Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,032
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, AKIFUNGUA RASMI BUNGE JIPYA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DODOMA, 30 DESEMBA 2005
. . . .Uchumi Unaoshirikisha Raia Wengi
. . . .
Mheshimiwa Spika:
Serikali ya Awamu ya Nne itaongeza kasi ya kupambana na umaskini. Tutawezesha Watanzania kwa makundi. Kundi la kwanza ni la Watanzania wasomi, walio ndani au nje ya nchi yetu. Zamani ilikuwa mtu ukitoka Chuo Kikuu, kazi ya Serikali inakungoja. Leo hali si hiyo. Wengi inabidi watafute kazi kwenye sekta binafsi, au wajiajiri wenyewe.
Napenda leo nitoe changamoto na ahadi kwa wasomi wetu hao, wenye fani mbalimbali kama vile kilimo, mifugo, uvuvi, uhandisi, ubunifu wa majengo, sheria, uhasibu na kadhalika. Katika dunia ya utandawazi na ushindani unaoambatana nao, Watanzania wasomi watabaki nje iwapo hawatakuwa wabunifu zaidi, wakaungana na kuanzisha kampuni kubwa za wazalendo.
Lakini wakikubali kuungana, na kuanzisha kampuni kubwa zinazoendeshwa kwa misingi halisi ya kibiashara, na sio ubabaishaji, Serikali, kupitia vyama vya taaluma zao, itawaunga mkono, itawasaidia na itawawezesha. Serikali ya Awamu ya Nne itakaribisha mawazo kutoka kwa vyama vya kitaaluma juu ya namna bora ya Serikali kufikia lengo hilo. Ninataka wasomi wetu wawe kiini cha wajasiriamali wasomi na wakubwa nchini.
Tunapenda kwenda kumwona sasa kuhusiana na ahadi yake. Tupeane maoni ni kipi tunapenda Serikali ITUUNGE MKONO, ITUSAIDIE na ITUWEZESHE?