Rais Kikwete; Kaza Mkanda, Bana Matumizi, Punguza Ukubwa wa Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete; Kaza Mkanda, Bana Matumizi, Punguza Ukubwa wa Serikali

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Mar 27, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mheshimiwa Rais Kikwete,

  Leo hii nakuja na ushauri kwako, tena ukiamua kukaa chini na kutafakari, yawezekana ukaleta mabadiliko makubwa sana ya kuifanya Tanzania iwe fanisi na kupiga hatua kujinasua kutoka umasikini.

  Mheshimwa Rais Kikwete, nakusihi Ukaze Mkanda, Bana Matumizi na Punguza Ukubwa wa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania.

  Serikali yetu na mfumo wake ni kubwa sana na haina ufanisi na ni gharama kubwa kwa Taifa letu. Kwa maoni yangu, asilimia 45 (45%) ya Serikali ya Tanzania na Taasisi zake (ikiwa ni Serikali Kuu, Wizara, Idara, Mikoa, Wilaya na Taasisi nyingine) ni mzigo ambao hauna manufaa na ni gharama zisizo la lazima. Nasema sehemu hii inatokana na kuundwa kwa mfumo huu kwa kutumia Usiasa zaidi na kuridhishana na si kutafuta Ufanisi halisi.

  Kama unataka ufanisi na kuimarika kwa utendaji, kinachohitajika ni Uimara kutoka kwenye uongozi wako na Viongozi na watu unaowapa dhamana ya kufanya kazi hiyo. Ufanisi na Maendeleo yatapatikana kama utakuwa mfuatiliaji mzuri, mchapa kazi na mwajibishaji bila woga kwa wale wanaoshindwa kufanya kazi kwa kufuata malengo, maelekezo na kutumia bajeti vizuri.

  Si suala la Ufisadi, au matumizi mabaya pekee ya fedha kuwa yakisahihishwa basi tutaanza kupiga hatua mpya au tutapata fedha na uwezo wa kupiga hatua za kimaendeleo.

  Tatizo letu ni Unene na Ubwanyenye wa kunona wa Serikali yetu ambako kunatufanya tuwe dhaifu, wavivu, wazito na kutegeana.

  Angalia kama inavyojulikana, mtu mwembamba ni mwepesi mwenye uwezo wa kufanya mambo kwa haraka na ufanisi bila kuchoka, lakini mtu mnene kwanza ni mvivu, anafanya mambo pole pole, anapumua kwa shida na kila mara ni mwepesi kuugua na huishia kujiliwaza kwa kuendelea kunenepa na kula kwa ulafi akidhani kuwa akiongeza mlo, basi matatizo yatajipotelea.

  Wewe ulikuwa mwana michezo, wasifu wako unasema ulikuwa mwanamichezo mahiri. Nafikiri utakubaliana nami kuwa staha yako ilikuruhusu si siku zile tuu, bali mpaka leo hii kuwa na siha ambayo inakuruhusu kukimbia bila kuchoka, kwa furaha na ukimaliza kufanya mazoezi una nguvu na upeo mzuri wa kufanya kazi na hulemewi na uchovu. Sasa ukiangalia mtu Kibonge, najua jibu unalo, mtu huyu ni goigoi, anategemea watu wengine wamsaidie au wafanye kazi kwa niaba yake na kwenye timu, mtu huyu kila siku yeye ni wa mwisho kwa maana hajiwezi, unene unamumbua na mbaya zaidi mtu huyu kila siku anavyoendekea kuwa mnono, ndivyo anavyoongeza uwezekano wa yeye kupata shinikizo na kuanguka chini puu, marehemu!

  Sasa Serikali ya Tanzania ni kama huyu Kibonge, Bongisa, Bwanyenye ambaye akitembea tumbo, mat ako, mapaja, mikono na shingo vinanesanesa vikiwa vimejaa mafuta makubwa na hata uwezo wa kufanya kazi au kuaminiwa kuwa atafanikiwa ni haba. Unene wa Serikali yetu, kama vile unene wa Mwanadamu, ni wazi kuwa ni ziada isiyo na manufaa, ni ziada isiyo lazima na isiyo na ufanisi.

  Serikali yetu imeiga mfumo wa Kikoloni, na hicho kilifanywa na Mkoloni ili kutudhibiti. Lakini sisi tumeendeleza utamaduni huu na hata kuufanya ni jambo la kisiasa na bila kufikiria, tumekuwa tunatumia pesa zaidi kujishibisha kwa kuipanua Serikali eti tukidai tunaongeza na kusambaza huduma za maendeleo kila kona.

