Rais Kikwete: Kuwa Makini Hii Issue Itakuangusha

Rais Kikwete: Kuwa Makini Hii Issue Itakuangusha

Raisi wa tanzania jakaya kikwete, ndege yake ndo inatumika kusafirisha madawa ya kulevya sehemu mbali mbali dunian, kupitia ziara zake. Unaambiwa mafisadi/dealers wameiteka bandari na mamia ya makontena ya dawa za kulevya hupitisha bandarini bila shida, mafisadi hao pia wameiteka airport, tra, police, mahakama, usalama. Wanamtumia raisi kama punda. Haiwezekani kuwaondoa hawa mafisadi sababu dawa za kulevya= CCM. Kwa taarifa tu tanzania ni nchi ya 4 yenye hazina kubwa ya madawa ya kulevya nyuma ya pakistani, mexico, india, then tanzania
 
nilipoingia Sweden mara ya kwanza 2007 airport zote i.e Doha na Arlanda haikuchukua dk 15 kukaguliwa na kuruhusiwa. this time Doha 45 minutes Arlanda almost one hour ndo niruhusiwe kukanyaga Sweden. jamani?
 
Tanzania bila madawa ya kulevya aiwezekaniki. chukua tahadhari.
 
kama serikali inajua uncle Deo kuwa mbowe na Bavicha wanadeal hizo, kwa nini Haiwakamati? Kama si biashara ya Ccm zaidi? cCM hoyee! idd Azan hoyee!
 
Tulikofikia, Ni vyema kama nimekalia tawi na nashindwa kulikata mwenyewe basi ni kuwaruhusu wenzangu walikate tawi hilo. Uhai binafsi kama bado ulikuwepo utaendelea kuwepo tu.

Mkuu anayeweza kufanya kama unavyoshauri lazima awe mzalendo kweli kweli.

Wangekwepo watu wa namna hiyo nchi yetu haingefika hapa ilipofika!
 
Anafikiri itaishia kwetu. Itaambata hadi kwa vitukuu vyake. Haya machozi ya Watanzania hayataenda bure!!
 
Ni muda muafaka kwa JK kujitengenezea ujiko akistaafu
 
Mkuu anayeweza kufanya kama unavyoshauri lazima awe mzalendo kweli kweli.

Wangekwepo watu wa namna hiyo nchi yetu haingefika hapa ilipofika!

Hebu tuwatafute hao wazalendo wachache waliobaki. Hata yule rais wa Njuwan alijiona yeye ni mazalendo lakini mataifa mengine ikiwemo TZ ikiongozwa na Rais wetu alisaidia kumtoa madarakani. (Yeye alijiona mzalendo lakini wengine wakaona tofauti ndio maana akang'olewa)
 
Yaaap tutakuwa Kama Colombia na Mexico muda si mrefu .
 
moja kati ya maombi yangu kwa Mungu ni kuifanya tanzania isiwe na viongozi wezi, wala rushwa na wasiojali masrahi ya wananchi hatimae naelekea kufanikiwa.
 
Je ni yupi kati yenu awezaye kukata tawi alilokalia yeye mwenyewe?
Umesomeka mkuu au nani kati yenu awezae kujing'oa kucha na meno kama walivyofanywa akina Kibanda na Ulimboka???sio rahisi unapozungumzia wauza madawa ya kulevya hapo unagusa mfumo mzima wa uongozi wa nchi yetu JK huwezi kumtenga na hilo.
 
Maendeleo hayatakuwa na maana iwapo nguvu kazi kubwa inatumika na kumalizwa na dawa za kulevya.

Wakati ni huu kwa watawala japo kuhurumia nguvu kazi ya taifa inayopotea kila siku na dawa la kulevya.

Kama majina na ushahidi upo kitu gani kinashindikana kuwatia mbaroni watuhumiwa hao.

Ni wazi kabisa kama suala halitashughulikiwa tutakuwa tunatengeneza taifa legevu lisilo na staa na mwisho

wa siku tutajikuta tunaishi naa mazombi badala ya watu waliostaharabika.

Wakuu japo tupieni jicho la huruma kwa maskini hao wanazidi kunyong'onyea kila siku.
 
Tatizo ukilichekea wakati ndio liaanza mwishowe linakuua, kimsingi tumeshachelewa, Akina nzowa wanahangaiika geresha tu maana wanajua kuwa maDealer wa izo ishu ni mabosi zao, ila hawana cha kufanya.
Si unajua njaa? Wako ajirani wafanyeje? Hawawezi kuwakamata mabosi zao! Kashindwa KAKA MKUU mjengoni!!
 
Ashughulikie nini mkuu wakati hela chafu ndo inazungushwa kwenye kampeni kununulia wakina mama khanga, ubwabwa, kuwapa nauli na posho za kujaza viwanja vya kampeni!
Fatilia mambo mengine mkuu lakini siyo kumpa ushauri mtu ambaye hawezi kuufanyia kazi ingawa ana uwezo mkubwa kimadaraka.
Ngumu sana. Unajua ushauri kiasi gani mpaka sasa ushafanyiwa kazi? Maprofesa washakaa wakaandika pepa juu ya kilimo kwanza na jinsi gani inaweza kumtoa mkulima toka kwenye hali ya sasa mbaya na wamelipwa hela yao ya feasibility study. What happened?
Basi bhana ngoja niache tu.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
WW umenichekesha sana, inasikitisha sana kama ndo hivyo, Mungu awarehemu, hawajui walitendalo!


Unafikiri kwanini CCM wameijia juu Red Guards....wanajuwa kuwa Green Guards wake wamepata wapinzani hivyo kunyanyasa watu kutapungua na ni kitu ambacho CCM hawataki, wao upinzani kwao ni ugaidi. Washenzi sana, yaani wanaendesha inchi kama nyumba yao.
 
mkuu ushawahi kuingia anga zao nini?mbona uko deep sana?au green guard?


Hapana ila yaliyomkuta ndugu yangu Mwangosi yamenipa kero sana na hawa watu. Don't listen to the hype, yale yaliyomsibu ndugu yangu Mwangosi yanahusishwa na hawa inzi vijana.
 

Tanzania imebadilika. Kila watanzania wamechafuka kimataifa. Kila wanapobeba paspoti ya Tanzania wanaonekana wauza unga. Nakumbuka Rais, umewahi kutamka hadharani kwamba unayo majina ya wauza madawa ya kulevya lakini kwa bahati mbaya uliamua kuwa kimya. Rais, Kikwete, kwenye kampeni ya Chama Chetu, 2010, hawa wauza unga kwa kiwango kikubwa walichangia kampeni zetu na kutupatia ushindi mkubwa. Licha ya kwamba walitusaidia, mheshimiwa rais, madhara wanayoleta katika taifa hili ni makubwa kiasi kwamba hauwezi tena kuyafumbia macho. Wauza madawa ya kulevya wanakuwa na nguvu za ajabu ndani yah ii nchi. Wanamiliki majumba makubwa humu nchini. Biashara nyingi na kubwa ni zao. Kila sehemu kwenye uchumi wetu wamo. Ni bora ukachukua hatua na kuwashugulikia kisheria kabla hawajaliyumbisha taifa.

Ushindi 2015 kuna wauza unga wana tenda za kutoa huduma sehem nyeti sana za nchi hii
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom