu or tambo airport , iliposhindikana nikapitishwa kwenye njia ya x ray . Nilifikiri racism at work, nikamuuliza security agent mmoja, kwa nini ilikuwa so harsh kwangu wakati wengine hawakupitia niliyopitia ,Jibu alilonipa macho makavu kabisa , kuwa Watanzania wanakakamatwa sana hapo na unga, na process ya kuingia kwenye x ray ina madhara makubwa , hivyo kwa vile sijakutwa na hatia naweza kudai fidia . Wako katika kuprotect national intrest by any means. Nilijawa na hasira na uchungu kwa pamoja baada ya jibu hilo ,nikajionea it was cheap for me kuendelea na shughuli zangu , kuliko kuhangaika na kesi za complaints.