Ni sahihi Kabisa, Hatupaswi kubadili mitaala na kutumia kiswahili pekee. Dunia ya leo inazidi kuwa Kijiji. Tunapotaka kutumia Lugha yetu maana yake tunajiwekea mipaka sio kielimu pekee bali hata kiajira, kujiendeleza kimasomo nje, na kimawasiliano.
Pia kiswahili ni lazima kiwe kigumu kuliko kingereza kwa kuwa wanafanya kazi ya kutohoa tu maneno ya kingereza ikiwa ni pamoja na kuunda maneno machache, kitu ambacho kinakifanya kiwe kigumu zaidi.
Siku zote huwa najiuliza, kama ishu ni watoto kutoelewa kwa kizuizi cha Lugha, hebu tuangalie ufaulu wa somo la kiswahili. Ni mbovu kuliko hata masomo mengine ambayo yanafundishwa kingereza. Hivyo Lugha sio tatizo, bali tatizo liko katika mitaala pamoja na uimara wa walimu wetu. Hapa ndipo tatizo liliko.
Muda mwingine najiuliza, au wanafanya hivi kwa ajili ya kujiandaa na kampeni hapo Oktoba ili wapate cha kutueleza majukwaani?
Tuendelee kupiga kelele mpaka waelewe kuwa wanatupeleka kusiko.