Rais Kikwete Bado Anatusubiri Tukamwone

.
Napenda leo nitoe changamoto na ahadi kwa wasomi wetu hao, wenye fani mbalimbali kama vile kilimo, mifugo, uvuvi, uhandisi, ubunifu wa majengo, sheria, uhasibu na kadhalika. Katika dunia ya utandawazi na ushindani unaoambatana nao, Watanzania wasomi watabaki nje iwapo hawatakuwa wabunifu zaidi, wakaungana na kuanzisha kampuni kubwa za wazalendo.

Lakini wakikubali kuungana, na kuanzisha kampuni kubwa zinazoendeshwa kwa misingi halisi ya kibiashara, na sio ubabaishaji, Serikali, kupitia vyama vya taaluma zao, itawaunga mkono, itawasaidia na itawawezesha. Serikali ya Awamu ya Nne itakaribisha mawazo kutoka kwa vyama vya kitaaluma juu ya namna bora ya Serikali kufikia lengo hilo. Ninataka wasomi wetu wawe kiini cha wajasiriamali wasomi na wakubwa nchini.
Kwa maoni yangu, a deserving farewell kwa member wetu yoyote, aliyetangulia mbele ya haki ni kumuaga kupitia maandishi yake, threads zake ili kujikumbusha mawazo yake, maneno yake na matendo yake tukiendelea kuishi Tribute to Sanctus Mtsimbe: Sio tu ni smart kwa mavazi na muonekano, pia ni smart kwa mawazo, maneno, na matendo, na very smart upstairs!

RIP Comred Santus Mtsimbe, maandishi yako humu JF, yatakuishi milele!.

Umepigana vita vilivyo Vitakatifu,
Mwendo Umeumaliza, Imani umeilinda.

Bwana Ameleta, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.

Paskali
 
Back
Top Bottom