  Ukweli ni huu Mheshimiwa Kikwete, tatizo la sisi kushinda kupiga hatua za kimaana kimaendeleo ni kutokana na ukosefu wa Tija na uongozi Imara ambao uko tayari kufanya kazi kwa bidii na maarifa, kama vile mkimbiajiwa mbio ndefu anavyoweza kimbia kwa masaa mawili, sawa na mkimbiaji wa mbio fupi anayeweza kimbia mita 100 kwa Sekunde 9!

  Tuna Mawaziri na Wizara nyingi kupita kiasi na hazina ufanisi. KUna makatibu wakuu wengi lakini hatuoni uwajibikaji. Tuna Wakuu wa Mikoa na wilaya ambao nao wamepewa wasaidizi wengi kwa majina ya Wakurugenzi, Waratibu na hata Wabunge, lakini kinachoishia ni matumizi kuongezeka lakini hakuna manufaa wala ufanisi.

  Kama tukipunguza ukubwa wa Serikali yetu kwa asilimia nilizozipendekeza kwako hapo juu, basi bajeti na fedha ambazo zimeendelea kutumika kulea unono maiti wa Serikali, zingetumika kwa kupeleka maendeleo na huduma kwa wananchi, iwe ni Afya, Elimu, Maji hata kuboresha Miundo Mbinu.

  Punguza Wizara, punguza Mawaziri, punguza Manaibu, punguza Makatibu na Wakurugenzi. Wazungu wanasema "Consolidate", basi unganisha chini ya mwamvuli mmoja na kuwa na watu maalumu kusimamia kila nyanja na utakayemteua kuwa kiongozi mkuu wa idara au wizara, ni bora ajue kuchapa kazi na si talalile na kubembea. Nawe uwe makini kumpumulia mtendaji huyu kwenye shingo yake, ukimdai ripoti na matokeo chanya. Wala usimruhusu akatumia madaraka au fedha kinyume na fungu au kilichopangwa.

  Tena watendaji hawa usiwape madaraka wafanye kazi tuu, bali wajue kujibana na kuweka akiba na si kufuja kila senti kisa fedha zipo!

  Punguza utitiri wa Watendaji wa Mikoa na Wilaya! hakuna maana ya kuwa na kivuli cha kila cheo kutoka Waziri Mkuu, Mkoa na Wilaya! Huku ni kuongeza matumizi yasiyo na maana. Leo kuna DC, DDD, DEO, DRD, na DDDDDD kila sehemu sawa na RC, RDD, RAO, na RRRRR nyingi.

  Kila kazi na cheo tunachokitengeneza, kinahitaji mshahara, gari, nyumba, marupurupu, watumishi na mambo megine mengi tuu. Hayo ni gharama hasa ukizingatia kuwa mfumo huu tumeutumia tangu tupate Uhuru na hatupigi hatua kama Taifa bali kama wateuliwa wa nafasi hizi, tunapata maendeleo kibinafsi ya kuwa matajiri, lakini Taifa linazidi kukwama kwenye tope la mfinyanzi wa Umasikini!

  Hata Ubunge, nao tumeufanya ni suala la kuzidiana kura na si suala la kuleta maendeleo. Hivi kwa nini kuna wilaya ambazo zimemegwa vipande na kuunda magharibi na mashariki?

  Je Iramba, Same, Rungwe, Arumeru na nyinginezo kama Kinondoni ilivyogawanywa kuwa Kawe, Ubungo na Kinondoni, zimeleta maendeleo gani ukifanya utafiti wa kina kama si kuongeza matumizi?

  Kama waliopewa madaraka na dhamana ya kuongoza wakati wilaya hizi zikiwa ni kitu kimoja si Magharibi, Mashariki, Kusini au Kaskazini walishindwa kazi na kuleta matunda, kwa nini waliendelea kuaminiwa kuwa iko siku watafanikiwa hasa kwa wale ambao wamekaa kama Wawakilishi na Watendaji zaidi ya miaka 20 na bado wanang'ang'ania eti wataweza kazi?

  Ni wakati wa kufanya mambo kisayansi na kuelekea katika mfumo wa kisasa kama vile uzalishaji mali ulivyoongezeka kutumia teknolojia ambako kumepunguza gharama na uwingi wa watu kufanikisha kazi.

  Hebu fikiria mishahara, nyumba, magari na marupurupu mengine, gharama za kiofisi, samani, na vifaa vya maofisi tunazozitumia kisa tuna watu wengi lakini hakuna ufanisi?

  Kazi ya wewe kuratibu na kupunguza Serikali tena sasa hivi itakuwa ni Rahisi! Tuna Kompyuta na mtandao wa kompyuta ambao utafanikiwa pindi huu mkonge wa nyuzi optiki ukikamilika na hata ule mradi wa Vitambulisho vya Taifa.

  Naomba ulitafakari hili unapojiandaa kuanza ngwe yako ya pili ya Utawala (nasikitika kukubali huna mshindani iwe ni ndani ya chama chako CCM au nje kupitia Upinzani mpaka dakika hii nikikuandikia salamu hizi) baada ya uchaguzi, basi uanze kampeni mpya ambayo itatumia sayansi kuboresha kauli mbiu yako ya Ari, Kasi na Nguvu Mpya!

  Wafundishe Watanzania kwa matendo kuwa tunaweza Kukaza Mkanda, Kubana Matumizi na kupunguza Ukubwa wa Serikali na kupata mafanikio hata yakatiririka katika nafsi zetu kama mtu mmoja mmoja, familia na jamii kwa ujumla.

  Kama Obama alivyosema "ndiyo, tutaweza" naamini nawe ukiwa na nia ya kizalendo bila woga au kujishuku na kutokujiamini, nawe utaweza pamoja na mapingamizi utakayopata kutoka kwa wale kupe, mbung'o na hata mchwa kama Mzee Mwinyi alivyotuambia majuzi ambao ni wanyonyaji na wamezoea vya kunyonya na vya urahisi na ndio maana wamenenepa kupita kiasi na kila siku wana mashinikizo na viugonjwa vinavyowalazimu kuiacha Muhimbili na kukimbilia India Bondeni na Ulaya Ulaya kwa matibabu.

  Mchungaji anakuambia Mheshimiwa, kama Mwalimu Nyerere alivyosema na kutukumbusha, Uwezo tunao, Sababu tunayo, je mwenzangu utajumuika na kuwa na Nia hii ambayo ninayo? Waswahili walisema penye Nia kuna Njia!

  "Ndiyo, Tutaweza" Yes, We Can!
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Jinsi ambavyo serikali ilivyo pesa karibu zote zinaishia kwenye utawala tazama mambo ya structure wa mfumo wa serikali kuanzia local government mpaka central government hapa ndio kuna tatizo. Ndio maana CHADEMA wanasema kuwa wanataka mfumo wa Majimbo. Ila itakuwa ngumu kwa CCM kubadili maana mfumo huu unawanufaisha wao na watoto zao na jamaa zao
   
 3. JM Aristotle

  JM Aristotle Senior Member

  #3
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah! Nimeusoma huu ushauri wote, tena kwa kina.
  Kwa kweli umenigusa sana, na sikuwahi kufikiria kabla kuhusu hili.
  Natamani hata, ungekuwa mshauri wa raisi. Una mawazo mazuri sana.
  Endelea na moyo huohuo wa uzalendo. Who knows where you'll be tommorrow...
   
 4. n

  nndondo JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Asante msemaji umesema yote kwa kifupi na kwa uchungu, tatizo ninaloliona ni moja, ni pale ambapo kwa kifupi JK mwenyewe hasikilizi la mtu hasa la maana, tunayoona akiyatekeleza ni yale ya majungu tu na uswahili wa mtaani, hasa katika kugawa ulaji ni kama vile yuko kwenye rehersal, ama laboratory jamani this is very sad.

  Ninachoweza kuongezea tu ni kwamba hata kama itatokea maajabu atapunguza serikali basi pia quality ya watu anaowachukua ifanane na uwezo wao. Wole Soyinka amenena juzi juu uongozi wa namna ya kina kikwete, kwamba Africa inashindwa kujikomboa kwa kuwa civil service imajaa watu wasiostahili kuwa huko, hawana uwezo, hawajawahi kuwa nao, walishindwa tangu shuleni, na tunawajua, wameua mashirika, na tunawajua, wezi wanakashfa chungu nzima, na tunawajua, wameshindwa kimaisha, na tunawajua huko wameenda kuganga njaa, hata wenyewe wamekiri hivyo na tunawajua, sasa huyu mtu mmoja anayetumia madaraka yake kwa yeye binafsi yuko busy kujenga tabaka la watawala wasio na maadili wala track record, ana nini huyu? Haogopi hata Mungu? Anawachukuliaje watanzania? Tazama keshaona watu wake wamefikia ku doctor muswada pamoja na kwamba hauna maana, lakini kafanya nini? you name it.

  Bahati mbaya unachoongelea ni cha muhimu mno hata kwa mtu wa kawaida asiyekua Rais wa nchi, lakini mwenzetu na serikali yake hawana macho, macho yao yako kwenye nafasi za serikali na kupeana. Tuombe tu siku ya siku ifike mapema, hiyo ngwe ya pili ni ya kula tu, ndio tutegemee balaa juu ya nchi hii, kama hawakuweza kufanya kazi huko nyumba itakua sasa wakati wanajua wanatoka? Lakini hala hala, historia na shida za watanzania ziko juu yao,
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,438
  Trophy Points: 280
  Mkuu Rev wanasikia hawa? Sasa wanataka kuongeza idadi ya Wabunge kitu ambacho hatukihitaji sasa na kuna matumizi chungu nzima ambayo hayana maslahi na nchi hata kidogo lakini wametia pamba masikioni wanakula nchi tu. Tunaweza kabisa kupunguza gharama zisizokuwa za msingi kati ya 20 to 30% ya budget ya Serikali, tatizo tulilonalo hakuna aliyeweka maslahi ya nchi mbele wanataka kutumbua kadri wanavyoweza.
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Halafu hata wanachokifanya hakionekani
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni kwamba focus yao iko kwa Wawekezaji na kuomba misaada.

  Leo ho Ngeleja anatoa kauli kuwa tukitaka kuwa na mfumo mzuri wa Umeme tunahitaji pesa mara tatu ya uwezo wetu na bajeti yetu. Iwe alichosema ni sahihi au kuna makosa, kuna njia nyingi sana za kuliongezea Taifa uwezo wa kujitegemea na kutoa huduma.

  Tushapiga kelele kuhusu misamaha ya kodi, kurudia mikataba na kuongeza kodi kwa Wawekezaji. Hiyo ni solution moja.

  Solution zingine ni kuweka sheria kali kupigana na ufisadi, that is okay.

  Ninachomuomba Mheshimiwa ni Solution ingine ambayo ni nzuri zaidi na ya manufaa zaidi maana itatuondolea matumizi mabaya na kutuwezesha kufika pale tunapotaka na kuwa na uwezo wa kuwa na sheria kali na kanuni ambazo zitashirikisha kuondoa misaada, kufuta misamaha ya kodi na kupiga vita ufisadi.
   
 8. M

  Msee Lekasio Member

  #8
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Padri wangu... hata kama tungehitaji pesa mara kumi ya uweso wa bajeti yetu... sisi sio masikini... uweso huo tunao. Tatiso kubwa ni matanusi yasiyoendana na kipato chetu. Dheo nimesoma sredi moja inaedhesea eti bosi wa shirika dha nyumba dha taifa atapokea mshahara wa saidi ya shilingyi milyoni kumi na tanu. Karibu ningeshikwa na kifafa....

  Hata hifyo nimefarijika kwa mapendekeso yako yaliyojaa hekima japo hawatakusikilisa.

  Ni mimi
  Msee Lekasio Makusare
   
 9. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Msee Lekasio,

  Labda siku watu watakapoamua kuvulia uvivu wao na kuonyesha ghadhabu na hasira ndipo masikio na mioyo yao itasikia.

  Hata Biblia inasema nitaifanya mioyo yao iwe migumu, naam hawajui Siku wala Saa gharika litakaposhuka na damu kumiminika barabarani!
   
 10. R

  Renegade JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,770
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280
  Mkuu hawa watu hawajali chochote wanachoangalia ni kupeana ulaji tu. Gharama wanaijua basi.Hapa maslahi mbele, Ndo maana wanataka kucreate usultan Tanzania, we ngoja tuone kule Zanzibar Karume anaondoka hukawii kusikia Dr, Mwinyi, Si unaona jinsi JK anavyomleta RJK Kwenye ulaji. Tutasikia.
   
 11. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Msee Lekasio,

  Kwa lugha yako hii wanasiasa walijua wananchi wanaona shida sana mtu akiambiwa analipwa mil. 7, 10, 20... badala yake wakasema haya ngojatu-wa-fool wadanganyika.

  Basic Salary monthly _________________________2.0M, taxed
  Furniture Annually 24M, Monthly_______________2.0M, tax free
  Umeme hata usipotumia.______________________ 0.5M, tax free
  Simu nyumbani na ofisini______________________ 1.0M, tax free
  Ulinzi______________________________________ 0.5M, tax free
  Transport cost________________________________ 1.5M, tax free
  Safari za nje na kujirusha_______________________10.0M, tax free
  Vikosi kazi__________________________________3.0M, tax free
  Board meeting as member or technorat____________ 2.8M tax free
  Strategic, Status & Operational meeting____________2.4M tax free

  total __________________________________________25.7


  Kwa hiyo ndugu yangu heri uambiwe mshahara 15M kuliko kudanganywa kama mtoto mdogo... in fact hapo hajalamba dume, la mwezi wa sita kumalizia budget isirudishwe hazina.

  Mshahara ya 15M kwa CEO wa kampuni kubwa kama lile ni mshahara wa kawaida... na kwa kweli ukimpa M.5 ujue atajilipa 50M. Na yeyote anayekubali kulibwa chini ya 10M ni mbabaishaji na asiruhusiwe kushika hilo kampuni.
   
 12. S

  Selemani JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2010
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Good post kaka. I shared this we so many folks. A massive government which is incredible inefficient when comes to collect revenues ni mzigo sana. The irony is that kila siku tunasikia wilaya mpya na majimbo mapya--I'm sitting wondering do these folks really get it?

  Anyways--moving forward there are few challenges. You can trim the government but hapa bongo that means you have to improve technology and make civil servants more productive. We need new guidelines for government workers, moving away from kujuana and hire folks who are actually educated. Because a small government needs efficient workers.

  Halafu, if we are going to trim the government then we ought make sure we have policies that are friendly for growth of public sector especially small business (SIDO can be instrumental). Currently I don't think we have capacity for that.

  Pia, there will be massive opposition from status quo and the union of government workers. Cutting down the government wouldnt be easy because there are people striving in this bureaucracy and they wouldn't let go easily. Where else you can get a weekday, 9 to 4 job with holidays paid off and an hour lunch break? Only in serikali ya Tanzania.

  Mwisho, I think we need a leader that understands the contents of Global economy system. And 2015 Presidential prospects as of now are disappointing (we need to recruit some people I guess). I definitely think 2015 is the most important presidential election in the history of our country. That if we need to be serious about improving the lives of our fellow countrymen.
   
 13. S

  Sheba JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni ushauri mzuri. Ni rahisi kushauri hivyo, ni vigumu kutekeleza ushauri wenyewe. Nchi yetu bahati nzuri sana haina upungufu wa washauri na wadadisi....ina upungufu mkubwa wa watendaji na watekelezaji.

  Ni maoni yangu kuwa tatizo letu kubwa ni tatizo la kimfumo....mfumo unazaa matatizo mengine nyemelezi moja wapo likiwa ni ukubwa wa serikali. Kimsingi watanzania wanakubaliana sana na hoja ya kuwa serikali ni kubwa na upo ulazima na fursa kadhaa za kuipunguza. Changamoto kubwa ni namna ya kupunguza serikali yenyewe bila kuwa na athari kubwa katika maendeleo na misingi na nguzo zinazoshikilia nchi.

  Rev Kishoka na wengine wengi waliochangia wameangalia zaidi kigezo cha gharama. Sina ubishi katika hilo. Tatizo ninalopata ni kuwa ukubwa wa gharama huu unalinganishwa ama kupimwa kwa kigezo kipi? Ninavyofahamu ni kuwa, baadhi ya mambo yanaweza kuwa na gharama kubwa kifedha lakini yakawa na faida kubwa kithamani. Mathalani, kuendesha JKT kumedaiwa kuwa ni gharama kubwa na likafutwa......lakini leo tu mashahidi wa madhara makubwa zaidi yaliyotupata kutokana na kufuta JKT kuliko gharama ambayo tungelipia. Tumeua uzalendo, tumeua maadili ya taifa, tunajenga kwa kasi matabaka na tumeondoa ukakamavu na 'sense of responsibility' kwa taifa. Eneo lingine ambalo tumewahi kulipuuza kwa kukwepa gharama huko nyuma ni elimu. Tumejenga shule za kata kwa kisingizio kuwa ni gharama kubwa kuendelea na mfumo wetu wa zamani wa wanafunzi kutoka mkoa mmoja kupelekwa kusoma sekondari mbali na makwao. Mfumo ule ulitujengea utaifa, ukawezesha kuoleana na muingiliano wa makabila na dini. Huko tunakokwenda shule za kata zinaturudisha kwenye ukabila (Ukata) na kupelekea vijana kutochangamana.

  Kwa mantiki hiyo, pamoja na gharama kubwa, mfumo wetu unatuwezesha kutujengea utaifa. Natambua idadi ya Baraza la Mawaziri ni kubwa kwa kuwa pamoja na mambo mengine linazingatia kupata mawaziri kutoka kila mkoa. Lakini pia, ukubwa wa serikali unatokana na ukubwa wa Chama Tawala. Tukumbuke kuwa CCM kilikuwa Chama pekee na kilishika hatamu, kikatengeneza mfumo kama Serikali ambao umetuunganisha wote kama taifa. Tumepaki magari CCM na kwa muda mrefu tumetumia Mabalozi wa CCM wa nyumba kumi katika kuhakikisha usalama wa maeneo yetu na kuunganisha Seriklai na wananchi wake. Haya yote yanaweza yasiwe na mantiki sana leo katika mfumo wa vyama vingi. Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa yametusaidia sana kutujenga kama taifa, ukizingatia kuwa nchi hii ina makabila yapatayo 120, dini kadhaa na ukubwa wa karibu Kilomita za mraba milioni 1. Baada ya mfumo huo kukamilisha dhima yake ya kutuunganisha, ubunifu unatakiwa wa namna ya kukifanya Chama Dola nje ya mfumo wa Chama Kimoja kujiunda upya. Kigugumizi kinakuja, Je, makada wa Chama watapelekwa wapi baada ya kutumikia chama muda mrefu kama si kupewa u- DC katika wilaya?

  Kwa kumalizia, narejea tena msimamo wangu wa awali kuwa ushauri wa Rev Kishoka ni mzuri. Ila Kishoka na wengine wataisaidia zaidi nchi yetu kwa kushauri namna nzuri ya kupunguza ukubwa wa CCM, kisha tuone namna bora ya kupunguza ukubwa wa Serikali katika namna ambayo haitaathiri sana umoja, utaifa na usalama wetu. Katika hili ushauri wangu ni kuwa tusiangalie gharama pekee bali pia thamani inayopatikana kwa kupunguza gharama hiyo. Hii itasaidia kuepusha kufanya maamuzi kama ya kufuta JKT au kubinafsisha viwanda hata vile vya msingi kwa kisingizio cha gharama za uendeshaji bila kuzingatia thamani inayopatikana kutokana na gharama hizo.

  Udumu Rev. Kishoka
   
 14. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kaka Sele,

  Shukrani ndugu. Mara nyingine solutions tunazo lakini tunazikalia kama vile Mzee Mwinyi alivyosema uchumi tumeukalia.

  Ukweli ni kuwa hili ni eneo ambalo Wanasiasa wengi hawalioni kama ni muhimu kupunguza matumizi na kutumia mbinu za kisasa kujiendesha.

  Ndio maana utakuta tunabadilisha viongozi wakuu, lakini kama huku ngazi za chini watu bado ni goigoi na wanajiburuza, tunaingia gharama nyingi zisizo na msingi kisa tumpunguzie mtu majukumu kazidiwa. Kama kazidiwa tupime je ni kutokana na mtu huyu kutokuwa na uwezo, ni mbangaizaji, mvivu au mzembe asiyewajibika?

  Sheba,

  NI lazima tuangalie ni vitu gani vya muhimu tutumie pesa na vitu gani si vya muhimu. Kupunguza Serikali na ukubwa wake inabidi kupima tunachopunguza, umuhimu wake, njia tofauti (alternative), uwezo wa sekta binafsi kufanya kinachofanywa na Serikali, na tutachokipunguza fungu lake tutalipeleka wapi na tutapata mafanikio gani.

  Sasa hivi nitakutajia vitu kadhaa ambavyo vinahitaji vipewe kipaumbele cha hali ya juu; Afya, Elimu, Maji, Lishe, Miundo Mbinu na Mishahara ya watu.

  Tukipunguza matumizi hasa yale ya kuifanya Serikali kuwa mzalishaji na kuiacha Serikali iwe mratibu na msimamizi, utaona watu binafsi na sekta binafsi zikiamka na kufanya mambo ambayo hayakuwezekana kutokana na Serikali kujipanua kupita kiasi.

  Leo hakuna maana kwa Serikali kuendesha ATCL, huku tuna sekta binafsi ambayo inaweza kufanya huduma kama hizo. Kama vile tulivyoachana na KAMATA, ATCL inaweza kuachwa ikawa ni shirika huru na si la Serikali. Vile vile TRL, NASACO, THA, na mashirika mengine mengi ya umma.

  Hata ukija kwenye Mawizara, au Tawala za Mikoa (TAMISEMI) kuna utitiri mrefu wa kila cheo na kila kazi lakini ufanisi ni mdogo sana. Kinachoitajika ni consolidation, evalutation of priorities, delegating authority and find credible people who can deliver.

  Najua kudeliver kwa environment ya Tanzania ni very challenging, lakini inawezekana kama kuna nia na viongozi wasio kata tamaa!
   
 15. m

  miner Member

  #15
  Mar 29, 2010
  Joined: Dec 14, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rev Amani iwe na kwako pia !

  Ushauri wako maridhawa kabisa lakini sikio la kufa halisikii dawa, wala mwenye macho haambiwi tazama. Tatizo letu ni kupenda sifa tu.
  Nakumbuka vizuri lakini sikumbuki ni gazeti gani nilisoma wakati Mustafa Mkulo anawasilisha mapendekezo na sura ya bajeti ya 2009/10 Matumizi ya kawaida ni kama trillion 6 Mapato ya ndani ni trillion 5 kwa hiyo mapato yanayokusanywa hayatoshi hata kuendesha serekali achilia mbali fedha za maendeleo maana yake nini maendeleo yetu yanategemea wahisani tumewapa jina zuri tu Devolpment Parterns kisha viongozi wetu kila kukicha ni kusafiri kuomba na kukopa si kwamba hawajui wanajua sana njia pekee ni kubana matumizi lakini ni wataka sifa kesho wanaongeza wabunge wafikie 360 kweli tunahitaji wabunge wengi kiasi hicho tena nusu yake wawe wanawake.

  Sina tatizo na wanawake hata kama watakua zaid ya 200 tunahitaji namba au uwezo hapa kinachotafutwa ni sifa tumefikiwa malengo ya millenia na matakwa ya wahisani na si vinginevyo maana malengo ya SADC tumeishafikia na tena wa kwanza, sifa tu bila kutazama uwezo wa kubeba mzigo huo kama Taifa.

  Wiki chache zilizopita Kamati za ushauri za Mikoa zilikutana kutoa mapendekezo ya kuongeza majimbo ya uchaguzi, kuanzisha Kata, Wilaya na Mikoa mipya kwa dhana ya kupeleka maendeleo kwa watu ni dhana njema nani anabeba gharama hizo ni yuleyule Mtanzania maskini kadri unavyoongeza ukubwa wa serekali unaendelea kumkamua maskini kubeba gharama

  Laiti viongozi wetu wangakua wabunifu wa vyanzo vya uhakika wa mapato na usimamizi mzuri na matumizi ya nidhamu ya pesa hakuna tatizo ni sawa na kisa kile cha watumwa waliotaka wawe huru wakapewa uhuru wakafurahi wakanywa nakucheza siku tatu njaa ilipowashika wakaenda kwa bwana wao kuomba chakula wakaambiwa si mlitaka uhuru chakula ni juu yenu kukitafuta wakalia na kuomba waendelee kubakia watumwa siku zote ili wapewe chakula hawakujua chakula unapata kwa kufanya kazi si kunywa na kucheza. Viongozi wetu waone aibu ya kuomba punguza matumizi ya serekali ushauri wa Rev si wa kupuuzwa hata kidogo.
   
 16. F

  Froida JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  @Rev ,Kishoka ,Ukweli nimependa ulivyonyambulisha ushauri wako Kwa Raisi Kikwete,Lakini ninavyoangalia kwa ndani toka afanye kazi ngazi ya Uraisi ni mtu aliyepoteza muelekeo kabisa,na ameonyesha kuwa ni mtu asiyejali matumizi ya serikali kwa kutumia fedha za walipa kodi,na matumizi yasiiyo naulinganifu na maisha ya mtanzania wa kawaida.Kutokana na matatizo tuliyonayo kikatiba hili tatizo litakuwepo kwa muda mrefu kama watanzania hatatutakataa na kusema inatosha sasa,kwa sababu katiba inaruhusu kiongozi yeyote wa uraisi kuchezea nafasi na kuunda kwa kiasi atakacho,hii inaleta usumbufu mkubwa sana kwa wananci mpaka leo kuna wizara nyingi nashindwa kuzitaja sawasawa kutoka na mabadiliko aliyoyafanya alivyoingia madarakani.

  Nina uhakika kama atapiata ataongeza au kupunguza kwa jinsi itakampendeza yeye ,hilo ni kosa kubwa la kikatiba,katiba inapaswa kubadilishwa ili kuwa na nidhamu na mienendo ya wataendaji ngazi ya uraisi pale anapoingia madarakani ,ukimpata mtu mwenye mashoga wengi kama Kiwkete ndipo hapo utakoishia kuwa na watendaji wengi wa ngazi za juu serikalini tuu kwa sababu kiongozi anataka kuridhisha wanamtandao wake.

  Lingine ni lazima kuwe na mfumo wa viongozi wote ngazi ya mawaziri ,manaibu viungozi wa taasisi za kiserikari kuthibitishwa na BUnge hii itapunguza sana Raisi kutwekea vimada vyake na marafiki zake tutakuwa na watendaji watakao jali maslahi ya taifa

  Kwa ushauri tuu huyu mwenzetu (Raisi sidhani kama anamsikiliza mtu angekuwa anasikiliza mambo mengi mpaka sasa yangekuwa yametengamaa,nadhani anayoamua yeye na anayoona yanamnufaisha yeye na chama chake anadhani yanawanufaisha watanzania wote,tuna kazi kwelikweli
   
 17. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Wabunge washaongezeana mikopo, ikifika mwezi juni wataoongezeana mishahara! Serikali inazidi kunenepeana!
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Apr 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  REv. Kishoka,
  Mkuu wangu unapigia mbuzi gitaa..hakuna kiongozi hata mmoja ndani ya CCM anaweza kukubaliana na mawazo yako -HAKUNA.
  majuzi tu nimeona wabunge wakijisifia wao kwa kutoa misaada ama kupelekea maendeleo ktk wilaya zao kwa fedha zao za mfukoni na hakika wabunge hawa wanapendwa sana na kupongezwa hadi hapa kijiweni..Sasa tujiulize hivi? hivi kweli hiyo ndio kazi ya Mbunge? mbunge anapopeleka maendeleo kijijini kwake kwa kutumia fedha yake ndivyo inavyotakiwa ama ndio tunawapa mwanya wa wao kutumia Takrima kupata kura za wananchi.. Iweje leo jamani kazi ya mbunge isiwe kuwakilisha wananchi bungeni ila ni kuwaondolea adha na matatizo yao kiasi kwamba mbunge anafikia kujisifia kwamba kuanzia saa 11 asusubuhi hadi jioni watu hujipanga mlangoni kwake kupata kuondolewa matatizo yao ya kila siku.. Tena basi kuna mbunge mmoja mama Ghama alifikia kujisifia kwamba mishahara na posho wanazopata sii kubwa hata kidogo kutokana na kwamba fedha zao nyingi hutumika kuwasaidia watu wenye matatizo..
  Sasa tunapopotosha manaa ya UBUNGE na kuruhusu watu kutoa michango yao kifedha na mali ktk jamii ili mradi wapate kuchaguliwa sijui nini faida ya wabunge kwenda bungeni! kwa nini tusiwachague matajiri kina Manji na Mengi wenye fedha tayari watatusaidia zaidi ya hao wabunge wanaosubiri posho zao kuwa ndio mtaji wa miradi ya jimbo...

  Haya kuna watu wanaomsifia hata Lowawengine wakidai kwamba Lowassa ni kiongozi mzuri mchapa kazi ambaye Tanzania inamhitaji... kweli unaweza amini maneno kama haya? kuna mtu aliniuliza kama nafikiri Pinda ni Waziri mkuu mzuri kuliko Lowassa..ajabu sana kana vile nchi yetu haina tena watu zaidi ya Lowassa. Nikamjibu kwa nini unafananisha Pinda na Lowassa na sio Lowassa na Mwanri, Mwandosya, Magufuli na wengine wengi tu ambao pia wana sifa za uchapa kazi?..

  Hivyo mkuu wangu sisi wenyewe akili zetu zimefungwa katika zizi la Ujinga. Tumekuwa kama kuku wa kienyeji walifungiwa usiku kucha ndani ya banda. asubuhi banda linapofunguliwa kutoka mkuku wakakimbia hovyo hovyo na huchua muda waka settle down na kujiona huru..Matatizo ya KIkwete ni matokeo ya upeo wetu sote ktk mitazamo mingi ya kisiasa na kiutawala...
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mawazo mazuri lakini umeangushia ndani ya sikio lililokufa. Halisikii hata dawa! Mawazo yake na vitendo vyake vinaashiria hivyo. Yuko tayari kumsikiliza yule ex ktibu tarafa anaitwa makamba lakini hawezi kusikiliza mambo ya kichwa kama haya!
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Unasema ukweli mzee wangu. Lakini uko wapi siku hizi tumemiss sana mchango yako mkuu wetu.
   
Loading...